Kwa kiyahudi huitwa ‘Tevat’, ni chombo cha majini kilichotumika mahususi kwa ukombozi. Ni mfano wa meli iliyotumika kuokoa watu/wanyama kutoka katika maangamizi fulani. Kwamfano katika biblia tunaona Nuhu aliagizwa atengeneze safina, ambayo ataingia yeye pamoja na familia yake, na wanyama wa nchi.
Ukisoma Mwanzo 6-8, utapata kufahamu vipimo vya safina hiyo vilivyokuwa na vigezo vyake, japokuwa biblia haijatueleza mahususi umbo la chombo kile kilivyokuwa.
Lakini pia wakati Musa anazaliwa, tunaona wazazi wake walimtengeneze a naye kisafina kidogo, akafichwa ndani yake, ili kunusuriwa na maangamizi ya Farao.
Kutoka 2:1 Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi.
2 Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.
3 Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto.
Jambo la muhimu kufahamu ni kuwa safina hizo ilikuwa ni lazima zipakwe LAMI ndani na nje. Lami hizo ni mfano wa gundi nzito zilizopakwa, lengo lake likiwa ni kuzuia maji yasiweze kupenya sehemu yoyote ndani ya Safina, (Mwanzo 6:14, Kutoka 2:3). Safina zilikuwa na sifa kama za “nyambizi” tulizonazo sasa, ambazo hazihathiriwi na maji mahali popote ziwapo juu au chini ya maji.
Ni Kristo Yesu, yeye ndiye mwokozi wetu dhidi ya ghadhabu ya Mungu juu ya ulimwengu huu kwa wenye dhambi. Na DAMU yake ndiyo ile LAMI. Inayonyunyizwa kwetu sisi. Mtu yeyote ambaye hajamwamini Yesu, ni dhahiri kuwa ghadhabu ya Mungu ipo juu yake, hawezi kuiepuka. Kwasababu amekataa msamaha wa dhambi, tuliopewa bure kwa kifo chake pale msalabani.
Je! Unaichezea neema? Kumbuka ulimwengu huu unafikia mwisho. Kristo amekaribia kurudi, kuwanyakua watu wake. Je! Bado upo kwenye dhambi? Ikiwa utataka kuupokea wokovu leo bure, basi uamuzi huo ni bora kwako, Hivyo waweza, fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala hiyo ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.
Mvinje ni mti gani? (Mwanzo 6:14)
About the author