Mvinje ni mti gani? (Mwanzo 6:14)

Mvinje ni mti gani? (Mwanzo 6:14)

Swali: Mti wa Mvinje uliotumika kutengenezea safina kulingana na Mwanzo 6:14 ndio mti gani kwasasa?.

Jibu: Tusome,

Mwanzo 6:13 “Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. 

14 Ujifanyie safina ya MTI WA MVINJE; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami”.

Mti wa Mvinje ni jamii ya miti inayoota karibia sehemu kubwa ya dunia, ikiwemo barani Afrika (Tazama picha juu).

Sifa ya miti hii ni migumu sana na Imara, lakini iliyo kuu kuliko zote ni uwezo iliyonayo ya kutoathiriwa na maji.

Tofauti na miti mingine, ambayo adui wake wa kwanza ni maji, (inapogusa maji basi inaoza), lakini Mti wa Mvinje wenyewe hauathiriwi na maji, hivyo kufanya mbao ya mti huo itumike kwa matumizi ya kutengeneza boti ndogo ndogo na hata kubwa (boti za wavivu na baadhi ya za abiria zinatengenezwa kwa kutumia miti hii), vile vile mbao ya mti wa Mvinje inatumika kutengenezea viti vya viwanja vya michezo na sehemu za Uma, na vile vile inatumika kutengenezea viungio vya barabara za treni (Reli), na matumizi mengine ya samani za ndani kama vile milango na makabati.

Kwa sifa miti hiyo iliyoibeba ndiyo ikawa sababu ya Mungu kumwambia Nuhu ajenge safina kwa kutumia miti hiyo, kwani ingetumika miti mingine huenda isingeweza kuvumilia kudumu juu ya maji kwa miezi yote ile mitano, kwani maandiko yanasema mvua ilinyesha siku 40 usiku na mchana, na maji yalidumu juu ya uso wa nchi siku 150 (Miezi 5) soma Mwanzo 7:4,24.

Maandiko mengine katika biblia yanayohusu mti wa mvinje ni pamoja na Isaya 6:13 na Isaya 44:14.

Lakini leo hii mvinje wetu ni nini?

Mti wa Mvinje leo hii si mwingine Zaidi ya msalaba utuokoao sisi na dhambi zetu, na safina yetu ni Bwana Yesu Kristo, tuwapo ndani ya Kristo basi gharika ya ghadhabu ya Mungu ambayo imekusudiwa kumwagwa katika siku hizi za mwisho haitatupata.

Je umeokoka? Kama bado unasubiri nini? Kumbuka dunia hii inaenda kuisha, tupo nyakati za majeruhi na unyakuo umekaribia.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mretemu ni mti gani?

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Mwerezi ni nini?

FANYA BIDII ZOTE ULE MATUNDA YA UZIMA.

JE NI KUTII AU KUPATA KWANZA MAARIFA?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments