Hebu tengeneza picha umeajiriwa, halafu aliyekuajiri anakutumikisha kwa mateso makali na mwisho wa siku anakulipa mshahara wa kifo!, Je kabla ya kuanza hiyo kazi, utakubali kutia sahihi mkataba huo??
Bila shaka kwa mtu mwenye akili timamu, hawezi kukukubali.
Lakini ajabu ni kwamba Zaidi ya nusu ya wanadamu wa kizazi chetu, wametia sahihi na huyu boss, ambaye anawatumikisha halafu anawalipa mshahara wa kifo. Je unataka kumjua huyu boss mkatili, na tena mwenye mshahara mbaya wa kifo?.. Biblia imemtaja ni nani katika Yohana 8:34-35 na Mshahara wake ni upi katika Warumi 6:23.
Yohana 8:34 “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni MTUMWA WA DHAMBI”.
Mtu anayetenda dhambi, tajiri wake ni DHAMBI!.. Dhambi ni boss mbaya asiye na huruma…na huu ndio mshahara wake..
Warumi 6:23 “Kwa maana MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI….”.
Huyu boss hamdhulumu mtu, bali “anamlipa mtu mshahara tena kwa wakati”… kwasababu kila anayefanya kazi anastahili malipo biblia inasema hivyo katika (Luka 10:7 na 1Timotheo 5:18).
Dhambi inaua.., dhambi inaua.., dhambi inaua…, dhambi inaua..! Dhambi inaua,..Dhambi inaua…
> Dhambi inaua ule Upendo mdogo uliopo ndani yako
> Yale mahusiano madogo uliyoyaanza na Mungu wako, dhambi inayaua, inakusababisha kabisa usioune uso wa Mungu,… Tena biblia inasema inasema “Inafarikisha”…kufarikisha sio “kufarakanisha”… Kufarikisha inatokana na neno “kufariki” yaani “kufa/kutengwa”
Isaya 59:2 “lakini maovu yenu YAMEWAFARIKISHA ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”
> Dhambi inaua “furaha” ndogo na kubwa uliyonayo..
> Dhambi inaua “amani” na kuleta hofu.
> Dhambi inaua “wema” mtu alionao.
> Dhambi inaua “ndoa”
> Dhambi inaua huduma/karama/kipawa.
> Dhambi inaua “Heri” za mtu.
> Dhambi inaondoa “Baraka” za mtu
Mwisho dhambi inaua “Mwili”….. huyu ni boss asiyefaa, mwenye mkataba Mbovuuu!!!!…Tumkimbie! Na kumwendea Bwana YESU, ambaye yeye anasema Nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi, nasi tutapata raha nafsini mwetu (Mathayo 11:28).
Tukimkimbilia Bwana YESU anatufungua kutoka kwa huyu mwajiri mbaya (dhambi) na kutuweka huru.
Yohana 8:35 “Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Yohana 8:35 “Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Bwana YESU anatulipa UZIMA badala ya KIFO…. na si Uzima tu, bali UZIMA WA MILELE.
Bwana anamlipa mtu uzima katika Nafsi yake.
Unaongeza uzima juu ya upendo wa mtu, lakini dhambi inaua!
Bwana YESU anaongeza Uzima juu ya Amani ya mtu, lakini dhambi inaua!
Bwana YESU anaongeza Uzima juu ndoa ya mtu na maisha kwa ujumla, lakini dhambi inaua!
Na Zaidi ya yote, Bwana YESU anamlipa Mtu UZIMA WA MILELE (Yaani maisha baada ya hapa)..Kwanini tusimchague huyu??.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Je unaye tayari?..kama bado unangoja nini?.. kwanini dhambi ikukaushie uzima wako wa hapa duniani na ule wa milele ujao??..na matunda ya dhambi ni yale yote yaliyotajwa katika Wagalatia 5:19-20.
Wakati uliokubalika ni sasa, mkaribishe YESU leo maishani mwako akuweke huru.
Ikiwa bado hujampokea Bwana YESU na unahitaji msaada huo basi wasiliana nasi, tutakusaidia buree.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
TENDA JAMBO LA ZIADA.
ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.
Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.
Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?
UFALME WAKO UJE.
Rudi Nyumbani
Print this post