SWALI: Mjombakaka ni nani kwenye maandiko?
JIBU: Neno hilo tunalipata kwenye vifungu hivi;
Walawi 11:29 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake,
Katika agano la kale, Mungu alitoa maagizo ya wanyama wanaopaswa kuliwa na wale wasiopaswa kuliwa. Na mmoja wa viumbe vilivyokatazwa kuliwa alikuwa ni mjombakaka.
Mjombakaka kama lilivyotumika hapa kwenye maandiko ni Kobe, na aina zake zote.
Walioorodheshwa katika vifungu hivyo ni wanyama wasio na mabawa, tofauti na wale wa kwenye Mambo ya walawi 11:20-23 wenye mabawa, ambao wote kwa pamoja wamewekwa katika kundi la viumbe najisi ambavyo haviruhusiwa kushikwa au kuliwa, kwasababu “vinatambaa” yaani matumbo yao yakiburuta chini.
Lakini Mungu aliruhusu visiliwe sio kwasababu za kiafya kama wengi wanavyodhani. Hapana, kwani hata sasa zipo jamii nyingi zinakula baadhi ya wanyama hao na wanaishi bila matatizo yoyote ya kiafya, bali walikatazwa kutokana na tabia walizobeba, ambazo zinafunua jambo la kiroho ambalo mtu akiwa nalo, basi anaweza kuonekana najisi mbele za Mungu.
Kwamfano, walikatazwa kula wanyama wasiocheua, kama nguruwe. Mnyama asiyecheuwa hana sifa ya kuhifadhi chakula na kukirejesha tena mdomo kukitafuna kisha kukimeza tena kama ng’ombe. Kufunua kuwa tukiwa watu tusioweza kukumbuka fadhili za Mungu alizotutendea nyuma, tukiwa watu wa kusikia tu Neno halafu baada ya hapo ndio imeisha hatulitendei kazi, sisi mbele za Mungu tunaonekana kama viumbe najisi.
Halikadhalika na hapa, wanyama hawa walionekana najisi, kwasababu wanatambaa, matumbo yao yanagusa chini. Nyoka alipolaaniwa aliambiwa kwa matumbo atakwenda. Ikiwa na maana haikuwa ni mapenzi ya Mungu viumbe vyake vitambae, tengeneza picha mwanadamu angekuwa anatembea huku tumbo lake likiburuta chini, angekuwa mdhaifu kiasi gani.?
Vivyo hivyo rohoni, hatupaswi kutambaa, bali kukimbia. Mashindano tuliyowekewa mbele yetu sio hata ya kutembea, bali kukimbia kabisa,
1Wakorintho 9:24 “ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate”.
Hivyo hupaswi kuwa mlegevu, ukijiona upo katika ukristo ule ule miaka nenda miaka rudi, huna jambo jipya uliloliongeza katika ufalme wa Mungu, au uliloliongeza ni dogo kulinganisha na muda uliodumu kwenye wokovu wako basi ujue kuwa unatambaa na hivyo Mungu anakuhesabu kama mmoja wa wanyama najisi.
Hivyo tujitahidi tusiwe wakristo wa namna hii, onyesha bidii kwa Mungu, itende kazi ya Mungu kwa karama uliyowekewa ndani yako. Kila siku jiulize ni jambo gani jipya nimeliongeza kwa Mungu wangu. Kwasababu ukumbuke kuwa kila mmoja atatolea hesabu talanta yake aliyopewa na Mungu siku ile. Je wewe umeongeza nini kwenye ufalme wa Mungu?
Bwana atupe nguvu ya kulitendea kazi Neno lake.
Shalom.
Angalia chini maana ya wanyama wengine kibiblia.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Lumbwi ni nini katika biblia?
JINSI UNAJISI UNAVYOMGHARIMU MTU.
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).
HAKUONA MAHALI PA KUTUA KWA WAYO WA MGUU WAKE.
Nyamafu ni nini?
Naivera ni nini? Kwanini Daudi aliihitaji alipomtafuta Mungu?
Rudi nyumbani
Print this post