SWALI: Nini maana ya Mithali 21:3
[3]Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
JIBU:
Mstari huo unatufundisha mambo ambayo Mungu huvutiwa nayo zaidi…
Mungu hupendezwa zaidi na sisi tunapoishi maisha ya haki, tunatenda mema, tunawajali wengine, tunaishi sawasawa ni viwango vyake vya kiroho hapa duniani..kwake hiyo ni bora zaidi ya sadaka zetu tumtoleazo.
Sadaka huwakilisha mambo yote Ya kidini tunayoweza kumfanyia Mungu, mfano ibada, fedha, mifungo, maombi, kuhubiri, kuimba n.k
Bwana huvutiwa zaidi na mioyo na tabia zetu, na sio zile Ibada za nje tu..
Haimaanishi kuwa hapendezwi na hivyo vitu hapana…bali hivyo vifanywe baada ya kutii kwanza..
Tunaona jambo kama hilo amelisisitiza sehemu nyingi kwenye maandiko; Tukianzia kwa Sauli alimwambia, hivyo;
1 Samweli 15:22
[22]Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Mika 6:6-8 inasema;
[6]Nimkaribie BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja?
[7]Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?
[8]Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
Soma pia..
Isaya 1:11-17 – Inasema…Bwana huchukizwa na sadaka za watu wanaishi katika dhambi
Hivyo ni lazima tujiulize Je! tunatenda haki kwa wengine?
Je! Tunatembea kwa unyenyekevu mbele ya Mungu wetu?
Je! tunamtii Mungu, kuliko vitu vingine vyovyote?
Je tunawahurumia wengine…?
Mambo kama haya ndio yenye uzito zaidi kwa Mungu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Maana ya 2Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote
About the author