Zaburi 42:7
[7]Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tutafakari pamoja Neno la Mungu.
Biblia inatuambia kila jambo tunalolifanya lina matokeo sawa rohoni. Ikiwa wewe ni mwizi malipo ya wizi utayapata rohoni, ikiwa wewe ni muuaji, malipo ya uuwaji utayapokea vilevile rohoni, mito ya maji inapoelekea huko huko ndipo inaporudia.
Ufunuo 13:10
Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Sasa hapo tumeona katika eneo la ubaya, je vipi katika upande wa Mema?
Maandiko hayo hayo yanatuambia kwamba Kilindi hupigia kelele kilindi.
maana yake ni nini?
kilindi ni mahali pa katikati kabisa mwa bahari. Sasa mwandishi wa zaburi anatumia mifano ya kitu halisi kana kwamba kinaongea… anasema Kinaita chapigia kelele kilindi. Na cha kushangaza ni kwamba hakiiti eneo lingine lolote la maji labda ufukweni.. au kwenye rasi, au ghuba.. hapana bali kinapigia kelele kilindi chenzake.
Kilindi chapigia kelele kilindi
Maana yake ni nini?
Tukitaka mambo ya ndani ya Mungu, mambo ya vilindini, lazima na sisi tuwe vilindini. Ni muunganiko wa ki-Mungu. kila kiwango kina sauti yake. kamwe hizo sauti haziingiliani, ni sawa na mbwa amwite tai kwa sauti yake ya kubweka, haiwezekani kuja inahitaji, ajifunze sauti yake ili yule tai aelewe, vinginevyo atakuwa anapiga kelele tu.
Na sisi vivyo hivyo kwa Mungu, wengi tunatamani tumwone Mungu kwa undani katika maisha yetu, lakini hatutaki tuzame ndani yake.
Mwandishi wa Zaburi mwanzoni kabisa kabla hajasema maneno hayo kwenye hiyo sura 42 anasema
Zaburi 42:2-3
[2]Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? [3]Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
[2]Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
[3]Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
Kuonyesha ni mtu ambaye alimtamani sana Mungu wake.
Sehemu nyingine Daudi anasema..
Zaburi 63:1-8
[1]Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. [2]Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. [3]Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. [4]Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu. [5]Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. [6]Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. [7]Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. [8]Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
[1]Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
[2]Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.
[3]Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.
[4]Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
[5]Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
[6]Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.
[7]Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
[8]Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
Umeona, usiku kucha, anamtafakari Mungu, kuonyesha ni mtu ambaye moyo wake upo kwa Mungu asilimia mia..unategemea vipi mtu kama huyo Mungu asijifunue kwake kwa viwango vile?
Nafasi hii pia mimi na wewe tunayo. Tumfuate Mungu wetu vilindini, ili ajifunue kwetu katika viwango vingine..
Na hiyo inakuja kwa kile Bwana Yesu alichosema..Tujitwike misalaba yetu tumfuate, tuwe tayari kuacha vyote visivyompendeza yeye na kumtii. Na kwa kufanya hivyo rohoni tunatafsirika kuwa tunamwita Mungu wa vilindini.
Anza sasa.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
Ni kelele gani zinazozungumziwa hapo katika Waefeso 4:31.
NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
Rudi Nyumbani
Print this post