Jibu: Jina la Bwana Yesu Kristo lisifiwe daima.
Matoleo ni Neno la ujumla linalomaanisha aidha sadaka, au michango.
Neno Matoleo linatokana na neno “Kutoa” Hivyo chochote kile mtu anachokitoa kwa Mungu wake kinaitwa Matoleo.
Lakini sadaka ni toleo rasmi ambalo linalenga moja kwa moja madhabahu, na matoleo ya sadaka tofauti na matoleo mengine kama michango ni kwamba sadaka inakuwa ni siri lakini michango mengine inaweza isiwe Siri,
Kwamfano yale matoleo Anania na Safira mkewe waliyoyatoa ya kuuza viwanja na kuleta thamani yake chini ya miguu ya mitume, hayakuwa siri, bali lilikuwa ni jambo linalowekwa wazi kwa wote.
Lakini sadaka haipaswi kuwa kitu cha kuonyesha mbele za watu, bali kinapaswa kiwe siri ya mtu na Mungu wake…kama Bwana wetu Yesu alivyotufundisha.
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”. 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Na Matoleo yote (iwe changizo au sadaka). Yana thawabu kubwa mbele za Mungu kama yakitolewa kwa nia njema na dhamiri njema na kulingana na Neno la Mungu,na Mungu anayaangalia sana.
Ukiahidi au ukipanga kumtolea Mungu kitu, basi hakiksha unatimiza kama ulivyoahidi au ulivyopanga pasipo kupunguza hata kidogo, ili isiwe kwako dhambi kama ilivyokuwa kwa Anania na Safira mkewe, ambao waimdanganya Roho Mtakatifu kwa matoleo yao.(Matendo 5:1-11).
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +25569303661
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
Rudi nyumbani
Print this post
Je, wachungaji kupokea sadaka na kutumia vile waumini hawajui ni mpango wa Mungu? Na je, wao wanastahili kula hizo sadaka? Na je, sadaka zinakazi gani kwaajili ya kanisa?
Muktadha mzima wa sadaka ni siri… inapotolewa na mtu yeyote hana uhalali nayo tena, isipokuwa inakuwa chini ya viongozi waliotiwa mafuta na Bwana kuzipangia kazi za kufanya..