Ni vitu vipi hivyo tumekirimiwa vitupasavyo uzima na utauwa? (2Petro 1:3)

Ni vitu vipi hivyo tumekirimiwa vitupasavyo uzima na utauwa? (2Petro 1:3)

SWALI: Ni vitu vipi hivyo tumekirimiwa vitupasavyo uzima na utauwa? (2Petro 1:3)

2 Petro 1:3

[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia “vitu vyote” vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.


JIBU: Andiko hilo linatufundisha kuwa Mungu anao uweza wake, ambao una nguvu ya kumfanya mtu kuwa kama anavyotaka. Sasa hapo tunafunuliwa kuwa uweza huo ameuachilia katika maeneo mawili makuu la kwanza ni UZIMA la pili UTAUWA. Uzima ni maisha ya milele, na utauwa ni utakatifu.

Sasa swali linauliza ni vitu gani hivyo ambavyo Mungu ametukirimia vinavyozungumziwa hapo vitufanyavyo  kuufikia huo uzima na utauwa, anaousema?

Vitu vyenyewe ni kama vifuatavyo

1) Mwana wake (Yesu).

Bila Yesu Kristo kuja duniani, kuwa fidia ya dhambi zetu kwa kifo chake, tusingeweza kupokea uzima wa milele. Kwasababu ilihitajika kumwagika kwa damu isiyokuwa na dhambi ili kutuondolea sisi dhambi zetu tupokee uzima wa milele. Hivyo uweza huu wa uungu, umetukirima Yesu Kristo, kutuondolea dhambi ndani yetu.

Tuna kila sababu za kumshukuru Mungu sikuzote, kwa huruma zake hizi. Tunaye mkombozi ambaye kila amwaminiye tu. Uzima anao. (Yohana 3:16)

2) Roho Mtakatifu.

Roho wa Mungu ni msaidizi wetu, bila yeye, ni kweli tungesamehewa dhambi lakini tusingeweza kuwa watakatifu. Hivyo yeye anapokuja juu yetu na kujaa vizuri tunajikuta tunaweza enenda katika mwenendo wa utakatifu. Hivyo huu ni uweza wa Mungu mwenyewe.

Yohana 14:16

[16]Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

Wagalatia 5:16

[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

3) Biblia.

Hichi ni kitu kingine ambacho Mungu ametukirimia kwa uweza wake, kwa kuisoma tunatambua wazo lote la Mungu, na hivyo kuturahisishia kuisikia sauti ya Mungu. Tusomapo biblia tunabadilishwa tabia zetu, kwa maonyo, mafundisho, faraja, shuhuda n.k.

2 Timotheo 3:16

[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

4) Kanisa.

Kanisa ni uweza wa Mungu kwetu, hekima ya Mungu ambayo aliibuni yeye mwenyewe siku ile ya pentekoste. Kuwakusanya watakatifu wake na kuwahudumia kwa karama mbalimbali. Kanisa humlinda mwamini, kanisa humwombea mwamini, humsaidia mwamini, humfariji mwamini na kumwongoza.

Sikuzote  Uthabiti wa mwamini hutegemea kanisa. Mtu asiye na kanisa (ushirika), ameukana uweza huu wa Mungu, ambao Mungu huutumia kutukamilisha sisi.(Waebrania 10:25)

1 Wakorintho 12:27-28

[27]Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.

[28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.

5) Malaika

Bwana huwatuma malaika wake, kumlinda mwamini asijikwae. Huu ni uweza wa Mungu pia.

Waebrania 1:14

[14]Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Zaburi 91:11-12

[11] Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. [12] Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

Kama si Mungu kutuagizia malaika zake, bila shaka adui angepata penyo nyingi sana za kutuletea majaribu na kutuangusha. Ukiwa ndani ya Kristo adui hana nguvu juu yako, kwasababu unalindwa na jeshi lake. Unapiganiwa kwa namna usiyojua wewe.

Na hivyo kuishi maisha ya utauwa kwako inakuwa ni vyepesi zaidi ya mtu mwingine yeyote aliye nje.

Swali ni je umepokea vitu hivi vyote?

Ukipungukiwa kimoja wapo, ni lazima tu eneo lako la utauwa  au uzima litakuwa na kasoro. Kumbuka Bwana ameshatukirimia ni sisi tu kukubali na kupokea.

Wokovu upo bure, biblia ipo wakaki wote, Roho yupo, kanisani lipo, malaika wapo. Amini tu na  kutubu dhambi zako, kwa Kumaanisha kabisa kugeuka na kumfuata Yesu, akupaye ondoleo la dhambi. Kisha ukabatizwe, upokee Roho. Na baada ya hapo, shiriki sasa vitu hivyo vya ki-ungu kwasababu vimewekwa tayari kwa ajili yako na mimi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments