Katika mapokeo ya kikristo, moja ya eneo ambalo limezuia mikanganyiko mingi, ni eneo hili linalohusiana na “Uungu wa Mungu” . Migawanyiko ya madhehebu mengi unayoyaona sasa chimbuko kubwa hasaa ni hapa.
Wapo wanaoamini Mungu ni mmoja amegawanyika katika nafsi tatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu), lakini wapo wanaoamini Mungu ni mmoja mwenye nafsi moja (Hajagawanyika), yaani Yesu ni Yule Yule Yehova aliyekuwa zamani zile, wengine hawaamini kabisa kama Yesu anastahili kuwekwa katika nafasi ya uungu, wengine hawaamini kuwa Roho Mtakatifu ni halisi, bali ni nguvu tu ya Mungu, ni Yesu na Mungu tu basi. Je! Ukweli ni upi? Na Je tunapaswa tusimamie wapi?
Jambo la kwanza kufahamu, ni kuangalia kiini, cha kumjua Mungu? Kama kiini kimeharibika hapo ndipo penye shida kubwa. Tunaposema kiini, tunamaanisha idadi ya miungu. Cha ajabu ni kwamba makundi yote haya yanaamini “Mungu ni mmoja”, sawasawa na maandiko yanavyosema..
Marko 12:29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, BWANA MUNGU WETU NI BWANA MMOJA; 30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
Marko 12:29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, BWANA MUNGU WETU NI BWANA MMOJA;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
Tena kizuri zaidi ni kwamba wote wanaamini kazi ya Kristo ya ukombozi, wanaamini pia kazi za Roho Mtakatifu mioyoni mwetu.
Kinachotofautisha ni kutambua tu, nafasi zao za kiungu. Hilo tu, ambalo kimsingi halina nguvu sana, zaidi ya kuzitambua kazi zao mioyoni mwetu. Ni sawa na watu wawili wanaoshindania kama MUWA, ni jamii gani ya mmea, mmoja anasema ni tunda, mwingine anasema ni aina ya jani. Embu jiweke wewe katika hiyo nafasi, ukiulizwa swali hilo utasema ni nini?. Ni rahisi kusema “muwa” ni tunda, lakini kibaolojia muwa ni jamii ya “jani”, isipokuwa limerefu tu zaidi ya mengine na lina maji matamu, .
Sasa je! Kufahamu kama ni jani, au ni tunda? Maarifa hayo yanaweza kubadili asili yake? Kwamba ukifahamu sukari yake itaongezeka, au itawabadilikia maumbo. Wewe na yeye hamna tofauti, kiladha, isipokuwa kiufahamu tu.
Vivyo hivyo na kwenye uungu wa Mungu, Tunatafuta “UJUZI”. Na ujuzi ni mzuri, lakini mara nyingi tunapoung’ang’ania sana haujengi, bali huleta matengano, Ni upendo tu ndio unaojengwa.
1Wakorintho 8:1b…Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga
Ndio maana kwanini hatushangai kuona kanisa la kwanza, liliweza kutembea katika utimilifu wote wa ki-Mungu ijapokuwa hawakuwa na maarifa ya kutosha ya kutambua uungu wa Yesu, vema, isipokuwa baadaye sana katika nyaraka za mitume, ambayo hata hivyo waliita ‘Siri ya Mungu’. Lakini hao hao waliweza kumwabudu Kristo, lakini pia wakamwabudu Baba, bila shida yoyote, wapo waliotambua siri hii, lakini wapo ambao hawakutambua vema.
Kuonyesha kuwa hilo sio jambo la kung’ang’ania sana kana kwamba usipojua utakwenda kuzimu, kama inavyochukuliwa leo, mpaka kutupelekea matengano.
Ukweli ni kwamba Mungu wetu ni Yule Yule mmoja, isipokuwa ametenda kazi kwenye nafasi tatu tofauti kwa lengo la kumkamilisha mwanadamu, na sio yeye. Na sio kana kwamba ni watu watatu wamepatana katika jambo moja. Ni sawa na maji, mvuke na barafu. Vyote vitatu vikiwekwa pamoja vinaweza kuonekana na vitu tofauti tofauti kabisa, lakini ni kitu kile kile kimoja, ambacho ni maji. Ndivyo alivyo Mungu wetu.
Kutembea katika ofisi ya ubaba, na wakati huo huo mwana, na wakati huo huo Roho Mtakatifu, sio shida kwake, amefanya hivyo ili sisi tukamilishwe. Kama mwanadamu asingeanguka hakukuwa na haja ya Mungu kujifunua katika ofisi zote, angebakia katika ubaba wake ule ule mmoja,
Ni sawa na mtu aliyebuni simu, kama kusingekuwa na changamoto ya umbali ya nini mtu kuzungumza kupitia kifaa hicho?. Vivyo hivyo Mungu kuuvaa mwili, ni ili kutuunganisha sisi na yeye, katika mahusiano ambayo tuliyapoteza pale Edeni. Baadaye akaingia kabisa ndani yetu, kwa Roho wake Mtakatifu, kiasi kwamba sasa tunamwabudu Mungu wetu moja kwa moja ndani ya mioyo yetu.
Kwahiyo, Mungu wetu hajagawanyika. Ni Yule Yule mmoja, wala hana nafsi tatu, bali moja. Wala hakuna mahali kwenye maandiko yanathibitisha kuwa Mungu anazo nafsi tatu. Lakini hilo si jambo la kuzozana nalo, kwa wanaoamini Mungu anazo nafsi tatu, maadamu hawaamini miungu mingi. Akimwabudu Baba, ni Yule Yule, akimwambudu Yesu ni yuleyule Mungu, akimwabudu Roho bado haabudu Mungu mwingine zaidi yake yuleyule mmoja. Hilo ni suala tu la kiufahamu ambalo halimwondolei mtu wokovu.
Hivyo ikiwa wewe ni mkristo, umemwamini Kristo kama ni mwokozi wako, na mwenzako pia kampokea kama wewe tu ulivyopokea, lakini haamini kama ni Mungu bali ni mwana wa Mungu. Lakutosha, usishindanie mambo ambayo ni ya ujuzi. Mwombee tu, Mungu ampe ufahamu kamilifu, kwasababu kujua kama utatu mtakatifu ni sahihi au sio sahihi hilo haliwezi kumtenga na Mungu wake, maadamu haubudu nje ya hao. Tukue kiufahamu, tusimpe adui nafasi ya kuleta mtengano yasiyo na maana.
Kwa maarifa ya ndani zaidi kuhusu, mafundisho ya uungu wa Mungu pitia haya masomo >>>
JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?
Je Yesu ni Mungu au Nabii?
MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
UUNGU NI NINI? (1Petro 1:3-4)
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
Roho Mtakatifu ni nani?.
Rudi Nyumbani
Print this post