Tafsiri ya Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

Tafsiri ya Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

14 Nami nitaonekana kwenu, asema Bwana, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema Bwana; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka

Huu ni utabiri ambao Mungu aliwaambia Israeli, pindi tu walipochukuliwa utumwani Babeli, akiwaahidia atawarudisha tena kwenye nchi yao baada ya miaka sabini. Na zaidi ya hayo akawapa pia na Neno la ahadi kwamba wakati huo wakimtafuta kwa mioyo yao yote, watamwona, watamwomba atawasikia, na wote watarejeshwa nyumbani ijapokuwa walichukuliwa mbali sana.

Na kweli utabiri huo ulikuja kutumia, kwani mwishoni mwa hiyo miaka sabini, mbiu ilipigwa waisraeli wote warudishwe kwao. Na aliwaonekania sana pindi waliporejea.

Ni neno la ahadi hata kwetu,

Kwamba tukimtafuta yeye kwa mioyo yetu yote, tutamwona. Kumbuka anasema “MIOYO YETU YOTE”. Kosa linatokea pale tunapompenda Mungu kwa sehemu, leo kwake kesho kwa shetani. Ndio Inayopelekea tusimwone Mungu katika ukamilifu wake wote. Mungu anahitaji vyako vyote vielekee kwake, ndipo tumwombe na kumwita ili atuitikie..

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

Nini Maana ya Adamu?

FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ezra ndambuki / from Kenya
Ezra ndambuki / from Kenya
1 month ago

Amina mtumishi
Kweli Sisi kama wakristo hatufai kusubukasubuka na mambo ya kiulimwengu, maana tayari tunao ufalme mambengani mwetu,ni bidii letu kukaza mwendo katika safari yetu,huku tukiwashauri na wengine kuhusu wokovu ulio ndani ya BWANA WETU YESU KRISTO,wapate kuuendea shalom

Last edited 1 month ago by Ezra ndambuki / from Kenya