VAA MAVAZI SITA YA NDANI.

VAA MAVAZI SITA YA NDANI.

Yapo mavazi ya nje na yapo mavazi ya ndani… Mfano wa mavazi ya nje ni haya tunayoyavika juu ya miili yetu (kanzu, suruali, kitani n.k) haya kazi yake ni kuusitiri mwili katika heshima, na ni lazima tuvae mavazi ya kujisitiri..

Lakini pamoja na hayo yapo mavazi ya ndani, ambayo ni ya muhimu sana, na yanamaana kubwa sana zaidi hata ya nje, na haya ni lazima tujivike, kwamaana kama tukijivika vizuri mavazi ya nje, halafu ya ndani tukayakosa, tutakuwa tuna kasoro kubwa sana.

Sasa hetu tujifunze mavazi hayo ya ndani ni yapi…

Wakolosai 3:12 “Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa REHEMA, UTU WEMA, UNYENYEKEVU, UPOLE, UVUMILIVU,

13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

14 Zaidi ya hayo yote JIVIKENI UPENDO, ndio kifungo cha ukamilifu”.

Hapo Biblia inatumia neno “JIVIKENI” Ikiwa na maana kuwa mambo yafuatayo yanafananishwa na mavazi.. na anayataja pale kuwa ni moyo wa Rehema, Utu wema, Unyenyekevu, Upole, Uvumilivu na mwisho anamaliza na Upendo, tutazame moyo baada ya lingine.

    1. REHEMA.

Hapo anataja moyo wa rehema,  Mtu mwenye moyo wa rehema wakati wote atajishusha mbele za Mungu, na kujitakasa, kamwe hawezi kujiona ni bora mbele za Mungu, na pia mtu mwenye rehema siku zote atakuwa ni mtu wa kuwarehemu wengine, kuwasamehe na kuachia, kwahiyo nasi hatuna budi kujivika moyo huo wa rehema kila siku.

    2. UTU WEMA.

Hapa anasema “Utu” maana yake ni “jambo la ndani” sio nje. Mfano wa Utu ulio mwema ni ule aliokuwa nao Yule Msamaria, ambaye alimwona mtu Yule kaangukia mikononi mwa wanyang’anyi akaenda  kumsaidia kwa moyo wote Luka 10:30-37. Nasi lazima tulivae hili vazi la Utu wema (2Wakorintho 6:6)

    3. UNYENYEKEVU.

Unyenyekevu ni hali ya kujishusha,  na kinyume cha unyenyekevu ni kiburi na majivuno, ili tuhesabike tumesitirika kiroho ni lazima tujivike vazi hili la unyenyekevu 1Petro 5:5.

     4. UPOLE.

Anasema “Upole” na si “Unyonge”.. Unyonge ni ile hali ya kuwa mtulivu kwasababu ya hofu, au hali Fulani..lakini upole ni hali ya kuwa mtulivu si kwasababu unashindwa kurudisha majibu au kufanya jambo..uwezo wote unakuwa unao lakini hufanyi hivyo, kama alivyokuwa Bwana wetu Yesu, yeye alikuwa na uwezo wa kushusha moto kwa wasamaria lakini hakufanya hivyo.. nasi ni lazima tujivike hili vazi. (Mathayo 11:29)

      5. UVUMILIVU.

Uvumilivu ni uwezo wa ndani wa kustahimili jambo baya, laweza kuwa shutuma, mapigo, au jambo jingine lolote, uwezo huo ni muhimu sana sisi wakristo kuwa nao.

Yakobo 5:10 “Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.

11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma”.

     6. UPENDO.

Hapa anasema kuwa hiki ndicho kifungo cha ukamilifu.. Maana yake tukiwa na upendo ni sawa na mtu aliyevaa shati sasa anamalizia kuvaa koti juu yake na kufunga vifungo vyake, na tena Biblia inasema pasipo upendo sisi si kitu haijalishi tunanena kwa lugha au tunafanya ishara (1Wakorintho 13:1).

Kwahiyo hayo ndio mavazi tunayopaswa kuyavaa katika utu wetu wa ndani kila siku, na utaona pia yamerudiwa katika Wagalatia 5:22 kama matunda ya roho, na mengine baadhi kuongezeka.

Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TUNZA MAVAZI YAKO NA FUA NGUO ZAKO!

VAA MAVAZI, USIVALIE MAVAZI.

USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!

WALIYATWAA MAVAZI YAKE, WAKAFANYA MAFUNGU MANNE,

JINSI MATENDO YA IMANI YANAVYOWEZA KULETA UTAMBULISHO MPYA KWA MTU.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments