Siku moja nilikuwa nakatiza eneo fulani la biashara ambalo limechangamka sana, Ni e neo ambalo watu wengi wanapishana..ghafla kwa mbele nikamwona kijana mmoja ameinama, baada ya muda kidogo akachuchumaa, na mara akaanza kutapika matapishi mengi sana.. Uso wake ulionekana kuumwa, hivyo moja kwa moja nilipomwangalia moyoni mwangu, niliguswa sana na ile hali aliyokuwa anapitia..
Kikawaida zipo hali ambazo ukiumwa Unaweza kuzivumilika mpaka ufike mahali fulani pa matibabu..lakini kuumwa mpaka kutapika Hakuzuiliki, na kama ulishawahi kutapika unaelewa nguvu inayotumika, hali unayouisikia wakati huo.. ni kama nusu ya kufa..
Sasa sisi ndivyo tunavyomfanya Mungu, ajisikie muda wote tunapokuwa Na aina ya mwenendo wa uvuguvugu maishani mwetu, .alisema hivi;
Ufunuo wa Yohana 3:15-19
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. [16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. [17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. [18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. [19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
[19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Uvuguvugu ni ile hali ya kuwa mtu wa kidini na sio wa kiroho, unahudhuria ibada lakini mabadiliko huna, unavaa vizuri kanisa lakini ukiwa nje unavaa nguo zisizo na adabu, unaimba kwaya, lakini wakati huo huo unasikiliza nyimbo za kidunia, ni mtumishi mzuri wa kanisani lakini bado unaishi na mume wa mtu..
Maisha ya uvuguvu, yanamtesa Kristo isivyo kawaida..Ikiwa wewe hupendi kutapika- tapika Kwanini wewe umfanye Mungu kuwa na hali hiyo?
Ukristo ni mwendelezo sio tukio…eti mimi nimeshamkiri Yesu kwa Kinywa..inatosha nimeokoka, hapana…bali ni ukuaji wa kiroho.. ni lazima uonyeshe ukuaji…kitu chochote kilicho hai kinakua…lakini kuwa mtu yule yule kila siku wewe ni vuguvvugu.
Kanisa La Laodikia, lilikuwa na sifa ya kujiona ni tajiri Kisa Lina vyombo vizuri vya miziki, lina Makongamano makubwa ya nje, lina mwonekano wa kuvutia, lina umaarufu, Lakini Yesu aliliona si la kiroho hata kidogo..Linamheshimu Mungu kwa nje tu, lakini ndani limepoa zaidi ya barafu..
Hizi ni nyakati ambazo watu wengi wanazisahau ibada za kweli, wanatafuta fedha na Midundo inayovutia masikio ya watu lakini hawajali ujumbe wa rohoni au ‘uzuri Wa utakatifu’.
Na watu ambao wakiwaona wengine wamesimama kikamilifu mbele za Mungu wanawaita “walokole” …
Embu tubu, rafiki…uzuri wako, mwonekano wako, Sifa zako, udunia wako, havina ushirika na Kristo, hizo status zisizo na staha na elimu, unampostia nani mitandaoni? Hiyo mitandao ya kizinzi unayoitembelea kila siku, na kujichua unakoendelea nako kwa siri na wakati huo huo unasema umeokoka, nini unakiunda kama sio kumfanya Bwana atapike?…maanisha kumpokea Kristo. Simama katika imani, ili umwone Mungu wa kweli na sio sanamu.
Kumbuka hizi ni nyakati za kusimama kikamilifu, kwasababu mwisho umekaribia..Unyakuo Ukipita watakaokwenda na Bwana ni walio moto tu, na sio vuguvugu.
Kutubu ni kugeuka…Geuka tu leo kwa kumaanisha na Bwana atakusamehe kabisa na kuanza na wewe..Ikiwa hujaokoka na upo tayari leo kufanya hivyo…Basi wasiliana nasi kwa mwongozo sala sala ya Toba..
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NAYAJUA MATENDO YAKO.
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
Nini maana ya kumwabudu Bwana katika uzuri wa utakatifu?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ