Je! Yohana alimtilia shaka Bwana YESU? (Mathayo 11:3)

Je! Yohana alimtilia shaka Bwana YESU? (Mathayo 11:3)

Swali: Tunasoma katika Yohana 1:29 kuwa Yohana anamshuhudia Bwana YESU kuwa yeye “mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu”.. Lakini tukirudi katika Mathayo11:3 tunasoma tofauti, Yohana anawatuma wanafunzi wake wamwulize kama yeye ndiye Kristo au wamtazamie mwingine, sasa swali ni je Yohana alimtilia shaka Bwana Yesu au hakumwamini tangu mwazo?.


Jibu: Ni ngumu imani ya Yohana kutikisika kirahisi lakini hebu kwanza turejee kitabu cha Mathayo…

Mathayo 11:2 “Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,
3 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?
4 Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;
5 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.
6 Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami”.

Ni kweli Masihi ajaye alikuwa ametabiriwa kuwa atakuja na nguvu kuwaokoa Israeli na utumwa wa maadui zao, na Israeli wote walitazamia kabisa kuwa Kristo atakayekuja atawafungua na utumwa mgumu wa warumi.. lakini haikuwa hivyo kwa YESU KRISTO, kwani alianza kushughulika na dhambi za wana wa Israeli, zaidi ya Taifa.. Hiyo ikawafanya baadhi ya watu kumtilia mashaka YESU kama yeye ndiye KRISTO (Yaani Masihi).

Na bila shaka Yohana hakuwa na wasiwasi wa YESU kuwa Masihi, kwani tayari alishaonyeshwa wakati anambatiza YESU kuwa Yule atakayembatiza na ishara ya hua ikionekana juu yake basi huyo ndiye Masihi, na ni wazi kabisa Yohana alijua kuwa wakati wake aliokuwa anaishi duniani, Kristo naye alikuwa anaishi, ila hakumjua ni nani mpaka wakati wa ubatizo, Roho kama Hua aliposhuka juu ya Bwana, na mbingu kufunguka. (Mathayo 3:16-17).

Sasa kama ni hivyo ni kitu gani kilichomfanya Yohana Mbatizaji atume wanafunzi wake kwa YESU na kumwuliza swali ambalo tayari alikuwa na jibu lake?.

Jibu ni kwamba baadhi ya watu ikiwemo wanafunzi wake Yohana bado hawakuwa na uhakika wa moja kwa moja kama YESU ndiye KRISTO, kwahivyo kwa kusikia Neno linalotoka moja kwa moja kinywani mwa YESU, ingeweza kuwafanya waamini zaidi, hivyo Yohana lengo lake huu ni wanafunzi wakasikie na kujihakikishia wenyewe, kwamaana muda wake wa kuishi ulikuwa umekaribia kuisha na watakayebaki naye ni YESU. Na walipokwenda walipata majibu.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Yohana hakuwa na mashaka na Bwana YESU, bali wanafunzi wake na baadhi ya watu, na hiyo ni kutokana na kwamba Bwana YESU hakuwa anajitangaza hadharani kuwa yeye ni KRISTO.

Yohana 10:24 “Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi”.

Soma pia Luka 22:77..

Je umempokea YESU?.. Una uhakika kwamba YESU akirudi leo utakwenda naye?.. kama bado upo nje ya Imani fahamu kuwa upo hatarini sana, hivyo mkaribie YESU leo usamehewe dhambi zako na upokee ujazo wa Roho Mtakatifu.
Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)

NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?

“Hakuna aniulizaye unakwenda wapi”, maana yake nini? (Yohana 16:5).

Nini maana ya  “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:13)

Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply