KATIKA UOVU MGEUZWE WATOTO WACHANGA

KATIKA UOVU MGEUZWE WATOTO WACHANGA

1Wakorintho 14:20 “Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika UOVU MGEUZWE WATOTO WACHANGA, bali katika akili zenu mkawe watu wazima”.

Biblia inatufundisha kuwa “Watu wazima” katika Akili, lakini tuwe watoto wachanga katika uovu, sasa ni nini maana ya kuwa watoto wachanga katika uovu?

Tukiwatazama watoto wachanga tunajifunza mengi, lakini jambo kuu tunaloweza kujifunza ni “Ukamilifu” watoto wadogo wanyonyao wanakuwa hawana hatia, sio waongo, si waasi, si walevi, si wazinzi, si wauaji, si wadhalimu, si wahuni, si waasi na mambo mengine maovu hayapo kwao, Na ndio maana Bwana YESU alisema kuwa ni lazima na sisi tugeuzwe kitabia na kuwa kama watoto wachanga..

Mathayo 18:3 “akasema, Amin, nawaambia, MSIPOONGOKA NA KUWA KAMA VITOTO, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni”.

Lakini haishii tu kusema tuwe “watoto katika uovu” bali pia tuwe “watu wazima katika akili”.. Mtu mzima katika akili ni Yule aliyeyabatilisha mambo mabaya, ya kale… mtoto anayechezea matope na kupenda kula peremende kila siku anapokuwa mtu mzima, ndipo anapoyabatilisha mambo ya kitoto na kuwa mtu mzima (hapo tunasema ameimarika kiakili).

Vile vile mtu ambaye alikuwa katika machafu ya dunia (ambayo ndio mfano wa uchafu wote wa utotoni), anapompokea YESU basi ya kale yanakuwa yamepita na sasa amekuwa kiumbe kipya.

2Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”.

Lakini mtu aliye nje ya imani, na kuendelea na machafu yote ya dunia, kibiblia anakuwa hana akili, na anafananishwa na mnyama.

Zaburi 49:20 “Mwanadamu mwenye heshima, IWAPO HANA AKILI, Amefanana na wanyama wapoteao”.

Ndio kwani biblia imesema mtu aziniye hana akili kabisa (soma Mithali 6:32, Mithali 7:7), na mtu anayemdharau mwenzake pia hana akili (Mithali 11:12).

Kwahiyo ni lazima tuache mambo ya kale, na kumgeukia Kristo, ili tupate akili, na mwenye uwezo wa kutubadilisha ni YESU tu peke yake, lakini wanadamu wengine wote hawawezi kutusaidia kitu, je umempokea huyu YESU?.. Je unauhakika Kristo akija leo unakwenda naye?.

Kama bado haujampokea YESU unangoja nini?.. maisha ya dhambi na anasa yamekusaidia nini?.. je ukifa leo utaenda wapi?

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

MPE MUNGU MAJUTO YAKO.

NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?

Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply