SWALI: Nini maana ya Mithali 3:27 ?
[27]Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
JIBU: Kuna mambo mawili yaliyogusiwa katika hicho kifungu..
Hili ni agizo la Bwana kuwasaidia wengine. Lakini pia Bwana anataka tujue ni akina nani wenye haki hiyo ya kusaidiwa.
Kibiblia Makundi ambayo ni haki yao kusaidiwa.(wawapo na shida), ni matatu (3)
i) Familia (yaani ndugu wa mwilini)
1 Timotheo 5:8
[8]Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Wazazi wako, wadogo zako, watoto wako. Ni haki yao kuwasaidia, kwasababu ni damu moja na wewe. Usipotimiza wajibu huo unahesabika sawa na mtu aliyeikana imani. Hakikisha jicho lako haliwapiti ndugu zako, ni sehemu ya wajibu.
ii) Ndugu wa rohoni:
Wagalatia 6:10
[10]Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Kanisa la kwanza lilitambua jukumu hili la kusaidiana, vivyo hivyo na sisi ikiwa mpendwa mwenzako yupo katika hali na uhitaji mkubwa hupaswi kufumba macho, bali msaidie, watumishi wa Mungu wanaojibidiisha kuhubiri kweli ya Mungu wanastahili kusaidiwa mahitaji yao. (Warumi Romans 12:13, Hebrews 13:16).
1Yohana 3:17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Hapa inalenga pia na wajane pia walio ndani ya kanisa wale walio wajane kwelikweli. (1Timotheo 5:3–5, 9–10)
iii) Maskini.
Wapo maskini wengi ulimwenguni, ambao wanashindwa kufikiwa na mahitaji yao ya msingi, wengine wanakuwa mabarabarani walemavu, wagonjwa, majirani maskini, wote hawa pia wanastahili kusaidiwa.
Wagalatia 2:10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.
Hayo ndio makundi yenye haki ya kusaidiwa. Lakini wengine wanaweza kusaidiwa lakini sio haki yao,ikiwa na maana hata wasiposaidiwa hakuna shitaka lolote juu yako kwa Mungu.
Lakini Ukiendelea kusoma anagusia tena jambo la pili ambalo ni; “Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda”.
Akiwa na maana gani?
Mtume Paulo kwa uweza wa Roho aliandika maneno haya;
2 Wakorintho 8:12-13
[12]Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo. [13]Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
Yaani kwa jinsi moyo wako unavyoguswa, tenda mema, lakini pia kulingana na uwezo wako uliokirimiwa na Mungu, ili upande mmoja usiuache na taabu au kupungukiwa kabisa. Kwamfano umepata rizki kipimo cha watoto wako tu, ukaenda kukichukua na kuwapa maskini huku familia yako ikabaki Kulala njaa.. hapo hujafanya busara kwasababu umehamisha Tatizo sehemu moja kupeleka kwingine, hujatatua tatizo.
Tenda mema, bila kusahau pia kipimo chako ulichopimiwa cha mema.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Masomo mengine:
Elewa tafsiri ya Mithali 27:22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni.
Elewa maana ya Mithali 18:23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.
Nini maana ya Mithali 24:11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe?
About the author