Je “Kaaba” ni nini na ipo kwenye biblia?, Na wanyama wanaochinjwa kuelekea Kaaba je tunaruhusiwa kuwala?.
Angalizo: Makala hii haina lengo la kushambulia Imani Fulani, wala kushabikia Imani Fulani, pia haina lengo la kumchafua mtu yoyote, wala kumdhalilisha, bali kutoa elimu sahihi kuhusiana na tunayoamini na yanayoaminiwa.
Kama hujapitia sehemu ya kwanza ya Makala hii, inayohusu msikiti wa Al-Aqsa uliopo Yerusalemu pamoja na unabii wake basi waweza fungua hapa >>> UKWELI KUHUSU UISLAMU Sehemu ya kwanza: (Msikiti wa AL-Aqsa).
Leo tunaendelea na sehemu ya pili, na tutalitazama “Jiwe la Kaaba” na uhusiano wake na Imani ya kikristo.
“Kaaba” au kwa jina lingine al-Ka’ba al-Musharrafa ni jengo la “Jiwe Jeusi” lililopo katikati ya msikiti uitwao “Masjid al-Haram” uliopo mahali pajulikanapo kama “Makka”, huko nchini Saudi Arabia.
Jiwe hili linaaminika na dini ya kiislamu kuwa “nyumba ya mungu”. Na pia linaaminika kuwa ni ufunuo Mungu aliompa Abramu (Ibrahimu) pamoja na Ishaeli mwanae kama mahali pekee na sahihi alipopachagua Mungu pa kuabudia, kulingana na Quran, Al Imran 3:96 (Sasa kujua ukweli wa jambo hili kibiblia soma Makala hii mpaka mwisho).
Zaidi inaaminika kuwa mahali hapo “Kaaba (hapo Makka)” ndipo mahali ambapo Malaika walikuwa wakimwabudu Mungu kabla ya mwanadamu kuubwa, na baadaye mwanadamu alipoumbwa ndipo Adamu akapajenga tena mahali hapo kama sehemu ya kumwabudu Mungu, na baadaye baada ya mafuriko ya Nuhu mahali hapo pakapotea, pakawa hapajulikani, na alipotokea Ibrahimu ndio akapata ufunuo wa mahali hapo (kujua usahihi na ukweli wa jambo hili kibiblia soma Makala hii mpaka mwisho).
Baadaye kulingana na imani ya kiislamu, Abramu (Ibrahimu), aliambiwa awaambie wageni wote kutoka uarabuni na kila mahali wasafiri na kufika hapo kuhiji, na hiyo ndio sababu ya watu wa Imani ya kiislamu kuwasili huko Makka kuhiji kila mwaka.
Na si tu watu kuwasili pale, bali pia wanyama wachinjwapo wanaelekezwa (kibla) huko Maaka palipo na Kaaba.
Swali?.. Je ukweli wa mambo huu ni upi?
Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa Mwana wa Ahadi alikuwa ni Isaka mzao wa Sara, na si Ishmaeli aliyekuwa mzao wa kijakazi Hajiri.. Ingawa Mungu alimbariki pia Ishmaeli mwana wa Hajiri, lakini hakuwa amekusudiwa kubeba ahadi yoyote ya urithi wa mzaliwa wa kwanza, kwanini?.. kwasababu hakuwa mwana wa mke halali wa kwanza wa Abramu, na hiyo ndio sababu ya Sara kumfukuza Hajiri, na Mungu akawa upande wa Sara.
Mwanzo 21:9 “Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. 10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. 11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. 12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. 13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. 14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba”.
Mwanzo 21:9 “Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.
10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.
12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba”.
Sasa Imani ya kiislamu inaamini kuwa Ishmaeli(au Ismail) ndiye mwana wa ahadi halali wa Abramu, na biblia haisemi hivyo, na hapa ndipo MAKOSA YALIPOANZIA!!!!...Ndipo adui alipoanza kutengeneza MTI WAKE!!.
Na kwasababu hiyo, ya kuamini kuwa Ishmaeli ndiye mwana wa ahadi na si Isaka, basi ndipo zikazuka habari nyingine zisizo za kweli kwamba Abramu alishuka mpaka Makka na kupewa ufunuo uliopotea zamani kuwa mahali pa kuabudia ni hapo Makka, na pia zikatengenezwa habari nyingine kuhusiana na kisima maarufu kijulikanacho kama ZAMZAM, ambacho tutakuja kukiangalia katika Makala inayofuata na hatari yake kiroho.
Ukweli ni kwamba Abramu baada ya kumruhusu Hajiri aondoke na Ishmaeli, hakuendelea kufuatilia habari zake kwani Mungu alishamwambia amsikilize Sara, na ajihusishe na Isaka Zaidi ya Ishmaeli, hivyo si kweli kwamba Abramu aliwahi kushuka Saudi Arabia akiwa na Ishmaeli na kupewa ufunuo wa mahali hapo Makka, na hata biblia haionyeshi mahali popote jambo hilo.
Zaidi biblia inaeleza wazi kuwa baada ya Isaka kumzaa Yakobo, na Yakobo kulizaa Taifa la Israeli, kupitia Taifa hilo la Israeli alitokea Mfalme Daudi, ambaye baada ya kumpendeza sana Mungu, ndipo Mungu akauchagua mji wake Daudi (yaani Yerusalemu) uwe mahali pa kuweka nyumba yake na jina lake, na mahali pa kuabudia mpaka nyakati zake Masihi (yaani YESU).
2Nyakati 6:5 ”Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wo wote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu ye yote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli; 6 LAKINI NIMEUCHAGUA YERUSALEMU, JINA LANGU LIWE HUMO; NA DAUDI NIMEMCHAGUA AWE JUU YA WATU WANGU ISRAELI”.
2Nyakati 6:5 ”Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wo wote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu ye yote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli;
6 LAKINI NIMEUCHAGUA YERUSALEMU, JINA LANGU LIWE HUMO; NA DAUDI NIMEMCHAGUA AWE JUU YA WATU WANGU ISRAELI”.
Na tangu wakati ambapo Hekalu la Mungu lijengwe na Sulemani, mwana wa Daudi pale Yerusalemu, wenye Imani ya kiyahudi ndio walikuwa wanatoka Mataifa mbali mbali kwenda kuabudu pale, kwamaana ndio mahali alipopachagua Mungu aliweke jina lake.
Na hata watu wakiwa mbali walikuwa wanaabudu kuelekea Yerusalemu mahali hekalu lile lilipojengwa, mfano wake ni nabii Danieli katika Danieli 6:10, soma pia 1Wafalme 8:29-30.
Hivyo watu waliendelea kuwasili Yerusalemu mahali pale ambapo Mungu alipachagua, kwa miaka mingi ndio maana hata kibla ya kwanza ya uislamu ilikuwa ni hapo hapo Yerusalemu, walipokuja kujenga msikiti, mahali hekalu lilipojengwa, ingawa walikuja kugeuza na kusema si hapo tena bali ni Makka, penye “Kaaba”.
Na Masihi alipokuja (YAANI YESU KRISTO) ndipo atakapoonyesha sehemu sahihi ya kuabudia, alipopachagua MUNGU kabla ya kuwekwa misingi ya Ulimwengu, na kwamba watu wote wakusanyike hapo ili wamwabudu MUNGU sawasawa na mapenzi yake.
Kwani watu wote walijua kuwa siku Masihi atakapokuja atasahihisha mambo yote, na kuonyesha njia sahihi, sasa njia hiyo ni ipi?? Tusome maandiko yafuatayo..
Yohana 4:19 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, NANYI HUSEMA YA KWAMBA HUKO YERUSALEMU NI MAHALI PATUPASAPO KUABUDIA. 21 Yesu akamwambia, MAMA, UNISADIKI, SAA INAKUJA AMBAYO HAMTAMWABUDU BABA KATIKA MLIMA HUU, WALA KULE YERUSALEMU. 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. KWA MAANA BABA AWATAFUTA WATU KAMA HAO WAMWABUDU 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. 26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”.
Yohana 4:19 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!
20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, NANYI HUSEMA YA KWAMBA HUKO YERUSALEMU NI MAHALI PATUPASAPO KUABUDIA.
21 Yesu akamwambia, MAMA, UNISADIKI, SAA INAKUJA AMBAYO HAMTAMWABUDU BABA KATIKA MLIMA HUU, WALA KULE YERUSALEMU.
22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. KWA MAANA BABA AWATAFUTA WATU KAMA HAO WAMWABUDU
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”.
Umeona mahali sahihi alipopachagua Mungu pa Ibada?.. Si Yerusalemu tena, wala mahali pengine popote bali ni katika Roho Mtakatifu, na katika kweli ya MUNGU.
Maana yake kama mtu hana Roho Mtakatifu ndani yake basi hawezi kuwa na ibada halisi, kama hawezi kuutunza mwili wake na roho yake, basi hakuna mahali pengine popote duniani atakapoweza kumfanyia Mungu ibada akaikubali, kwasababu maandiko yanasema miili yetu ni HEKALU la ROHO MTAKATIFU (Soma 1Wakorintho 3:16 na 1Wakorintho 6:19).
Na Hekalu tafsiri yake ni sehemu ya nyumba ya ibada, hivyo ibada ya kwanza inaanza ndani ya mtu, hiyo ikiharibiwa mtu huyo hata aende wapi hawezi kumwona MUNGU wala kukutana na MUNGU, hata apae juu ya sayari zote, bado atakuwa mbali na Mungu na maombi yake hayasikilizwi.
Lakini kama akitakasika katika utu wake wa ndani na wa nje, basi mahali popote pale alipo ibada itakuwa inabubujika ndani yake, na hiyo ndio siri ya agano jipya.
Sasa swali ni je!, Wanaoenda Yerusalemu au Makka wanafanya makosa?
Kama mtu ataenda Yerusalemu kwa lengo la utalii, au kujifunza mambo, na pengine kumshukuru Mungu kwa atakayojifunza…hafanyi makosa lakini kama ni kwa lengo la Ibada, akiamini kuwa ile ni ardhi takatifu, hivyo atakokea kitu cha ziada, anakosea sana kwasababu Bwana Yesu alishasema.. saa yaja, nayo ipo, kwamba waabuduo halisi hawataenda tena Yerusalemu, bali watamwabudu katika roho na kweli.
Vile vile wanaoenda kuhiji Makka, wapo nje ya Imani kabisa, kwasababu hata huko Makka hapajaagizwa kabisa na Mungu, ni ufunuo wa ibilisi uliosambaa ili kuwafanya watu wasimwabudu MUNGU WA KWELI katika roho na kweli, badala yake katika makosa makubwa. Hivyo wanaokwenda kuhiji Makka wanahitaji msaada wa kumjua YESU, na NEEMA yake, ili watoke katika hayo makosa.
Hali kadhalika hakuna agizo lolote la mnyama achinjwapo basi aelekezwe Yerusalemu wala Makka, hayo pia ni maagizo ya ibilisi, ambayo yanalengo la kuingiza roho katika vile tuvilavyo.
Ikiwa nyama inauzwa buchani, Mkristo anaweza kuinunua akiongozwa na Amani ya Roho mtakatifu, na baada ya kuinunua anaweza kuitakasa kwa maombi, kisha akaitumia, lakini kama katika bucha hilo, wauzaji wamekiri waziwazi kuwa nyama hiyo imechinjwa kwa kuelekezwa kibla yoyote ile iwe ya Yerusalemu au Makka au penginepo popote nyama hiyo usinunue wala usile, kwasababu ya Dhamiri, ndivyo maandiko yasemavyo..
1Wakorintho 10:25 “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; 26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo 27 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri. 29 Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?”
1Wakorintho 10:25 “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;
26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo
27 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
28 Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.
29 Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?”
Usikose mwendelezo wa sehemu inayofuata wa Kisima cha Zamzam, na mengineyo.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
MJUE SANA YESU KRISTO.
DANIELI: Mlango wa 9
JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Rudi Nyumbani
Print this post