Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)

Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)

Jibu: Turejee kuanzia ule mstari wa 11..

Luka 1:11 “Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.

12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.

13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.

14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.

15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.

16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.

17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, NA KUWATILIA WAASI AKILI ZA WENYE HAKI, NA KUMWEKEA BWANA TAYARI WATU WALIOTENGENEZWA”.

Haya ni maneno ya Malaikaa aliyokuwa anamwambia mzee Zakaria kuhusu mtoto atakayezaliwa (ambaye ni Yohana Mbatizaji), kwamba mtoto huyo atajazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni, na atatembea na roho (yaani huduma) ya Eliya, lakini pia atawatejeza wengi wa Mungu, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa, na zaidi sana KUWATILIA WAASI AKILI ZA WENYE HAKI!

Sasa kabla ya kutazama ni kwa namna gani Yohana Mbatizaji “aliwatilia waasi akili za wenye haki” hebu kwanza tutazame alimwekeaje Bwana tayari watu waliotengenezwa..

Ikumbukwe kuwa baadhi ya wanafunzi wa Bwana YESU kabla ya kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu walikuwa kwanza wanafunzi wa Yohana mbatizaji.. baadhi ya hao walikuwa ni Andrea na nduguye Petro (Soma Yohana 1:35-41).

Kwahiyo akina Andrea na wengine ni watu waliotengenezwa kiroho kabla ya kuanza kutembea na Bwana, hivyo kwao haikuwa ngumu kumwamini Bwana au kumwelewa.. (hiyo ndio maana ya kumwekea tayari Bwana watu waliotengenezwa)

Sasa terejee sehemu ya Pili ambayo ni “Kuwatilia waasi akili za wenye Haki

Hapa kuna mambo mawili, 1. Waasi, 2.Akili za wenye haki.

Waasi wanaozungumziwa hapo ni Wana wa Israeli ambao wameiasi sheria ya MUNGU na kumwacha Mungu (Soma 2Nyakati 29:6), Na anaposema “akili za wenye haki”.. maana yake zipo “akili za wasio haki” maana yake akili za watu wasiomjua MUNGU, Lakini akili za watu wanaomjua MUNGU/wenye haki ni zile zinazomfanya Mtu amwangalie Muumba wake katika jicho la usafi na utakatifu, ndio zile alizowaambia katika Luka 3:8-14..

Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?

8 Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.

9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

10 Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi?

11 Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo.

12 Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi?

13 Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa.

14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu”.

Akili za wasio haki, zinafundisha DINI tu, kwamba wao ni wayahudi wanaye Baba ambaye ni Ibrahimu, kwahiyo ni uzao mteule, lakini akili za wenye haki zinafundisha kwamba pamoja na kwamba wanaye Baba ambaye ni Ibrahimu bado wanapaswa kujitakasa maisha yao ili wakubaliwe na MUNGU, kuwa tu mwana wa Ibrahimu haitoshi, inahitaji matendo yanayoendana na hiyo Imani.

Hivyo wengi walipojua hilo walitubu na kumrudia Mungu kwa matendo yao.

Hali kadhalika hata leo tunahitaji hizi akili za wenye haki.. hatuwezi kusema sisi ni wakristo wenye madhehebu makubwa, na majina mazuri ya kibiblia halafu matendo yetu hayaendani na asili ya imani yetu, ni lazima tupate akili za wenye haki.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je kuna Yohana wangapi katika biblia?

Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?

YOHANA MBATIZAJI

Nini maana ya “SAA INAKUJA” na “SASA IPO” (Yohana 4:23).

MGAWANYIKO WA ISHARA ZA UJIO WA BWANA YESU KRISTO.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply