Jibu: Awali turejee mistari hiyo..
Isaya 7:17 “Bwana ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru.
18 Tena itakuwa katika siku hiyo Bwana atampigia kelele INZI ALIYE KATIKA PANDE ZA MWISHO ZA MITO YA MISRI, na NYUKI ALIYE KATIKA NCHI YA ASHURU.
19 Nao watakuja na kutulia katika mabonde yaliyo ukiwa, na katika pango za majabali, na juu ya michongoma yote, na juu ya malisho yote.”
Huu ni unabii ambao Mungu alimpa Nabii Isaya ili amweleze Mfalme wa Yuda aliyeitwa Ahazi, endapo akitegemea msaada kutoka kwa Mataifa makubwa na kuacha kumtegemea MUNGU kuwa baadaye yatampata mabaya badala ya mema anayoyatazamia.
Ikumbukwe kuwa Mfalme Ahazi alikumbwa na hofu kubwa baada ya kuona Mataifa mawili (ambayo ni Israeli na Shamu) yamegeuka kinyume naye, yanataka kumpiga na kumtoa katika ufalme..
Na mfalme Ahazi badala ya kumtegemea Mungu, alitaka kwenda kutafuta msaada kutoka kwa mfalme wa Ashuru, na Mungu alimwonya kupitia nabii wake Isaya, kwamba msaada kutoka kwa mataifa ya kigeni hautamsaidia, bali utaleta uharibifu zaidi, Lakini Mfalme Ahazi wa Yuda hakusikia na matokeo yake alikwenda alituma wajumbe kwa Mfalme wa Ashuru, kutaka msaada kwao (soma 2Wafalme 16:7-9)
Ingawa msaada huo ulionekana kama ulileta unafuu kwa Mfalme Ahazi, kwani kweli Mfalme wa Ashuru alikubali kumsaidia na kumwangamiza Mfalme Resini wa Shamu.
Lakini matokeo yake baada ya hapo yalikuwa ni makubwa, kwani Yuda walilazimika kuwa tegemezi kwa Ashuru baada ya hapo, na mfalme Ahazi alilazimika kuonyesha utii kwa mfalme wa Ashuru kwa kufuata taratibu zao za kidini na kisiasa (soma 2Wafalme 16:10-18).
Na Uovu wa ibada za kipagani uliongezeka Yuda mpaka kufikia hatua ya Ahazi kujenga madhabahu ya kipagani mfano wa ile iyokuwepo Dameski, jambo ambalo ni machukizo makubwa kwa MUNGU (rejea 2 Nyakati 28:3).
Katika Isaya 5:8-5, Nabii Isaya aliwaonya kwa Neno la MUNGU kuwa kutegemea Ashuru kungeleta taabu zaidi kwa Yuda badala ya msaada.
Sasa “Inzi walio watokao katika kijito cha Misri” ni nini?, na “Nyuki wa Ashuru”.
Hizi ni lugha zinazowakilisha “uharibifu na magonjwa”
Moja ya kitu kilichoiharibu Misri wakati Farao anapigwa na Bwana ni pamoja na wale Inzi, katika ..
Kutoka 8:24 “Bwana akafanya; wakaja wingi wa mainzi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa kwa ajili ya wale mainzi”.
Kama vile Inzi walivyoiharibu Misri, (kwa zile kero) vile vile Bwana ataleta kero kubwa kwa watu wa Yuda..
Hali kadhalika Nyuki ni wadudu waumao na wanaofukuza, (Kumbukumbu 1:44) ambao ghasia zake ni zaidi ya zile za nzi, na hapo Bwana anawaonyesha kuwa watafukuzwa kwa maumivu kutoka katika nchi yao..
Mambo hayo yalikuja kutokeo huko mbeleni kama yalivyo, Kwani maovu ya Yuda yalipozidi alikuja Nebukadreza mfalme wa Babeli na kuwaondoa katika nchi yao, kwa maumivu makali kama ya nyuki.
Funzo kuu tulipatalo kutoka katika habari hii, ni kumtegemea MUNGU na si wanadamu, Mfalme Ahazi alimwacha MUNGU wa Israeli na kuwategemea wanadamu, ikawa laana kwake na kwa watu wa YUDA wote.
Bwana atusaidie tumtegemee yeye peke yake wala tusirudi nyuma.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author