Shalom! Mwana/binti wa Mungu, karibu tuyachunguze maandiko, natumaini leo utajifunza jambo jipya litakalokusaidia katika maisha yako ya maombi..Embu jaribu kufikiria mfano huu watoto wawili mapacha wamemfuata baba yao tajiri kwa faragha na kumwomba awapatie kitu..mmoja kamwambia baba nimeona suruali nzuri dukani naomba uninunulie, na mwingine akasema baba nimeona ndege kubwa inapita angani, naomba uninunulie na mimi niwe na ya kwangu niendeshe..We unadhani maombi ya nani yatakuwa ya kwanza kujibiwa kwa haraka zaidi ya mwingine?..Ni wazi kuwa aliyeomba nguo inawezakana isipite hata siku awe ameshatimiziwa haja yake..Lakini huyo mwingine japo aliomba na mwenzake katika muda mmoja, japo walisikiwa wote katika muda mmoja, japo baba yao aliwahidi wote kuwapa walivyoviomba, lakini majibu ya huyu wa pili, yanaweza yasije kwa wakati alioutarajia, inaweza kumgharimu mambo mengi sana, ikiwemo muda, na maisha.