Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?

Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?

SWALI: Kwanini Mungu alimuadhibu Eli kwa kosa la kutowaonya watoto wake, angali tunasoma katika maandiko aliwaonya hapo kabla?

Tusome;

1Samweli 2:22 Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. 

23 Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote.  24 Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana. 

25 Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua.

Lakini Hapa Mungu anasema…

1Samweli 3:12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho. 

13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye HAKUWAZUIA. 

14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.


JIBU: Kibiblia “Kuonya” sio tu kusema kwa mdomo, bali pia kuchukua hatua stahiki, endapo maonyo hayatatekelezwa. Eli ni kweli aliwaonya watoto wake, kwa dhambi walizokuwa wanazifanya madhabahuni pa Mungu, lakini aliendelea kuwaangalia, wakifanya mambo yao maovu bila kuwaondoa katika nafasi zao. Ndio maana hapo kwenye 2Samweli3:13 Mungu anamwambia Samweli, kwamba HAKUWAZUIA. Hakuwaondoa katika kazi ya utumishi, Pengine kwasababu ni watoto wake, warithi wake, akawastahi zaidi ya  Mungu. Hivyo wakati wa adhabu ulipofika yeye naye alishiriki adhabu ile.

Hili ni funzo, pia kwa viongozi wote wa imani, nyakati hizi tunazoishi, kanisa limegeuzwa kama mahali pa kila mtu kujiamulia jambo lake, na viongozi wanaona wanafumbia macho. Utakuta mchungaji ni mzinzi, lakini askofu akipata taarifa, badala wamwondoe katika ofisi ile, wanamwonya tu, kisha wanamuhamisha dayosisi, wanamstahi, na akifika kule anaendelea na maovu yake, anahamishwa tena dayosisi.

Utakuta watoto wa wachungaji, ni walevi, hawana maadili, lakini wanaendelea kubaki katika nafasi za wazee wa kanisa au waimbaji kwaya. Mchungaji akiambiwa, anachokifanya ni kuwaonya tu, lakini bado wanaendelea kushika nafasi hizo za madhabahuni. Hii ni hatari. Mungu anataka hatua stahiki zifuatane na maonyo kama hakuna mabadiliko.

Hivyo kama wewe ni kiongozi, kumbuka maonyo yako ni lazima yaambatane na vitendo.

Bwana atusaidie.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini Kuhani wa Mungu Eli alikufa kwa kuvunjika shingo?

IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments