SWALI: Je ni kitu gani hasaa kilikuwa kinatokea mpaka wafikie hatua kama ile, je! Ni utahira ulikuwa unawapata au ni nini hasaa?
JIBU: Silaha mojawapo ambayo tuona Mungu alikuwa akiitumia kuwashindania watu wake mara myingi wawapo vitani, Ni hii ya “machafuko” yaani Ni kuwavuraga maadui washindwe kuelewana na hatimaye kuanza kushambuliana wao kwa wao.
Kwamfano wa matukio kama hayo tunaweza kuyathibitisha katika habari hizi;
Wana wa Israeli Walipoizunguka Yeriko.
Waamuzi 7:22
[22]Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuendelea Serera, hata mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.
Sasa tuone ni njia zipi alikuwa anazitumia Mungu mpaka wauane wao kwa wao, watu ambao walikuwa wamekubaliana kabisa kwenda vitani?
Hii ni hali ya kutoweza fikiri vema, kuwa kama mtu fulani nusu aliyerukwa na akili.
Kumbukumbu la Torati 28:28
[28]BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
Hii ni hali yakutokuwa sawa katika ufahamu, unamwona mwenzako kuwa ndiye adui, na hatimaye vita vinaanza kabla hata ya maadui wenyewe kufika..hili ndio yamkini Bwana alilowapiga watu wa Yeriko.
Kama tu vile Mungu alivyowapiga upofu watu wa Sodoma na Gomora wasione mlango wa Lutu, vivyo hivyo hawa wanapigwa katika eneo la fikra wasifiri vema wauane, wao kwa wao.
Hii ni namna ambayo mnapisha usemi. Kiasi kwamba hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake, huyu anataka hili, Yule hili, kila mmoja haafikiani na mwenzake hatimaye chuki inatokea, matengano na mwisho kuanza kupigana wao kwa wao.
Watu wa Babeli walipigwa ‘usemi’ isipokuwa tu wao hawakufikia hatua ya kuuana, lakini ni namna tu hii hii .(Mwanzo 10)
Hii ni hali ya kuwashuku wenzako kuwa ni wasaliti, hivyo ghafla kupoteza imani nao, na kuanzisha vita ili kujilinda…mfano wa hili tunaliona kwenye ile vita ya Yuda na majeshi ya wamoabu, waamoni na wameuni walipokutanika kupigana na taifa la Mungu..ghafla moabu Na amoni wakaipiga Seiri, halafu baadaye wakarudiana Wao kwa wao.
2 Mambo ya Nyakati 20:22-23
[22]Nao walipoanza kuimba na kusifu, BWANA akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa.
[23]Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe.
Hii ya visasi inatokeaje?
Labda mmoja alikuwa na chuki na mwenzake, hivyo unamlipizia kisasi, na huyu naye kaona ndugu yake kauliwa anaamka kumtetea, mara kabila hili na hili hatimaye taifa zima linaiingia katika kujiharibu.
Hivyo Mungu anapotaka kutupigania, silaha hii huwa anaitumia hata katika agano jipya hususani hapo kwenye kugonganisha ndimi.
Kwamfano mtume Paulo alipokamatwa awekwe barazani ili ahukumiwe…kwa hekima ya Roho alipewa kujua kuwa katikati ya baraza wapo mafarisayo na masadukayo. Hivyo alilolifanya ni kuwachonganisha ndimi, badala ya kumshambulia yeye..wakaanza kushambuliana wao kwa wao…hiyo ni silaha ya Bwana ambayo kwa hekima ya Roho aliitamka..
Matendo ya Mitume 23:6-7
[6]Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.
[7]Alipokwisha kunena hayo palikuwa na mashindano baina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukafarakana.
Ni vema kufahamu aina hii ya silaha ni mbaya kuliko ile ya kushindana na adui yako.
Lakini ni vema kufahamu kuwa hata shetani hutumia silaha hii, pale tunapotoka nje ya mpango wa Mungu.
Israeli iliingia kwenye vita vya wao kwa wao, na kupelekea mauaji mengi sana…
Ni nini kilitokea?
Baadhi ya wana wa Benyamini waliendekeza dhambi ya uasherati mpaka ikafikia hatua inayokaribia ile ya sodoma Na Gomora na Israeli yote ilipopata taarifa, wakataka wawatoe hao watu wauliwe, lakini wabenyamini wakawaficha kwasababu ni watu wa kabila lao. Machafuko yakaanzia hapo, hatimaye wakauana Sana. (Waamuzi 19-21)
Hata sasa silaha hii shetani hupenda kuirusha kwenye kanisa la Mungu, watu wapoteze upendo na utakatifu ili waanze kulana na kung’atana..kwasababu ya wivu, visasi na vinyongo.
Wagalatia 5:14-15
[14]Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
[15]Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.
Lazima tuijue hila hii ya shetani na kukataa kuipa nafasi.. Na Bwana atatuhifadhi, na matokeo itakuwa ni yeye kuleta machafuko kwa maadui zetu wanaposimama Kinyume na sisi.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je mapepo yanakufa? Na kama hayafi, tunashindanaje vita vya kiroho?
About the author