(Masomo maalumu ya utakaso)
Jina la Bwana na Mwokozi YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze Biblia, Neno la MUNGU wetu lililo Taa na Mwanga wa Njia yetu.
Je unazijua sehemu Nne (04) za Mwili wa Bwana YESU zilizotobolewa na kumwaga damu pale msalabani?.. Basi kama huzifahamu sehemu hizo ni 1)Kichwa, 2)Mikono, 3)Ubavu na 4)Miguu.
Tutazame moja baada ya nyingine, na pia tujifunze kwanini ni viungo hivyo ndio vilimwaga damu na kwanini vinahitaji utakaso sana.
1.KICHWA
Maandiko yanatuonyesha kuwa Bwana YESU alivikwa taji ya Miiba ..
Mathayo 27:28 “Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. 29 Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!”
Mathayo 27:28 “Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.
29 Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!”
Kwanini sehemu hii ya kichwa ilimwagika damu?.. Ni kwasababu kichwani ndiko kwenye ufahamu wa mtu, na milango yote ya ufahamu kama macho, masikio, pua na ulimi vipo huko.. na kwa kupitia vitu hivyo watu wanafanya dhambi, kwamfano kupitia ulimi mtu atasema uongo, atatukana, atakejeli n.k,
Kupitia macho mtu atatazama kwa kiburi sawasawa na (Mithali 6:17), kupitia macho mtu ataangalia uchafu, na pia kupitia masikio mtu atasikiliza mabaya, usengenyaji, njama mbaya n.k
Kwahiyo ni lazima Damu ingekota usoni kutakasa uso wa Bwana kwani dhambi zetu zote alizibeba yeye
2. UBAVU.
Biblia pia inatuonyesha kuwa Ubavuni mwa YESU palitokea damu..
Yohana 19:33 “Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; 34 Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji”.
Yohana 19:33 “Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu;
34 Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji”.
Sasa kwanini ubavuni?.. Ni kwasababu ubavuni ndipo Moyo wa mtu ulipo, na hata wale Askari wa kirumi walikusudia kuhakiki kifo cha Bwana YESU kwa kumpiga mkuki katika moyo..
Na moyo ndio ubebao mawazo yote ya mtu ikiwemo mawazo mabaya..
Mathayo 15:19 “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano”
Kwahiyo kulikuwa na sababu kwanini damu itokea moyoni ni kuonyesha utakaso wa Moyo..
3. MIKONO
Pia Biblia inatuonyesha kuwa mikono ya Bwana YESU ilitoka damu..
Yohana 20:25 “Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo”.
Kwanini mikono?.. Kwasababu mikono ndio inayoshika, inayofanya kazi za kila namna, (zilizo njema na mbovu)…watu wanafanya mauaji kwa kutumia mikono yao, kwa ufupi mikono ni nyenzo kubwa ya mabaya ndani ya mtu ndio maana katika ile ile Mithali maandiko yanasema, moyo uwazayo mabaya ni machukizo kwa Bwana..
Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. 17 macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu”
Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu”
4. MIGUU
Biblia inatuonyesha sehemu nyingine ya mwisho ya mwili wa Bwana YESU iliyomwagika damu ni miguu..
Luka 24:38 “Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo”.
Luka 24:38 “Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?
39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo”.
Miguu ni kiungo kingine chenye kuutia mwili mzima unajisi..watu wanatumia miguu kukimbilia mabaya, kukimbilia uzinzi, mauaji, ulevi n.k
Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. 17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu”
17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu”
Sasa viungo hivi ni lazima vitakaswe kwa damu ya YESU, na vinatakaswaje?
Vinatakaswa kwanza kwa kumwamini Bwana YESU KRISTO, na kuomba na kuacha dhambi.. zingatia hili neno “kuacha dhambi” kupitia viungo hivyo.
Angalia miguu yako inachokimbilia, je ni chema au ni kibaya.. jiuepushe miguu yako na njia za wakosaji, angali macho yako yanachokitazama ni chema au kibaya, jiepushe na kutazama mambo yasiyofaa, vivyo hivyo na mikono yako na moyo wako, angalia sana unavyovifuatilia na kuvifanya.
Mwisho, kumbuka tunaishi katika siku za mwisho, na Kristo amekaribia sana kurudi, wakati wowote parapanda ya mwisho italia na hukumu ya mataifa itaanza, je umejiandaaje?
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
USHUHUDA WA MATENDO NI MKUU KULIKO WA MANENO.
UZURI WA MAJIVU.
IPO NJIA YA MKATO YA KUFIKA KIWANGO VYA MBALI VYA KIROHO.
Na kipenu ni nini (Isaya 1:8)
Wokovu wa milele/ Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?
Print this post
Swali: Kughofiri ni kufanya nini kama tunavyosoma katika Zaburi 79:9?.
Jibu: Turejee..
Zaburi 79:9 “Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie, Kwa ajili ya utukufu wa jina lako. Utuokoe, UTUGHOFIRI dhambi zetu, Kwa ajili ya jina lako”.
Maana ya “Kughofiri” ni “kuondoa”.
Neno hilo limeonekana mara moj tu kwenye Biblia…na maana yake ni ile ile na ya kusamehe..
Lakini Biblia inazidi kutufundisha kuwa Bwana anatuokoa na kutusamehe pia makosa yetu kwaajili ya jina lake.
Maana yake pia kwa utukufu wa jina lake, anapotusamehe makosa basi pia jina lake linatukuzwa zaidi, hivyo ni fahari ya Mungu pia kutusamehe sisi.
Isaya 43:25 “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako”
Sasa swali kama Mungu anafurahia kutusamehe makosa yetu kwanini tusitumie hiyo fursa kuungama?.
Je umempokea YESU?.. Umetubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha?kama bado je unasubiri nini?…
Tubu leo upate msamaha wa dhambi, na upate ondoleo la dhambi pia.
Luka 24:46 “Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.
Luka 24:46 “Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.
NGUVU YA MSAMAHA
UMUHIMU WA KUOMBA MSAMAHA.
KAMA NISIPOKUTAWADHA, HUNA SHIRIKA NAMI
NINI MAANA YA UKOMBOZI?
ZIFAHAMU ALAMA KUU NNE ZA KRISTO NDANI YAKO.