Je ni sala gani inahitajika kabla ya kumchinja mnyama katika ukristo?

Je ni sala gani inahitajika kabla ya kumchinja mnyama katika ukristo?

Swali: Je sisi wakristo tunapaswa tuombe sala gani kabla kumchinja mnyama?, maana Imani nyingine tunaona kabla kuchinja wanatanguliza sala.


Jibu: Katika biblia hatujapewa maagizo yoyote ya kuomba sala, au kukiri maneno Fulani kabla ya kumchinja mnyama. Ndio zipo Imani zinazoelekeza kufanya hivyo, lakini si Biblia takatifu.

Maagizo tu yaliyopo katika biblia ni kushukuru kabla ya kula..lakini kupiga sala kabla ya kuchinja hatujapewa kwani hatuendi kutoa sadaka kwa miungu bali ni kwaajili ya kitoweo.

Katika agano la kale, wanyama waliombewa kabla ya kuchinjwa iwapo wanaenda kutolewa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana (dhabihu).

Walawi 4:32 “Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.

33 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa”.

Lakini katika agano jipya dhabihu ya mwili wa YESU ilishatolewa, (hiyo ndio dhabihu kamilifu)…sasa wanyama wanachinjwa kwaajili ya vitoweo, na si kwaajili ya sadaka.. na hakuna sala yoyote inayotangulia, na hata wanaoomba hizo dua bado kuna viumbe vitawafunga katika sheria hiyo, kwamaana samaki au dagaa au wadudu kama kumbikumbi au senene unawaombeaje dua kabla ya kutoa uhai wao?… utaombea dagaa mmoja mmoja??..ni jambo lisilowezekana vinginevyo hatutakula kabisa.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba hakuna sala inayotangulia kabla ya kuchinja au kuutoa uhai wa kiumbe chochote kwaajili ya chakula.. Na kufahamu kwa urefu kama wakristo anaruhusiwa kula nyama ya mnyama aliyechinjwa kwa dua, basi fungua hapa >>UKWELI KUHUSU UISLAMU Sehemu ya Pili: (Jiwe/Jabali la Kaaba).

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments