VUNJA MADHABAHU, ANGUSHA NGUZO, KATA ASHERA NA CHOMA SANAMU.

VUNJA MADHABAHU, ANGUSHA NGUZO, KATA ASHERA NA CHOMA SANAMU.

Haya ni mambo manne yanayopalilia matatizo kuanzia ngazi ya kifamilia mpaka ya kitaifa!. (Madhabahu, Nguzo, Ashera na Sanamu).


Kumbukumbu 7:5-6 “Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.

6 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi”

Labda utauliza mambo haya ni mambo gani kwa undani wake na yanaathiri vipi maisha.

   1. Madhabahu:

Madhabahu ni mahali popote panapotolewa dhabihu (sadaka).

Sadaka ina nguvu, ndio maana hakuna mganga anayetoa huduma bila sadaka,

Sasa si kwamba sadaka anahitaji tu  kwaajili ya mahitaji yake..La! bali anajua uchawi wake hautafanya kazi ipasavyo pasipo sadaka, kwahiyo madhabahu ni mahali mahususi kwa sadaka..

Katika biblia BWANA MUNGU aliwaagiza wana wa Israeli wazivunje madhabahu za wakaanani..

Na zilikuwa ni nyingi na za aina tofauti tofauti…na pasipo kuchagua waliambiwa wazivunje zotewasibakishe hata moja, kwani zitakuwa ni chanzo cha matatizo..

Ikimaanisha kuwa madhabu za mashetani ni za kuvunja si za kuziacha, kwani zinapeleka harufu mbaya mbele za MUNGU, na hivyo kuleta matatizo mengi…

Ikiwa kuna mahali ipo madhabahu wanapotolea sadaka karibu nawe, na hiyo madhabahu inakuhusu kwa namna moja au nyingine (kimila), ivunje bila kuogopa!..kama alivyofanya Gideoni, usiiache kwani yaweza kukuletea matatizo.

     2. NGUZO

Nguzo ni miimo ya Mahekalu ya ibada, yaweza kuwa Hekalu la MUNGU (soma 1Wafalme 7:21 na Mwanzo 28:22),  au yaweza kuwa hekalu la mashetani (Soma 2Wafalme 10:26-27).

Maana yake mahali popote penye msingi wa hekalu la miungu ni lazima pabomoshwe.

   3. ASHERA.

Ashera ni miti na maua yaliyokuwa yanazunguka mahekalu ya miungu, ambapo mimea hiyo iliaminika na kuabudiwa kama sehemu ya miungu.

Bwana aliwaambia wana wa Israeli wakate-kate maashera yote lisibaki hata moja (Kutoka 32:12-14).

Hali kadhalika yapo maashera hata sasa, utakuta upo mti fulani unaaminika kama ni wa kiungu na watu wanaenda kufanya matambiko hapo (hiyo ni ashera), ni ya kukata, wengine si miti bali maua tu…

Ondoa maashera katika nyumba yako, ondoa katika nyua yako na uzio wako kwani yaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi.

   4. SANAMU.

Sanamu ni kitu chenye umbile la mtu kinachowekwa katika mahekalu na kuabudiwa.

Hizi nazo Bwana aliagiza zichomwe moto,

Sasa swali linakuja, vipi kama Madhabahu hizi, na ashera, na nguzo na sanamu zipo mbali?.

Kama zipo mbali na upeo wa kuzifikia, tunazo silaha zinazosafiri masafa marefu zaidi ya silaha zote zilizowahi kutengenezwa na mwanadamu au zitakazokuja kutengenezwa.

Silaha hiyo ni Maombi.

Maana yake katika maombi Unazivunja madhabahu kwa Imani, unaangusha Nguzo kwa imani, unakata maashera kwa imani, na unazichoma moto hizo sanamu kwa imani kupitia jina la YESU.

Na kwa jinsi utakavyotamka, zitateketea kule zilipo kwa namna hiyo hiyo, lakini usiingie kwenye maombi ya vita kama wewe si askari mwenye silaha hizi za Waefeso 6:10-15.(utajitafutia matatizo zaidi).

Pia usiache kuzibomoa kwa mikono yako kama zipo mbele ya upeo wa macho yako. (Upo unaziona sio tu kuombea, bali kuzimoa kwa mikono kabisa).

Ukifanya hivyo utakuwa umeusafisha uwanda, hakuna laana juu ya mahali ulipo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments