UUNGU NI NINI? (1Petro 1:3-4)

UUNGU NI NINI? (1Petro 1:3-4)

2 Petro 1:3  Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe

4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

Uungu ni Ile Hali ya kuwa kama Mungu.

Kwamfano mtu anayefanya vitendo viovu kama vya  uuaji, utoaji mimba, uchawi, ushoga tunasema anafanya “Ushetani”.. Kwasababu anatenda kazi za shetani. 

Vivyo hivyo tunaposema “Uungu”. Tunamaanisha kuwa kama Mungu, au kufanya kazi kama za Mungu, au kuwa na sifa za Mungu ndani yako.

Na Tabia ya Mungu ndani ya Mtu. Si Kila mtu anazo. Bali ni wale tu waliozaliwa na yeye. Yaani waliokoka

Hizi ni baadhi ya Tabia za kiungu.

1. Uzima wa milele:

Kitu ambacho Mungu anawakiria watu wake waliompokea ni uzima wa milele. Ambao upo ndani yake. Mwanadamu wa Tabia ya asili Hana uzima wa milele ndani yake. Akifa Hana Tumaini la kuishi. Lakini aliyezaliwa mara ya pili. Huishi milele. Kwasababu uungu upo ndani yake.

Yohana 10:34  “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?”

Ukiwa kama mwana wa Mungu sifa hii ni lazima itaonekana ndani yako. Hakikisho la uzima wa milele, mwovu hana uzima wa milele.

2. Matunda ya Roho

Pili mtu mwenye uungu ndani yake, anatoa tabia za Mungu ndani yake, ndio zile tabia za Roho tunazozisoma katika Wagalatia 5:22, kama vile Upendo, , fadhili, uaminifu, utakatifu n.k.

Wagalatia 5:22-25

[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, [23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. [24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. [25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

Mambo ambayo huwezi kuyaona kwa mtu mwenye tabia ya asili. Yeye huwa kinyume chake, au akijaribu kufanya basi ni kwa unafki, kwasababu havipo moyoni mwake.

3. KUSHINDA DHAMBI:

Na pia mtu mwenye tabia ya uungu unakuwa na uwezo wa kuushinda ulimwengu(yaani dhambi) kama vile Kristo alivyoushinda ulimwengu..

1 Yohana 3:9

[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

Maana yake,dhambi inakuwa haina nguvu ndani yake. Maandiko yanasema hata wao wenyewe wakishangaa tunawezaje kuishi  maisha ya mbali na dhambi (1Petro 4:4). Hawajui  Ni kwasababu sisi tuna tabia za uungu ndani yetu.

Maandiko mengine yanayoeleza Neno uungu. Ni haya  (Matendo 17:29, Warumi 1:20).

Bwana akubariki.

Je! Na wewe utatamani uwe na tabia za Ki-Mungu ndani yako?. Ni wazi kuwa hii ni kiu ya kila mmoja wetu. Kama ni hivyo basi, hauwezi kwa akili yako au nguvu zako, bali kwa Roho wa Mungu. Kwasababu biblia inasema wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika wana wa Mungu (Yohana 1:12). Hivyo huu ni uwezo utokao kwa Mungu mwenyewe, na sio kwa mwanadamu. Na tunaupata kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kwa kumkiri Yesu, na kumfanya kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu. kisha kumpa nafasi ya kuyatawala maisha yetu.

Hivyo basi ikiwa upo tayari siku ya leo kutubu dhambi zako, ili Bwana akufanye kiumbe kipya. Basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa Sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

Uzima wa milele ni nini?

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

DANIELI: Mlango wa 12.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments