Swali: Simo ni nini, au ni nani kama tunavyosoma katika Ayubu 17:6.
Jibu: Tusome mistari hiyo mpaka ule wa saba (7).
Ayubu 17:6 “Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi. 7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli”
Ayubu 17:6 “Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.
7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli”
Neno hili “Simo” linasomeka tena katika Ayubu 30:9.
Ayubu 30:9 “Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao, Naam, nimekuwa simo kwao. 10 Wao hunichukia, na kujitenga nami, Hawaachi kunitemea mate usoni”.
Ayubu 30:9 “Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao, Naam, nimekuwa simo kwao.
10 Wao hunichukia, na kujitenga nami, Hawaachi kunitemea mate usoni”.
Na maana ya neno hilo (simo) ni “Ni maneno ya dharau, mtu anayoyatunga kwa mwingine”
Wakati Ayubu mtumishi wa MUNGU anapitia yale majaribu ya kufiwa na wanawe na kupoteza mali zake zote, na zaidi ya yote kupitia matatizo ya kiafya, ile fahari yake yote iliisha na kusababisha watu wengi kumdharau kwa maneno hayo ikiwemo mke wake.
Lakini pamoja na kuwa SIMO mbele ya watu, kwa MUNGU alikuwa LULU kubwa sana, kwani majaribu yale hayakuwa kwasababu ya yeye kumwacha MUNGU bali ni kwasababu ya yeye kumkaribia Mungu zaidi, na wakati ulipofika alipata mara mbili, ya alivyovipoteza na miaka mingi zaidi ya kuishi (Ayubu 42:12-16).
Na sisi tunajifunza mambo hayo hayo, kuwa tujaribiwapo kwaajili ya haki tuna heri…
Lakini tupitiapo majaribu mfano wa yale ya Ayubu tukiwa katika dhambi, tunapaswa tujifikiri mara mbili, kwani huenda ni mapigo na laana kutoka kwa Mungu ili tutubu na si kwa lengo la kuzijaribu imani zetu kama Ayubu.
Ndivyo Neno linavyoma katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 28.
Kumbukumbu la Torati 28:15-16,37-39 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. 16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. 37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA. 38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. 39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu”.
Kumbukumbu la Torati 28:15-16,37-39 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
Kwanini Mungu alimkataa Sauli? (1Samweli 15:23)
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
Rudi Nyumbani
Print this post