JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

2 Petro 1:3

[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 

Kuna mambo makuu sana ya kujifunza ndani ya vifungu hivi;

Hapo tunaonyeshwa kuwa Mungu anao Uweza wake. Kama vile tu mwanadamu alivyo na uweza wake usiokuwa sawa na mbwa. Kwamfano mwanadamu anaweza kuunda silaha, ambayo inaweza teketeza mji mzima kwa maarifa yake. Anauwezo wa kuruka angani zaidi ya kiumbe chochote duniani kwa vyombo alivyovibuni, anaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali sana hata na kuona uso wake kwa vyombo vya mawasiliana alivyojibunia.Mambo ambayo mnyama hawezi. Huo ni uweza wake wa kibinadamu.

Vivyo hivyo na Mungu wetu, anao uweza wake wa uungu, ambao ametukirimia sisi, Tunapoupokea huo  tunakuwa na sifa kama zake.

Ndio hapo anasema…

“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.

Lakini sasa nataka uone hapo uweza huo umeshushwa juu yetu, si katika kila kitu bali  katika mambo mawili makuu.

1) La kwanza ni uzima.

2) la pili utauwa.

Yaani mambo yote yanayohusiana na uzima wetu, ametuwezesha yeye mwenyewe. Ndio maana kwa kumwamini Yesu tunapokea msamaha wa dhambi. Tunakuwa tumevuka kutoka  mautini kuingia uzimani. Hatuangamii, tunakuwa na uzima wa milele ndani yetu.

Kwasababu Hatuna kifo ndani yetu, tunalala tu, kupumzishwa ili baadaye tuamshwe. Lakini Uzima huu hauwezi kuupokea kwa juhudi zako, au kwa elimu yako, au kwa matendo yako mema, au kwa dini yako nzuri, hapana..Ni zawadi ya Mungu kupitia Kristo Yesu. Pale unapomwamini tu, unapokea msamaha wa dhambi zako, kwa neema, huu ni uweza wake wa ajabu, ambao wanadamu wanausumbukia hawaupati, kwasababu mwanadamu hana matendo mema ya kutosha kuununua uzima. Isipokuwa Yesu tu peke yake alitununulia kwa damu yake.

Yohana 3:36

[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. 

Lakini sio tu Uzima, uweza huo umetukirimia pia na katika Utauwa wote. Utauwa ni utakatifu. 

Mtu ambaye hajaokoka hawezi yatoa maisha ya utakatifu ndani yake. Vinginevyo atajitahidi sana kwa kuutumikisha mwili kwa nguvu, na hatimaye atashindwa, au atafanya kinafki kama mafarisayo na waandishi, ambao walikuwa wananena mambo ambayo hawayatendi,.kwasababu uweza huu haukuwa ndani yao.

Utauwa haswaa ni kazi ya Mungu mwenyewe mioyoni mwetu kupitia Roho Mtakatifu. Ni pale mtu anapompokea Kristo kama mwokozi wake, kisha kukubali kumtii, kwa kujikana nafsi yake. Ndio hapo hapo yeye mwenyewe anakuongezea nguvu, ambayo inakufanya uyakimbie yale maisha ya kale ya dhambi. Lakini kumbuka hiyo inakuja kwa kukubali kumtii Yesu, kukubali kuwa kiumbe kipya. Wakristo wengi wanataka Bwana awasaidie lakini hawataki kujikana nafsi zao wasaidiwe na Bwana. Ukimpokea kwa mdomo tu uweza huu hautakuwa na matunda ndani yako. Lakini ukiwa ni wa geuko la kweli, uweza huo ni lazima utende kazi ndani yako.

Utaweza kushinda zile dhambi ambazo ulikuwa huwezi ziacha.

Yohana 1:12

[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 

Unaposema Yesu ni BWANA wangu. Ni lazima, ujue unajifanya kuwa mtumwa wake.. sikuzote bwana yoyote humiliki mtumwa, chochote anachoagizwa.huwa ni amri kwake sio ombi. Kumbali kuongozwa na Yesu, acha kabisa wokovu wa mdomoni.

Kama mkristo, kuwa mtakatifu ni lazima sio chaguzi, ndio kitambulisho chako kuwa umepokea uzima wa milele. Kwasababu pasipo huo huwezi kumwona Mungu (Waebrania 12:14).

Hakikisha uweza wote huu umeupokea ndani yako. Usiseme hicho kingine cha utakatifu hakinihusu, vinginevyo utakuwa hujakamilika

Shalom.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.

Je! Utatu mtakatifu upo kibiblia?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments