2 Yohana 1:10-11
[10]Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. [11]Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.
[10]Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
[11]Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.
Ni salamu ya namna gani ambayo ililengwa hapo?
JIBU: Ukisoma habari yote tokea juu utaona mtume Yohana anazungumzia kundi la wadanganyifu ambao walitokea wengi duniani wakati ule, ni kundi la watu waliopinga kuja kwa Yesu katika mwili kwa namna ya kibinadamu, akasema hao ndio wapinga Kristo.
Na mbeleni akatoa katazo la kutowakaribisha hata majumbani kwao, wala kuwapa salamu, maana kuwapa salamu ni kushiriki kazi zao mbovu.
Swali je ni salamu ya namna gani ililengwa hapo.?
Salamu zinazozungumziwa hapo si salamu hizi za kijamii za “umeamkaje, au shikamoo, au za mchana” hapana bali ni salamu za kiroho ambazo hata wakati ule wayahudi walipozisema zilimaanisha ushirika mmoja katika kiimani. Kwamfano, walipokutana walibusiana na kusema “Amani ya Bwana iwe pamoja nawe”..
Sasa salamu kama hiyo utajiuliza ni bwana yupi ikiwa huyo mwingine haamini katika fundisho kama lenu.. ukimsalimia basi unakubaliana na bwana wake ambaye hajaja katika mwili. Tayari umeshazishiriki kazi zake.
Ni sawa na leo labda tuseme unakutana na watu wanaomwamini kweli Yesu, lakini Yesu ambaye hajafufuka, yupo kaburini mpaka sasa, halafu anakuja anakusalimia “Bwana Yesu asifiwe” na wewe unasema Amina..Mtu mgeni akipita akakusikia atajua kuwa mna imani moja kuhusu Yesu Kristo ambaye hajafufuka.
Hivyo hata kwa wakati huu, salamu zetu za kiroho zisimame mahali ambapo tunajua imani tulio nayo kuhusu Kristo ni moja.
Kwasababu salamu tu, hutangaza, zina nguvu kama lilivyo fundisho.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.
JAWA SANA MOTO ULAO.
Print this post
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu katika kujifunza Biblia.
Upo usemi usemao “wanadamu tumeumbiwa maradhi”..Usemi huu ni wa hekima za ulimwengu, ambao Biblia inasema ni upuuzi mbele za Mungu (1Wakorintho 3:19).
Ni kweli maradhi yapo lakini hatupaswi kuyakiri na kuyakumbutia kama sehemu yetu, (ikiwa tumeshampokea YESU) ….hata kama yapo ndani yako si sahihi kusema “hayo ni ya kwako” au “umeumbiwa”, ni kauli ambayo ni hatari sana.
Kwanini Maradhi si sehemu yetu tuliomwamini YESU? Na kwanini hatupaswi kutawaliwa nayo?.
Hebu tujifunze kidogo historia ya Maradhi mabaya na hatari kibiblia.
Kipindi wana wa Israeli wanatoka MISRI, kuelekea nchi ya Ahadi, Kanaani, Mungu aliwaambia yale maradhi yaliyokuwa yanawapata MISRI hayatawafuata Kaanani..
Kumbukumbu 7:15 “Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako MARADHI YO YOTE MABAYA UYAJUAYO YA MISRI, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao”.
Maana yake ni kwamba wakiwa Misri pamoja na kwamba walikuwa katika utumwa wa mwilini lakini pia Misri ILITAWALIWA NA MAGONJWA YA KUTISHA (Soma Kutoka 15:26 na Kumbukumbu 28:60).
Misri haikuwa sehemu salama kiroho na hata kimwili, kulikuwa kuna mlipuko wa magonjwa ya ajabu na ya kutisha, ambayo hayo yalitokana na miungu wa Misri waliyokuwa wakiiabudu..Na Bwana aliwaonya wana wa Israeli kwamba wakirudi kuitumikia hiyo miungu basi yale maradhi ya MISRI yatavuka kuwafuata waendako.
Kumbukumbu 28:60 “Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. 61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.
Kumbukumbu 28:60 “Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.
Kwahiyo tunachoweza kuona ni kuwa “Magonjwa yote asili yake ni Misri”, na Mungu aliyaweka kwa waMisri kutokana na maisha yao ya kuabudu miungu (shetani)..
Sasa swali kwanini yatutawale sisi ambao hatuabudu miungu ya Misri, na wala hatupo Misri, vile vile kama yanavyowatawala waMisri (watu ambao hawamjui Mungu)?
Ni swali la kutafakari sana..
Ukiona kuna ugonjwa unakusumbua miaka mingi, na umejaribu kutumia matibabu ya hospitalini yaliyo halali lakini tatizo linabaki kuwa sugu, au linakwenda baada ya muda linarudi..hebu wakati wa leo simama na kusema “imetosha”.
Huenda hujajua tu haki yako ndio maana ibilisi anakutesa na kukusumbua…anakujengea saikolojia kwamba huo ugonjwa ni wa kwako na huwezi kupona.. Leo hii simama na kusema “Magonjwa ya Misri si sehemu yangu”.
Kama umeokoka kweli kweli, usikae ukiri kwa kinywa chako, au uamini moyoni mwako kuwa “magonjwa ni sehemu yako”.. anza kuanzia leo kufuta kalenda za kwenda hospitali hospitali kila mara.
Tatizo linalowakabili watu wengi waliookoka ni kuamini na kujiwekea matumaini katika madawa na mahospitali, sio vibaya kuamini hivyo, lakini kunadumaza imani yako kwa MUNGU na kuyapa nafasi magonjwa ya Misri juu yako.
Si kila dalili tu ya mafua unayoyasikia unakimbilia dawa!..si kila homa tu inayokupata unakimbilia hospitalini utaacha lini hiyo tabia?.. Hufanyi dhambi lakini unadumaza imani yako.
Jenga tabia ya kuamini kuwa ninaweza kuwa na afya na uzima bila ya madawa wala hospitali, kwasababu wewe sio Mmisri, kwahiyo Maradhi ya Misri hayakuhusu, wala taarifa za maradhi ya Misri si sehemu yako.
Afya yako ni ya muhimu sana, ukiwa na maradhi hata uwezo wako wa kiutendaji kiroho unakuwa hafifu, hivyo usikubali hata kidogo, maandiko yanatufundisha hivyo kwamba ni mapenzi ya Mungu tuwe na afya zetu..
3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
Ikiwa una maradhi yanayokuonea leo kwa imani fuatisha maneno yafuatayo na yatakuacha haraka sana..
Sema “Bwana YESU ninasogea mbele zako, ninaomba unisamehe nilipofungua mlango wa maradhi katika maisha yangu, lakini pia naomba unisamehe nilipopungukiwa imani, siku leo ninakiri uzima na afya, ninayakataa maradhi yote ya Misri juu ya mwili wangu, kwakuwa mimi sio Mmisri, kuanzia leo mimi ni mzima na wala sitasumbuka tena, ninaomba na kuamini katika jina kuu lako Bwana YESU KRISTO. Amen”
Nini maana ya kuinuliwa juu ya nchi? (Yohana 12:32).
JINSI MATENDO YA IMANI YANAVYOWEZA KULETA UTAMBULISHO MPYA KWA MTU.
UTAIKUZAJE IMANI NDANI YAKO?
Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?
Je! Imani ya mitume ipo katika maandiko?
WhatsApp
Jina la Bwana YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze maandiko..
shetani hana jipya zaidi ya kunakili (kucopy) vile vilivyopo na kuvutumia kinyume.
Kwamfano kafara za wanyama kama mbuzi na kondoo kwaajili ya utakaso hazikuanzia kwa shetani, bali zilianza kwa MUNGU, ambapo katika Agano la kwanza (yaani Agano la kale) damu za wanyama hao zilitumika kwaajili ya utakaso, lakini sasa Agano jipya hazitumiki tena kwani Damu ya YESU ni bora zaidi ya damu za wanyama.
Kwahiyo shetani anachokifanya ni kunakili kilichokuwa kinatumika zamani (kisicho na matumizi tena) na kukileta siku za mwisho kwaajili ya matumizi yake, ndio maana utaona waganga wa kienyeji na wachawi ndio sadaka zao hizo.
Sasa sio tu hilo, lakini pia katika utumishi, shetani anayo desturi ya kutengeneza nakala..
Kwa namna gani?
Hebu turejee ile habari ya yule mchawi aliyeitwa.. “Bar-YESU” katika Matendo 13?..tuzisome habari zake kidogo kisha tuendelee mbele..
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BAR-YESU; 7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali SERGIO PAULO, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu”
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BAR-YESU;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali SERGIO PAULO, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu”
Huyu “Bar-Yesu” ni nabii wa uongo na ni mchawi, lakini ajabu ni kwamba jina lake limebeba jina la YESU ndani yake.. Je unaelewa maana ya Bar-Yesu?.. maana yake ni “Mwana wa YESU” hiyo ndio tafsiri yake..
Kwahiyo huyu mchawi na nabii wa uongo, alikuwa ni mtu anayemjua YESU na anayedai kufundisha habari za YESU, lakini nyuma yake alikuwa ni mwongo.
Na jambo jingine la ajabu ni kwamba huyu Bar-Yesu alikuwa ni mwalimu wa kiroho wa mtu mmoja aliyeitwa “Sergio-Paulo”… Je unaelewa maana ya Sergio-Paulo?…maana yake ni “Mhudumu-Paulo”..
Kwahiyo wakati YESU wa Mnazareti, anammiliki Paulo mtumishi wa Mungu, yupo mtu anaitwa Bar-YESU anayemmiliki Sergio Paulo.
Kwahiyo hapa kuna “Sergio-Paulo” na “Bar-Yesu” na kuna “Paulo” na “YESU”. Kuonyesha kuwa shetani hana jipya zaidi ya kunakili vile vilivyopo vilivyo halali na kuvigeuza kwa matumizi yake.
Maandiko yanasema hivyo…
2Wakorintho 11:14 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake NAO WAKIJIGEUZA WAWE MFANO WA WATUMISHI WA HAKI, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao”.
2Wakorintho 11:14 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake NAO WAKIJIGEUZA WAWE MFANO WA WATUMISHI WA HAKI, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao”.
Kwahiyo si kila anaitwa mtumishi wa YESU ni mtumishi kweli wa YESU, vile vile si kila anayejiita ni Mkristo, ni Mkristo kweli kweli, ni muhimu kuwa macho sana, na kujua vipimo halisi vya kuwatambua manabii wa uongo, waalimu wa uongo, wachungaji wa uongo, waimbaji wa uongo pamoja na wakristo wa uongo.
Na kipimo hiko si kingine zaidi ya NENO LA MUNGU, baada ya kujaa Roho Mtakatifu, Neno la MUNGU pekee ndio kipimo cha kumjua huyu ni wa MUNGU au wa ibilsi, hii ni sauti ya Mungu au ya ibilisi.
Je umeokoka?.. unao uhakika wa kwenda mbinguni ikitokea parapanda imelia leo?
Kama bado haujampa YESU maisha yako, bado parapanda haijalia leo, lakini muda wowote mambo yanabadilika, hivyo fanya mabadiliko kabla ya mabadiliko makuu kutokea.
JIHADHARI NA ROHO YA YEZEBELI.
Roho ya Malipizi/ roho za malipizi ni nini?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
UNAMALIZAJE MWAKA WAKO, JE NA MUNGU AU SHETANI?
Mfundishe mtoto namna ya kutumia jina la Yesu katika kutenda mambo yake yote.
Tambua Dhambi inaua chini kwa chini..
Je unajua ni kwa namna gani?….
Hebu fikiri kama mwili wako usingewekewa hisia ya maumivu kabisa, maana yake ukijikata na kisu hauhisi maumivu, ukipigwa husikii maumivu, ukinywa kitu chenye kudhuru husikii maumivu yoyote ya tumbo, ukiwa na vidonda vya tumbo husikii maumivu yoyote..
Unadhani ni nini kingetokea baada ya muda fulani?..bila shaka ni “kifo cha ghafla”.. kwanini? Kwasababu ungepata majeraha ambayo yangeendelea kukuharibu ndani kwa ndani, na usingekujua kama kuna tatizo kwasababu hakuna hisia yoyote ya maumivu utakayokupa taarifa ya tatizo mahali fulani, hali kadhalika usingekuwa mtu wa kujijali, kwani maumivu yanasaidia kujijali na kujihadhari.
Sasa dhambi iko hivo hivyo…haina hisia yoyote ya maumivu katika mwili, kiasi kwamba mtu anapoifanya anaweza kudhani hajaingiza madhara yoyote katika maisha yake, lakini mwisho wake ni kifo cha ghafla.
Hiyo ndio saababu ya Bwana MUNGU kumwambia Adamu pale bustanini kuwa asile yale matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwani atakufa, agizo hilo halikuwa kwa faida ya MUNGU bali kwa faida ya ADAMU na kizazi chake, ili waishi na wasife.
Mwanzo 2:17 “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”.
Na vinyo hivyo maandiko yanasema kuwa mshahara wa dhambi ni “MAUTI”
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Ndugu, dhambi haina maumivu mwilini, hautasikia maumivu yoyote mwilini ukishamaliza kuzini, au ukishafanya anasa, ukitukana, ukiishi maisha ya dhambi, n.k lakini madhara yake yanakuja ghafla utaona amani uliyokuwa ndani yako inakufa ghafla, furaha yako inakufa ghafla, Baraka zako zinazima ghafla, na mwisho kifo cha mwili kinahitimisha ikiwa mabadiliko hayatafanyika mapema.
Lakini habari njema na nzuri ni kwamba kwa YESU hata kama mambo baadhi yameshakufa kutokana na dhambi, ipo ahadi ya ufufuo wa mambo hayo endapo mtu atamkimbilia YESU kwa njia ya kutubu na kujinyenyekeza mbele zake, ile amani iliyokufa inarudi mara dufu, ile furaha iliyokufa inafufuka, ule ushindi ulioupoteza unarudi, ile afya iliyopotea inarudi na mambo mengine mazuri..
Je ni wewe leo ambaye dhambi imekuulia mambo yako mazuri, na ni ghafla?.. na hujui nini cha kufanya?.. hakuna atakayekutoa hapo, hata upate pesa kiasi gani bado shida itakuwepo, hata dunia nzima ije upande wako na kukufariji bado utaona kuna kupungukiwa mahali fulani..
Suluhisho lipo kwa mmoja tu, nakuambia ukweli.
Na huyo si mwingine zaidi ya YESU MNAZARETI, huyo atakugeuzia ukurasa wa maisha na kukupa uzima wa hapa duniani na ule wa milele ujao (uzima tele).
Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. 11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.
Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.
Unachopaswa kufanya ni kukiri kuwa wewe ni mkosaji, na dhamiria kuacha dhambi, yeye atashughulika kukuongezea nguvu ya kushinda dhambi, na pia tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi kwa jina la Bwana YESU KRISTO, (Matendo 2:38), hapo utakuwa umekamilisha hatua zako za wokovu, kwani yule Roho Mtakatifu ataingia ndani yako, na kukufanyia miujiza ambayo hata ukihadhithia huwezi kueleweka.
UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.
JINSI YA KUACHA DHAMBI INAYOKUTESA.
SHUGHULIKA NA HASIRA INAYOKAA KIFUANI
SAFARI YA KUUONA USO WA MUNGU.
MKATAE MWAJIRI HUYU MBAYA.
Uvuguvugu ni ile ya hali ya kuchanganya mambo mema na mazuri (mema na mabaya kwa wakati mmoja).. Na roho ya uvuguvugu ilianzia EDENI, ndiyo shetani anayoitumia kuangusha watu.
Turejee mojawapo ya miti iliyokuwepo Edeni, Biblia inatuambia kulikuwepo na “Mti wa Ujuzi wa MEMA na MABAYA” ambao Bwana MUNGU alitoa maagizo wasiuguse wala kula matunda yake.
Huu ulikuwa ni mti wenye sifa ya UVUGUVUGU, yaani wenye “Mema na Mabaya wakati huo huo”.. Na ibilisi alijua mwanadamu anapenda Uhuru wa kufanya mambo yote kwa pamoja, (mema kidogo na mabaya kidogo).. na alianza kupitisha ushawishi huo kwa Hawa, na pasipo kuzitambua hila za ibilisi, tukaingia katika kosa la moja kwa moja.
Ndugu ibilisi hamtegi mtu wa Mungu (aliyesimama) kwa mabaya.. bali atamtega kwa “Mabaya yaliyochangamana na mema”.. Ni ngumu kwa ibilisi kumwachisha mtu wa MUNGU mema!.. hawezi kumfundisha moja kwa moja aache mema, ni jambo gumu sana kwake, ingekuwa ngumu kwa shetani kumshawishi HAWA pale bustanini amwambudu yeye na aache kumwambudu MUNGU, Hawa asingeweza kumsikiliza nyoka)..ni jambo gumu sana.
Lakini adui alikuja na injili ya uvuguvugu, kwamba aendelee na mema, lakini na mabaya pia ayafanye kidogo na MUNGU atamkubali!.. kwaufupi afanye mema kidogo na mabaya kidogo, asiwe moto, awe vuguvugu kwani bado MUNGU atamkubali..pasipo kujua ni mtego mbaya, sana wa kutapikwa moja kwa moja na MUNGU.
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, KWA SABABU UNA UVUGUVUGU, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, KWA SABABU UNA UVUGUVUGU, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.
Ni jambo hilo hilo, analiendeleza leo katika kuwaangusha watu wa MUNGU waliosimama, anawashawishi kuamini kuwa Ukiwa mtu wa kiMungu sana utachanganyikiwa, ni lazima uchanganye na mambo mengine madogo madogo ya kiulimwengu..
Ijapokuwa umeshakuwa mkristo, unaenda kanisani, unatoa sadaka, basi siku moja moja onja mvinyo, ijapokuwa hutukani, huna ugomvi na mtu na unasaidia masikini sio mbaya pia siku mojamoja kwenda kwenye dansi za starehe, ijapokuwa huibi, hudhulumu sio mbaya ukifanya uasherati mara moja moja..Hii ni sumu hatari sana, iliyowaangusha wazazi wetu wa kwanza.
Jihadhari na roho ya uvuguvugu, kwani unamtoa mtu moja kwa moja kutoka katika Neema ya MUNGU.
Je umempokea YESU?. Unao uhakika wa uzima wa milele baada ya maisha haya?..Fahamu kuwa uzima wa milele upo kwa YESU tu, na si mwingine.
Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”.
Bwana atusaidie.
KUJITAKASA NI MUHURI WA UTAKATIFU
MAANA HUYAWAZI YALIYO YA MUNGU, BALI YA WANADAMU
Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)
Je Sulemani alifuga nyani? (2Nyakati 9:21)
MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.
Mathayo 3:16 “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; 17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, NINAYEPENDEZWA NAYE”.
Mathayo 3:16 “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, NINAYEPENDEZWA NAYE”.
Nataka tuone hiyo sehemu ya mwisho ya andiko inayosema.. “NINAYEPENDEZWA NAYE”.. hasemi ninayefurahiwa naye, au ninayeshangiliwa naye, au ninayetukuzwa naye, au au ninayeshabikiwa naye, au ninayeburudishwa naye, bali ametumia neno “NINAYEPENDEZWA NAYE”.. Hili ni neno kubwa sana.
Ni lazima tutafute “kumpendeza Mungu” siku zote hilo ndio jambo kuu na Mungu analolihitaji kutoka kwetu…
Waefeso 5:9 “kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; 10 MKIHAKIKI NI NINI IMPENDEZAYO BWANA”.
Waefeso 5:9 “kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
10 MKIHAKIKI NI NINI IMPENDEZAYO BWANA”.
Kumpendeza MUNGU maana yake ni kufanya mambo yanayoufanya moyo wa MUNGU kukufurahia na hayo si mengine zaidi ya matendo ya UTAKATIFU.
1Wathesalonike 4:2” Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3 Maana haya NDIYO MAPENZI YA MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
1Wathesalonike 4:2” Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
3 Maana haya NDIYO MAPENZI YA MUNGU, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA;
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
Na utakatifu ni ule nje na ndani, sio tu wa ndani bali pia wa nje, maana yake jinsi unavyouweka mwili wako pia.
Warumi 12:1” Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.
Warumi 12:1” Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.
Epuka kuwa mshabiki wa MUNGU bali tafuta “kumpendeza Mungu”.. Mtu ambaye ni mshabiki wa Mungu ni yule anayejua sana mambo ya Mungu na sheria zake, lakini hazifanyi na pia hazipingi huyu ni mfano wa mtu ambaye ni mshabiki.
Ni yule mtu ambaye anakubali Mungu ni mwenye nguvu, ni wa upendo, ni mwenye haki na hata kumsifia mbele za watu, lakini kimaisha na mwenendo hamfuati MUNGU, bali anafuata njia yake, na ibilisi ndiye anayemtumikia. (huyu ni mshabiki)
Epuka kuwa mshabiki, bali kuwa mwana wa MUNGU ambaye UNAMPENDEZA MUNGU aliyekuumba. Kuwa mtakatifu mwilini na rohoni.
FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.
MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?
YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.
Swali: Bwana YESU alikuwa na maana gani aliposema “Nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”?
Jibu: Turejee..
Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”.
Kuinuliwa juu kwa Bwana YESU, kupo kwa namna mbili (02), namna ya kwanza ni “KUINULIWA MSALABANI” na namna ya pili ni “KUINULIWA NA WINGU kwenda mbinguni”.
Tuangalie maana moja baada ya nyingine..
1. KUINULIWA MSALABANI.
Hii ndio maana ya kwanza kabisa ya “Kuinuliwa kwa Bwana YESU”.. Na kunafananishwa na wakati ule Musa alipomwinua nyoka wa shaba jangwani, ili kila mtu amtazamapo apone..
Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.
Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.
Kwa nguvu ile ile iliyowavuta watu wenye majanga ya kuumwa na nyoka jangwani, ndio nguvu hiyo hiyo iliyoachiwa pale msalabani, kwamba kila mtu mwenye mzigo wa dhambi na vifungo, autazamapo msalaba wa Bwana YESU kwa ufunuo, basi atapata msaada wa kufunguliwa kutoka katika dhambi, magonjwa na kila aina ya mateso ya ibilisi.
2. KUINULIWA NA WINGU.
Hii ni maana ya pili ya kuinuliwa juu kwa Bwana YESU, kulikotoa nguvu ya kuwavuta watu kwa Mungu..
Turejee Matendo 1:8..
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, AKAINULIWA, wingu likampokea kutoka machoni pao”.
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, AKAINULIWA, wingu likampokea kutoka machoni pao”.
Kwa namna gani au kwa njia gani, baada ya kuinuliwa Bwana YESU juu katika wingu watu walivutwa kwake na hata sasa tunavutwa kwake, si kwa njia nyingine zaidi ya Roho Mtakatifu.
Kwasababu alisema baada ya kupaa kwake atashuka Roho Mtakatifu, ambaye huyo ataushuhudia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8).
Kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, siku ile tu ya Pentekoste aliposhuka watu elfu tatu walimwamini Bwana YESU na nguvu zake, uamsho mkuu ambao mitume hawajawahi kuuona, hiyo ni kuonesha kuwa ahadi ya Mungu (yaani Roho Mtakatifu), ina nguvu zaidi ya vitu vyote.
Zekaria 4:6 “Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, BALI NI KWA ROHO YANGU, asema Bwana wa majeshi”.
Je Neno la msalaba umelitii??.. Umesamehewa dhambi?.. umeoshwa dhambi zako kwa damu yake?.. je umekimbilia msalabani upate wokovu?
1Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa”.
1Wakorintho 1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa”.
Mwamini YESU leo kama bado haujafanya hivo, na tubu kwa kumaanisha dhambi na ubatizwe.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii..
MANENO SABA YA YESU MSALABANI.
YESU MNAZARETI, ANWANI YA MSALABA.
MSALABA NI ZANA YA UJENZI WA MAISHA YAKO.
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
TAFUTA UTAKASO WA SEHEMU KUU NNE ZA MWILI WAKO.
Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze pamoja Biblia.
Bwana alipokutana na Petro aliambiwa “TANGU SASA UTAKUWA UKIVUA WATU”. Hii ni kauli pana, ambayo ni muhimu tuijadili kwa kina kidogo..
Luka 5:10 “na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia SIMONI, USIOGOPE, TANGU SASA UTAKUWA UKIVUA WATU”.
Luka 5:10 “na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu
akamwambia SIMONI, USIOGOPE, TANGU SASA UTAKUWA UKIVUA WATU”.
Hapa Bwana YESU alifananisha “Uvuvi wa Samaki” na “Uvunaji wa watu” . Kwa ufupi Bwana YESU alifananisha watu na “Samaki”… Kama vile samaki wanavyovuliwa kutoka majini hali kadhalika watu wanavuliwa kutoka upotevuni.
Sasa kama maji yanavyohusika katika “Uvuvi wa samaki” vile vile maji pia yatahusika “uvuvi wa watu” kama ishara.. na hapa ndio tunakuja kuona umuhimu wa UBATIZO.
Wengi hatuoni umuhimu wa Ubatizo katika kukamilisha wokovu, lakini Ubatizo wa maji mengi unasimama kama muhuri wa kukamilisha wokovu wa mtu (Soma Marko 16:16).
Unapobatizwa kwa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU ni ishara ya kwamba umevuliwa kutoka katika ulimwengu..
Sasa jiulize, Umeona wapi samaki anavuliwa kutoka katika nchi kavu?.. Vile vile wewe na mimi kama samaki tuliovuliwa ni lazima tuwe na ishara ya kutoka majini, ndio hapa linakuja agizo la ubatizo.
Na samaki akishatoka majini anapoteza uhai wa maisha yake ya kwanza, na vile vile baada ya ubatizo mtu anapoteza uhai wa maisha yake ya kwanza ya dhambi (maana yake yale maisha ya dhambi anayafia, anakuwa kiumbe kipya).
Je umeshabatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO (sawasawa na Matendo 2:38, Matendo 10:48 na Matendo 19:5).. Kama bado unasubiri nini?.. je bado unaendelea kushikilia mapokeo ya dini na dhehebu hata baada ya kuujua ukweli wa Biblia?
Siku ile hatutahukumiwa kulingana na Mapokeo tuliyopokea bali kulingana na maneno yaliyoandikwa katika vitabu vyote sitini na sita vya kwenye Biblia..
Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”.
Maneno ya Mungu ndani ya Biblia ndio yatakayotuhukumu siku ya mwisho, maana yake siku ile tutaulizwa kwa yale yaliyoandikwa kwenye biblia sio kwa yale tuliyoyapokea kwenye dini zetu..
Kwa namna gani?.. Hebu tuingie ndani kidogo kulifafanua hili..
Mtu mmoja alimfuata Bwana YESU na kumwuliza tiketi ya kuurithi uzima wa milele, hebu tusome jibu la Bwana YESU Mkuu.
Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? 26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?”
Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?”
Tazama jibu la Bwana hapa?.. hakumwambia “umerithishwa nini na wazazi, au umefundishwa nini kwenye dini yako”.. Lakini alimwambia “Imeandikwa nini” lakini sio tu imeandikwa nini, bali pia “Unasomaje”
Ikimaanisha kuwa wakati wa Mwisho, watu watahukumiwa kwa yaliyoandikwa katika Biblia..Na moja wapo ya jambo lililoandikwa katika maandiko ni ubatizo. Sasa kupuuzia agizo la msingi namna hii ni hatari sana, hatutakuwa na la kujibu siku ile, ikiwa tulijua kweli na hatukuifanyia kazi.
shetani amepofusha fikra za watu wengi katika siku hizi za mwisho, na kuwafanya wasijue wala kuona umuhimu wa ubatizo pamoja na baadhi ya mambo mengine ya msingi katika Biblia.
2Wakorintho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
Bwana atusaidie sisi tusiwe miongoni mwao wanapofushwa fikra na ibilisi.
AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?.
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
WOKOVU UKIHARAKISHA USIUZUIE.
Kuishi ni tufoauti na kuwa na uhai. Hata mti ni hai, lakini hauishi. Kuishi ni maisha, yaani unasifa ya kuwa na mfumo au ustaarabu Fulani ambao unatembea nao, unaweza kuchagua mahali pa kukaa, unafanya kazi, unapumzika, unajenga, unapanda, unajichagulia burudani mfano miziki, michezo, vyakula, unafanya ibada, unauza, unanunua.. mambo kama hayo kiumbe kikitenda tunasema kinaishi.
Lakini kuwa kifungoni, ndani ya gereza huoni jua wala mwezi siku zako zote uwapo duniani, hatuwezi kusema unaishi, tunasema wewe upo hai, lakini hauishi.. Au unapokaa kwenye kitanda cha wagonjwa mauti-uti, umepooza, huwezi kuongea wala kutembea, umekata kauli, kwa sikuzote uwapo duniani, hayo si maisha ijapokuwa upo hai.
Sasa kuna maneno Yesu aliyasema, ambayo si wengi hujaelewa kwa undani na upana.. Tusome;
Yohana 11:25-26
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Hii kauli ukiisoma vizuri, unaweza ukasema inajichanganya, Embu tafakari, jambo la kwanza Yesu anasema, tukimwamini tukifa tutakuwa tunaishi, lakini pia tukiwa hai na kuamini hatutakufa kabisa hata milele.
Je! Sisi tuliomwamini hatufi?
Jibu ni Ndio hatufi kabisa, bali tunahamishwa makao. Hicho kinachoitwa kifo, ni macho ya wanadamu yanaona hivyo, lakini sisi tunakuwa kama tumefumba macho, kisha tukafumbua na kujikuta katika ulimwengu mwingine kabisa, Ndio maana lugha ambayo hutumika kueleza hali hiyo kwa watakatifu ni kulala (Matendo 7:54-60, 1Kor 15:51-58, Yohana 11:11-19)
Sisi tuliomwamini Yesu hatutaona kitu kinachoitwa kaburi, wala hatutajikuta kwenye gereza Fulani , bali kwenye ulimwengu mwingine mzuri sana uitwao pepo, sio tukiwa hai, bali tukiwa tunaishi kabisa huru.
Maana yake, tunaendeleza maisha, ikiwa kuna kutembea, huku na huko au kushughulika kwa vitu vya kimbingu, kufanya hivi, kufanya vile..Tutakuwa tunayafanya. Hayo ndio maisha anayosema mtu akimwamini yeye, ajapokufa (lala), atakuwa anaishi.. Si atakuwa na uhai
Tutakaa huko pepo, kwa kipindi chote, ambacho tunamsubiria Yesu, kulikamilisha kusudi la watakatifu wote, kisha baadaye,(mwisho ukifika), atakuja mwenyewe kuwachukua walio hai Pamoja na miili yetu tuliyoiacha duniani, na sote kwa Pamoja tutaanza ziara mpya ya kuelekea mbingu ya tatu. Makao yetu ya milele yalipo (2Wakorintho 12:2-4)
Lakini waovu wanapokufa, wenyewe watajiona kwanza wakiingia makaburini, kisha wakishuka kuzimu, Uhai wao ukitunzwa kwenye vifungo vya giza wasijue chochote, wala wasitende kazi yoyote, mpaka siku ya hukumu itakapofika, ambapo watatolewa huko kisha watasimama kwenye kiti cha enzi cheupe cha mwana-kondoo kwa ajili ya hukumu, (Ufunuo 20) baada ya kuhukumiwa ndipo watakapotupwa kwenye ziwa la moto, na kuangamia milele.
Sasa wakiwa huko kuzimu, ambapo kwa jina lingine kunaitwa Jehanamu, ni mahali pa shida, dhiki nyingi na mateso yasiyoelezeka, huko hakuna maisha, ni mateso tu vifungoni.
Hivyo ndugu, unapomwamini Yesu ipo faida kubwa zaidi ya unavyofikiri, unapokea MAISHA YA MILELE, Tangu ukiwa hapa duniani, ndani yako hakuna kitu kinachoitwa kifo, wala hutakihisi hata kidogo. Kwanini leo usimkaribishe maishani mwako? Ikiwa upo tayari basi wasiliana nasi kwa namba hizi kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba, bure.
Au sema sala hii kwa Imani, na Moja kwa moja Yesu ataingia moyoni mwako.
Bwana akubariki
AINA ZA FARAJA BWANA AZIACHILIAZO KWA WATUMISHI WAKE.
ASIYEMPENDA BWANA NA AWE AMELAANIWA.