Je Sulemani alifuga nyani? (2Nyakati 9:21)

Je Sulemani alifuga nyani? (2Nyakati 9:21)

Jibu:  Turejee maandiko hayo..

2Nyakati 9:21 “Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu zilizokwenda Tarshishi pamoja na watumishi wa Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na NYANI, na tausi.

22 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima”.

Sasa swali, je Sulemani alifuga NYANI?..

Jibu ni ndio alikuwa anao NYANI, lakini hakuwa anawatumia kwa kitoweo, kwani kulingana na sheria za torati, Nyani alikuwa miongoni mwa wanyama najisi (wasiofaa kuliwa M/Walawi 11:27).

Lakini kama hakuwa anawatumia kama kitoweo alikuwa na anawatumia kwa shughuli gani?.. Jibu ni wazi kuwa kwa MAONESHO au michezo! (Ingawa Biblia haijaweka wazi kuwa ni kwa michezo).. lakini asilimia kubwa ni wazi kuwa Nyani na Tausi walitumika kwa kazi hizo katika majumba ya wafalme.

Hata sasa si ajabu ukiingia Ikulu utakuta nyani na Tausi na wanyama wengine, sasa uwepo wa wanyama wale Ikulu, si kwaajili ya kitoweo kwa Raisi, bali kwa maonyesho tu. Na Sulemani ni hivyo hivyo alikuwa ni mtu anayepokea zawadi nyingi kutoka mataifa mengi, na zawadi hizo ni za kila aina, hivyo si ajabu kuona akipewa zawadi za wanyama, au akifanya  biashara za wanyama.

Je na sisi wakristo tunaruhusiwa kufuga wanyama pori hao katika nyumba zetu au wanyama hao wamebeba roho?..

Jibu ni Ndio tunaruhusiwa ikiwa sheria juu ya wanyama hao hazijavunjwa.. kama mtu ana kibali cha serikali kumiliki wanyama hao wa pori, basi kibiblia si kosa kuwamiliki pia, lakini iwe tu kwa dhamira kama hizo za maonyesho, lakini ikiwa kwa shughuli nyingine kama za kiibada au kijangili, ni kosa kibiblia.

Je umempokea YESU?.. Je unajua kuwa tunaishi majira ya kurudi kwa pili kwa YESU?, na parapanda imekaribia sana kulia?..Mwamini Yesu, na tubu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je wanyama wote waliwezaje kuenea kwenye safina ya Nuhu?

Mjombakaka ni nani kwenye maandiko? (Walawi 11:29)

LINDA CHEMCHEMI YA MOYO WAKO.

Swali: Je Kula nyama mbichi ni dhambi?.

Kwanini MUNGU aangamize watoto kwenye gharika ya Nuhu?

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments