KUMBUKA NI AMRI MPYA!

KUMBUKA NI AMRI MPYA!

Yohana 13:34

[34]Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. 

Hapo mwanzo nilipokuwa nautafakari huu mstari, nilijiuliza maswali Yesu anaposema “AMRI MPYA..

Ni amri ipi hiyo mpya?

Maana ukitafakari anasema “mpendane” kwani kupendana ni amri mpya?

Mbona ilikuwepo tangu zamani? Na ilijulikana

Mambo ya Walawi 19:18

[18]Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA. 

Kupendana kulifundishwa tangu zamani za torati…lakini mpaka Kristo anasema amri mpya maana yake kupendana anakokusema yeye ni tofauti na kule kulivyodhaniwa…

“Ndio maana akasema…Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.”

Yaani mpendane kwa mfano wa upendo wangu, sio mfano wa upendo mwingine.

Je upendo wa Yesu ulikuwa upi?

Upendo wa upeo.

Yohana 13:1

[1]Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. 

Upeo ni ukomo wa mwisho kabisa…Yesu hakutupenda kwa wakati fulani tu…bali alitupenda (sisi tuliomwamini) mpaka mwisho, kabisa kutoka moyoni..

Ikiwa na maana alipiga gharama ikitokea huyu amenisaliti, Amenikana, amenizunguka…je nitakoma kumpenda?…hivyo akaamua kukubaliana na yote…liwalo na liwe nimempenda, na nitampenda mpaka mwisho..

Ndio maana ijapokuwa alijua Yuda atamsaliti, na Petro atamkana, hakuacha kuwapenda…sasa huo ndio upendo wa Kristo mpya..upendo wa upeo

Leo ni rahisi kupenda mtu kwa mema, au mazuri anayoyadhihirisha sasa…lakini ikitokea baadaye yule uliyemsaidia anakusaliti, uliyemhudumia anakudharau, uliyemsomesha hatimaye amekuwa na cheo kikubwa kuliko wewe sasa anakucheka,..hapo hapo unaanza kuumizwa, hata kumchukia, na kumlalamikia…sasa huo sio upendo wa upeo….ni upendo wa nyakati…lakini ikiwa anakutendea mambo yote hayo halafu hujali hapo ndio upendo ule mpya wa Kristo anapodhihirika.

Bwana anataka tupige gharama ya kuanzia mwanzo hadi mwisho…ukiamua kumpenda mtu..basi mpende daima. Bila sharti.

Upendo mpya.. ni ule wa kupenda wanaokuchukia, ule wa zamani ulikuwa mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye.(Mathayo 5:43-44).. kilele cha upendo huu mpya ni kuwa tayari kugharimika lolote kwa ajili ya wengine..(Yohana 15:13)

Je amri hii mpya tunayo?

2 Yohana 1:5

Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane. 

Bwana awe nawe.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.

JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.

JE UPENDO WAKO UMEPOA?

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply