Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

SWALI: Naomba kufahamu maana ya 1Wakorintho 15:24-25 , hususani hapo anaposema ‘hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26  Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti’.

1Wakorintho 15:24  Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

25  Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

26  Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.


JIBU: Bwana Yesu alikuja duniani kwa kazi maalumu ya kumkomboa mwanadamu pamoja na kumkamilisha. Na ukombozi huu, aliukamilisha wote siku ile pale msalabani kwa kifo chake. Hivyo tangu wakati ule mwanadamu ambaye atampokea, tayari maadui zake wote wamewekwa chini yake, ikiwemo na mauti yenyewe.

Lakini pia ni muhimu kufahamu, ukamilifu wa ukombozi wetu, sio sasa, kwasababu ijapokuwa tumeokolewa na ndani yetu tuna uzima wa milele, bado tutakufa (ki-mwili), bado tutaugua, bado tutazeeka, bado tutakula kwa taabu, bado tutapitia dhiki na masumbufu, bado tutakutana na uovu kila mahali tuendapo.

Hivyo ‘ukamilifu’ wetu kabisa kabisa bado. Lakini ‘ukombozi’ wetu tayari, tunaokoka tukiwa hapa hapa duniani, tukifa tunakuwa tunaishi. Sasa Ndio maana Yesu alikuja mara ya kwanza kama MWANAKONDOO achukuaye dhambi za ulimwengu, lakini pia atarudi mara ya pili, ambapo safari hii atakuja kama MFALME, Atawalaye kwa mamlaka na nguvu nyingi.

Safari hii atakuja sasa kwa ajili ya huo ukamilifu, kwanza atayahukumu  mataifa na falme zao,(Mathayo 25:31-46) vilevile mapepo (Ufunuo 19:20), kisha ataurekebisha huu ulimwengu ulioharibika,(Ufunuo 6:12-17) na kuufanya kuwa zaidi hata ya edeni. Kisha atatawala na watakatifu wake, kwa kipindi cha miaka elfu moja (Ndio ule utawala wa amani wa Kristo wa miaka 1000), Ufunuo 20, hapa hapa duniani, kwa wakati huo dhiki nyingi sana zitaondoka, watu wataishi muda mrefu sana, biblia inasema mtu atakayekufa na miaka mia ataitwa mtoto mchanga,(Isaya 65:20) wanyama hawatakuwa wakali tena, , hakutakuwa na laana ya nchi kutoa miiba, wala kuzaa kwa uchungu. Hichi ni kipindi ambacho dunia itakuwa salama na tulivu sana. Ni wakati wa Raha ambao Yesu amewaandalia watumishi wake.

Lakini wapo baaadhi watakufa (lakini sio sisi tutakaonyakuliwa), kwasababu shetani alikuwa bado hajahukumiwa amefungwa tu, hicho ndio kipindi ambacho Kristo atakwenda kutokomoza mauti ya mwili, hivyo shetani atafunguliwa kwa muda, ajaribu kuwaangusha watakatifu, atashindwa na kutupwa kwenye ziwa la moto pamoja na watu wote waovu (Ufunuo 20:7-10). Hapo ndipo mwisho wa yote, hakuna tena mauti, wala kifo, wala uchungu, wala huzuni,. Yesu atayakamilisha yote, ambapo adui wa mwisho ndio huyo mauti ya mwili.

Ufunuo 21:1  Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2  Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3  Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4  Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

5  Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6  Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure

Wakati huo ndio Kristo atakuwa ameikamilisha kazi yake yote, na kumrudishia Baba ufalme wote, kama ilivyokuwa kule mwanzo, ili tumwabudu Mungu, sio  katika kukombolewa, au kuchungwa, au katika kuongozwa tena, katika ile mbingu mpya na nchi mpya, Huduma ya Kristo itakuwa imeisha.

Yatakuwa makao yetu milele. Mambo ambayo tumeandaliwa huko ndugu, jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia. Unasubiri nini leo usimpe Bwana maisha yako? Kumbuka tunaishi katika nyakati ambazo Kristo amekaribia sana kurudi. Moja ya hizi siku parapanda italia, tutakwenda mbinguni. Tubu dhambi zako, mwamini Yesu, upokee uzima wa milele.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000

SIFA SITA (6), ZINAZOIKAMILISHA ILE SIKU YA BWANA ITISHAYO.

ILI TUONEKANE WAKAMILIFU MBELE ZA MUNGU.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments