Je! Adamu na Hawa walizikiwa wapi?

Je! Adamu na Hawa walizikiwa wapi?

JIBU: Ipo mitazamo mingi, ihusuyo eneo halisi la makaburi ya wazazi wetu wa kwanza, Kwamfano kwa mujibu wa hadithi za kiyahudi, wao wanaamini kuwa Adamu na Hawa walizikwa pale Israeli, mahali palipoitwa Hebroni katika pango lijulikanalo kama pango la  Makpela. Ambalo baadaye Ibrahimu na Sara walikuja kulinunua likawa ni eneo la maziko yao ya kifamilia, (Mwanzo 49:29-31)  kwa  urefu wa habari hiyo fungua hapa usome >>> Pango la Makpela ni lipi,

Wengine, wanaamini kuwa pale Kristo  aliposulubiwa Golgota, ndipo palipokuwa kaburi la Adamu, wakiamini kuwa kama Kristo alivyoitwa Adamu wa pili, maana yake ni alikuja kurudisha kile kitu ambacho Adamu wa kwanza alikipoteza, yaani uzima. Hivyo kama Adamu alileta kifo, Kristo alileta uzima kwa msalaba wake, na aliyafanya hayo  juu ya kaburi la Adamu.

Lakini je! kuna usahihi kwa mitazamo hiyo.

Kwasababu biblia haijaeleza chochote, kuhusiana na kaburi la Adamu na Hawa, hii yote ni mitazamo, ambayo yaweza kuwa ukweli au uongo, tusiweke imani yetu moja kwa moja katika mitazamo. Kwasababu gharika ilipokuja ilivuruga ramani yote ya ulimwengu, isingekuwa rahisi kupatambua mahali sahihi alipozikwa Adamu, isipokuwa kwa ufunuo.

Na habari hiyo kutoandikwa ni kutuonyesha kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua Adamu alizikiwa wapi. Ushindi tulioupata kwa kifo cha Kristo, na kufufuka kwake, ni habari tosha tunayopaswa tuitafakari usiku na mchana, zaidi ya kaburi la Adamu.

Lakini swali ni Je! Yesu amefufuka ndani yako? Fahamu kuwa  Ikiwa bado hujazaliwa mara ya pili, kifo kina nguvu juu yako, ukifa hakuna maisha kwako, ni mateso katika moto wa jehanamu. Lakini ukizaliwa mara ya pili uzima wa milele unao na hata ukifa, utakuwa unaendelea kuishi.

Yohana 11:25  “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26  naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

Unasubiri nini? Usiokoke leo.

Saa ya wokovu ni sasa, ni pale tu unapotubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kumwita Yesu ayatawale maisha yako, kisha kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Hapo unakuwa tayari umezaliwa mara ya pili. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua hapa kwa mwongozo wa Sala hiyo ya toba.>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?

JINA LAKO NI LA NANI?

Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments