Turejee..
Yohana 13:1 “Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo”.
“Upeo” ni kiwango cha mwisho cha Jambo… Kwamfano ukitazama juu, upeo wa macho yako unaishia kuona nyota zaidi ya hapo huoni kingine.. kwahiyo tunaweza kusema upeo wa kuona kwetu angani ni nyota..
Vile vile tunapofikiri kumhusu MUNGU, (kwa namna gani hana mwanzo wala mwisho) tunafikia kikomo cha kufikiri, tunafika mwisho wa Upeo wetu wa kufikiri (hatuwezi kufikiri zaidi ya hapo na kupata majibu).. na mambo mengine yote yana upeo wake..
Sasa hapa Bwana YESU aliposema kuwa “aliwapenda watu wake Upeo”.. maana yake alitupenda kiwango cha juu kabisa cha UPENDO, ambacho baada ya hicho hakuna kingine…
Upendo wa YESU kwetu ni MKUU mno, kina cha upendo wake, urefu wa upendo wake, mapana mapana ya upendo wake na kimo cha upendo wake hakielekezeki..
Waefeso 3:18 “ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu”.
Waefeso 3:18 “ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu”.
Mahali pengine anasema hivi..
Yohana 5:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake”.
Ni rahisi mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya mtoto wake, au mzazi wake au ndugu yake yoyote wa damu, lakini ni ngumu mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya Rafiki.. Kwasababu marafiki hawatabiriki, leo anaweza kuwa rafiki yako kesho msaliti wako, na adui..
Mtu anaweza kutoa msaada kwa rafiki yake lakini si UHAI, na mtu kama huyo akitokea basi upendo wake ni mkubwa sana!… na hapa Bwana YESU anajitaja yeye, kwamba anautoa uhai wake kwaajili ya rafiki zake, na tena si rafiki mmoja, bali wengi, ijapokuwa anajua kuwa katikati ya marafiki wapo wanafiki na wasaliti, lakini anautoa uhai wake kwaajili yao wote.. hakika huo ni UPEO wa mwisho kabisa wa Upendo.
Biblia inasema mtu ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe..lakini YESU ametufanya sisi kuwa rafiki zake na ametupenda kuliko ndugu.
Mithali 18:24 “Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; LAKINI YUKO RAFIKI AAMBATANAYE NA MTU KULIKO NDUGU”.
Neno la Mungu linazidi kutufundisha juu ya huu UPEO WA UPENDO WA YESU, kuwa hakuna chochote kilichopo duniani, wala kilichopo mbinguni, wala mahali pengine popote kitakachoweza kutuondolea Upendo wa YESU kwetu,.. YESU mwokozi ataendelea kutupenda na hakuna mtu atakayetuchonganisha naye..
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. 35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? 36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Sasa kama tunapendwa kwa upendo mkuu namna hii kwanini na sisi TUSIPENDEKEE??…Kwanini tusiitikie vyema huu upendo kwa kumpa yeye maisha yetu, na muda wetu na mioyo yetu?..
Utajibu nini siku ile, utajiteteaje siku ile, kama leo ukiudharau upendo huu mkuu?.. Ni heri ukampokea YESU leo kama bado hujafanya hivyo, kwa kutubu na kupokea Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;
JE! UMEFIKIA VIGEZO VYA KUWA BABA ROHONI?
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ