Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)

Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)

Jibu: Turejee..

Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya FALME na MAMLAKA, juu ya WAKUU WA GIZA HILI, juu ya MAJESHI YA PEPO WABAYA katika ulimwengu wa roho”.

Hapa kuna vitu vinne, vilivyogawanyika katika sehemu mbili.. Kundi la kwanza ni “FALME na MAMLAKA” na kundi la pili ni “WAKUU WA GIZA na JESHI LA MAPEPO” jumla mambo manne (4)

Sasa hebu tuanze na kundi la kwanza la FALME na MAMLAKA.

Mwandishi (ambaye ni Paulo, Mtume wa Bwana YESU) alitumia mfumo wa Tawala za dunia, kutoa picha ya tawala za ufalme wa giza.

Katika Dunia tunajua kunakuwa na Falme za wanadamu… Kwamfano kuna Falme za kiafrika, falme za kiarabu, Falme za kiasia n.k,

Sasa kwa vizazi vyetu nyakati hizi mfano wa Falme ni hizi SERIKALI tulizonazo (ambapo kila nchi inayo serikali yake), lakini zamani za kale Falme zilibaki kuitwa falme..Kwamfano kwenye Biblia utaona kulikuwa na Ufalme wa Umedi na Uajemi, Ufalme wa Babeli, Ufalme wa Uyunani, Ufalme wa Rumi n.k.. Hizi zote zilikuwa ni falme na ziliongozwa na Wafalme.. kwahiyo katika ulimwengu kulikuwepo na Falme Nyingi, zenye wafalme wengi, lakini dunia ni moja.

Tusogee mbele zaidi..

Chini ya kila Falme (au serikali) kunakuwa na Mamlaka, kwamfano katika Serikali ya nchi ya Tanzania, kuna Mamlaka mbalimbali, kuna Mamlaka ya mapato (TRA), Mamlaka ya Maji safi na maji taka, Mamlaka ya mawasiliano, Mamlala ya Hali ya hewa, Mamlaka ya Elimu, Mamlaka ya bandari n.k, hivi vyote ni viungo vya Serikali kwaajili ya kuwahudumu walio chini ya Serikali/Ufalme.

Kwahiyo tunaweza kurahisisha kwa kusema mfano huu, “Vyanzo vya maji vyote vilivyopo katika UFALME wa Tanzania vipo chini ya MAMLAKA ya maji ya maji ya nchi hiyo”… au Ukusanyaji wa kodi za wananchi katika Ufalme/serikali ya Tanzania upo chini ya MAMLAKA ya Ukusanyaji mapato (TRA)….Au jukumu la Ulinzi wa raia na mali zao la Ufalme wa Tanzania lipo chini ya Mamlaka ya ulinzi na usalama kupitia chombo chake maalumu kiitwacho Polisi….Umeona huo muunganiko wa Ufalme na Mamlaka?.

Na kawaida kila Mamlaka inayo Wakuu wake na jeshi.. Ndio hapo utasikia “Mkuu wa mamlaka ya mapato” au Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano,  na jeshi zima la mamlaka hiyo ni wafanya kazi wote waliopo chini ya mamlaka hiyo..

Na katika ULIMWENGU wa giza ni hivyo hivyo, kuna FALME na pia kuna MAMLAKA mbalimbali… Zipo mamlaka za uuaji na utekaji (mfano wa hizo ni zile zilizoruhusiwa kumkamata Bwana YESU (Soma Luka 22:53),

zipo mamlaka za uharibifu wa ndoa, zipo mamlaka za uharibifu wa huduma, zipo mamlaka za uharibifu wa familia, kazi n.k n.k,

Na kila mamlaka ya giza inayo Mkuu wake/Kiongozi ambaye ni Pepo (hao Ndio wanaoitwa wakuu wa giza)..  Hapa ndipo tunapofika katika kundi la Pili la WAKUU WA GIZA na MAJESHI YA MAPEPO.

Sasa kama kuna kiongozi au mkuu, ni wazi kuwa kuna Jeshi chini yake, (hakuna kiongozi/mkuu asiye  na jeshi la watu chini yake la kuliongoza)

hivyo mapepo yote yaliyosalia yanayofanya kazi chini ya Wakuu wa giza ndio wanatengeneza kundi la majeshi ya mapepo wabaya.

Kwahiyo Biblia inaposema kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali juu ya FALME NA MAMLAKA NA WAKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, imemaanisha kuwa tunapambana na wakuu wa giza (Wakuu wa mapepo) na majeshi yao ambayo yanatumia Mamlaka na Ufalme wa giza kupambana nasi.

Kwahiyo ufalme wa giza, imesimama katika ngazi zake, kuonyesha kuwa vita vyetu si virahisi kama tunavyovichukulia, kupambana na falme si kazi ndogo! Inahitaji msuli wa kutosha wa kiroho, maana yake ni lazima mtu uwe umesimama kwelikweli, umezama kweli kweli kwenye ufalme wenye nguvu kuliko huo wa giza.

Na hakuna ufalme mwingine wenye nguvu kuuzidi ufalme wa giza, zaidi ya UFALME WA MBINGUNI, ambao Mkuu wa Ufalme huo ni YESU KRISTO (Mwamba Mgumu). Huyo ndiye mwenye nguvu za kuuvunja nguvu zote za falme za giza, na hana namba mbili yake!..

Je unaye YESU moyoni na maishani?.. Kama hujaokoka fahamu kuwa upo chini ya ufalme wa giza na mamlaka za giza hata kama ni tajiri, au una afya au una mafanikio mengine yote, bado upo chini ya utawala wa giza, wanaweza kukufanya chochote kwa wakati wowote, na wanaweza kukutumia vyovyote watakavyo, Mgeukie YESU leo na uhame kutoka katika huo ufalme wa giza.

Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;

14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;

15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote”.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je mkristo anaweza akawa na mapepo?

Je! tunaweza kuwaamuru Malaika kama tunavyoyaamuru mapepo?

Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.

Wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale nguruwe. Akawapa ruhusa.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments