Ikiwa wewe ni mwanandoa, ni busara kuwa na maombi yako maalumu kwa ajili ya ndoa yako.
Waweza kutenga siku kadhaa katika wiki, au mara mbili katika wiki, kuwa na maombi maaalimu marefu kwa ajili ya ndoa yako.Â
Maombi ni nyenzo muhimu katika kuendesha na kufanikisha sehemu zote zamaisha yetu, huduma inahitaji maombi, kanisa linahitaji maombi, taifa linahitaji maombi, wewe unahitaji maombi, vivyo hivyo na ndoa yako pia inahitaji maombi ili iwe na ustawi Bora katika nyanja zote..hata kama huoni tatizo lolote ndani ya ndoa ..bado unahitaji maombi sana.
Â
Kwanini maombi? Ni kwasababu njia pekee ambayo Mungu huweza kuyaingilia maisha yetu ili ayatengeneze vema basi ni kwa njia ya maombi.
Â
Ndoa inaweza ikadumu lakini isiwe na amani, ndoa inaweza ikawa na amani lakini isiwe na mafanikio, ndoa inaweza ikawa na mafanikio lakini imekosa Mungu, vilevile inaweza ikawa na umoja lakini imejaa wivu, inaweza ikawa haina shida lakini watoto wanaokuja wakawa na matatizo, inaweza pia ikawa sawa leo, lakini kesho shetani akaishambulia….Hivyo suala la kuombea ndoa ni jambo la muhimu sana.
Â
Huu ni mwongozo wa maeneo muhimu ya kuombea kila uingiapo katika maombi ya namna hii. (Kila kipengele tumia dakika 30)
Mungu alipomuumba mwanaume na mwanamke na kuwaleta katika ndoa aliwafanya mwili mmoja tena..Maana yake aliweka Muunganiko usiowezekana kibinadamu Wa umoja..
Mathayo 19:5
[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?Â
Â
Hivyo hakikisha unaombea ndoa yako Bwana adumishe umoja wenu, uwe umoja kwelikweli, na kamwe pasiwepo matengano. Maana huo ndio mwanzo wa ndoa thabiti
Omba kwa nguvu, huku ukivunja roho za matengano, ukiangalia zaidi maeneo ambayo unaona kabisa yanahatarisha umoja wenu, yenye dalili ya kutaka kuwaachanisha hayo ndio uyaombee zaidi, ikiwa ni kazi, au watu, au magonjwa, mwambie Bwana apatengeneze hapo..tumia si Chini ya dk. 30 kuombea eneo hilo moja tu.
Hivi viwili navyo ni nyenzo kubwa sana katika ndoa thabiti. Bwana aliagiza mwanamume ampende mke wake kama mtu apendavyo mwili wake mwenyewe.. vivyo hivyo aliagiza mke amtii mumewe Kama mtumwa kwa Bwana wake.
Â
Waefeso 5:22-25
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.Â
[23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.Â
[24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.Â
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;Â
Hivyo ikiwa wewe ni mke, mwombee sana mumeo Bwana alidumishe pendo lake kwako, lakini pia ikiwa wewe ni mume mwombee mkeo Bwana amjengee utii kwako.
Lakini pia jiombee wewe sawasawa na jinsia yako Bwana akuzidishie upendo na utii..kwasababu vyote hivi ni nyenzo kwa wote, vizidi bila kupungua nguvu kwa jinsi siku zinavyokwenda.
Â
Ndoa ikikosa maelewano hupoteza dira yake.
Â
i)Â Omba Mungu ajenge usemi mmoja yaani lugha ya maelewano kwanza katika eneo lenu la kiroho.. Maana yake wote msisimame katika Bwana (muokoke), ikiwa mmojawapo hajaokoka mwombee neema Ya wokovu, injili imchome abadilike na kumpokea Kristo, na huku ukimhubiria pia.
ii) Omba pia Mungu awape Maelewano Katika majukumu yenu ya kiroho(utumishi). Mfano ratiba za ibadaza nyumbani, maombi, mikesha, mifungo, ushuhudiaji, na utoajik.
Ikitokea mmoja wenu haafiki majukumu hayo, si rahisi mwingine kutekeleza na matokeo yake inakuwa ni kushindwa kutimiza lengo kuu la kindoa. Kumbuka mmewekwa katika ndoa ili mumtumikie Mungu pamoja..hivyo jambo hilo ni lazima Lipewe nafasi ya kwanza na kubwa katika ndoa.
iii) Lakini pia omba maelewano katika mambo Yote ya kimaisha.
Mfano mikakati ya kimaendeleo, matumizi ya kifedha, n.k. huku ukigusia Maeneo yako yote ambayo unaona mikwaruzano inatokea, Au dalili hizo kutokea..ukiharibu hivyo vyanzo kwa maombi yako.
iv) Lakini pia Bwana awajengee mioyo ya kusamehe na kuachilia.
Ndoa nyingi zimeingia dosari, kupoa hata kufikia hatua ya kuvunjika kabisa kutokana na kuwa zimepoteza mioyo wa kusamehe na kuachilia Kwasababu ya majeraha au makosa yaliyofanyika nyuma..
Wakolosai 3:13
[13]mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Mwambie Bwana sikuzote, wote mpewe mioyo ya kusamehe na kuachilia.
Hapa pia ni mahali pa kupaombea sana.. Wengi wanadhani wanaweza linda ndoa zao kwa kuweka sheria kali, kwa kufuatilia nyendo zao, kwa kuwavisha mavazi ya kuficha mpaka nyuso, Lakini uhalisia ni kwamba ikiwa mtu amekosa uaminifu, huyo kamwe halindiki, atakuzunguka tu, Hivyo omba kwa Bwana juu ya mwenzi wako, na kwako pia Bwana awaumbie moyo wa uaminifu. Hilo linatosha kuwa ulinzi mkubwa kwa ndoa yako.
Nyuma ya mafanikio ya kitu chochote chema, ni lazima utaona uvumilivu ulipewa nafasi, hata  huduma ya  kufanikiwa hutegemea uvumilivu. Ndoa haimaanishi kila siku itakuwa ni furaha tu, zipo nyakati za kupishana kibinadamu, za kusemwa vibaya, za kuudhiwa zipo nyakati za kupungukiwa, yapo madhaifu pia.. Hivyo omba moyo wa uvumilivu thabiti uwe juu ya kila mwanandoa.. kuanzia wewe mwenyewe.Ili nyakati ngumu zitakapopita pasiwe na wepesi wa kuiacha ndoa au kuchukua Hatua za madhara.
Ndoa ikikosa mwelekeo wa ki-Mungu huishia pagumu. Omba Mungu awape dira sahihi isiyo na majuto katika mikakati yenu yote ya kimaisha.
Omba Bwana ayanyoshe mapito yenu, awafanikishe, awaepushe na njia ya majuto na upotevu wa yule mwovu.. kwasababu maandiko yanatuonyesha ndoa ya kwanza ilivamiwa na uharibifu kwasababu ya udanganyifu wa ibilisi, kwa kitendo cha Hawa kusikiliza na kuifuata njia nyingine ambayo hakuagizwa na Mungu, na matokeo yake alipokula tu lile tunda ikasababisha matatizo makubwa ambayo mpaka sasa tunayaona ..
Mafanikio Ya ndoa hutegemea pia mahusiano mema kwa ndugu na wakwe..Musa alifanikiwa kuiongoza huduma vizuri kwasababu alikuwa na mahusiano mazuri na mkwe wake Yethro. Ruthu alifanikiwa kuolewa na Boazi mtu mkuu na mwenye uwezo kwasababu alikuwa na ukaribu na mama mkwe wake Naomi hata baada ya kufiwa na mumewe.
Vivyo hivyo na wewe pia uhusiano wako ukiwa mzuri na watu wa upande wa mwenzi wako unaharakisha baraka na neema nyingi za Mungu.
Lakini pia ikiwa mahusiano ni mabovu, basi ndio utumie fursa hii kuombea utapatanisho haraka, sana. Eneo hili ni muhimu sana kuliombea, ijapokuwa wengi hulipuuzia.
Ikiwa ni ndoa ambayo tayari inayo watoto ni muhimu kuwaombea watoto wako daima, wasiwe chanzo cha nyinyi kufarakana, lakini kuwa mwiba na uchungu kwenye ndoa yenu.
Lakini ikiwa bado hamjawa na watoto, ombea uzao wako ujao ukawe faraja na neema kwenu. Watoto wakiwa wabovu wanaweza kuihatarisha ndoa yako, au kuifanya isiwe na amani. Hivyo waombee sana wokovu, ulinzi, afya, adabu.
Shalom.
Ukizingatia kuviombea vipengele hivyo, kila kipengele si chini ya nusu saa. (dakika 30), utaona neema kubwa sana ya Mungu ikifanya kazi katika maisha yako.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>Â https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?
NDOA NA TALAKA:
About the author