Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, na leo tutajifunza umuhimu wa kuongeza nguvu za rohoni.
Biblia inasema…
Mithali 24:10 “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache”.
Kuzimia kunakozungumziwa hapo ni ile hali ya kuzidiwa mpaka kufikia hatua ya kukata tamaa kabisa.
Kwa asili watu tuliompokea YESU hatujakusudiwa kuzimia wakati wa tabu.
Kwani tabu ni kama upepo kwa tiara, tiara inapokabiliana na upepo ndivyo inavyoruka juu zaidi.
Kama umeokoka na unaona dalili ya kuzimia au kukata tamaa au kuanguka kabisa unapokutana na tabu, ni ishara tosha kuwa nguvu zako za kiroho zipo chini.
Lakini kama changamoto na tabu kwako si kitu, na wala hazikuyumbishi..bali unasimama na kuendelea mbele kwa ushindi basi wewe nguvu zako za rohoni ni kubwa, shika sana ulicho nacho.
Sasa ikiwa umejigundua kuwa nguvu zako za rohoni ni chache, nataka nikuambie kuwa inawezekana leo hii kuzipandisha, ikiwa utakubali kufanya mambo macheche yafuatayo..
Lakini kabla ya kuyatazama mambo hayo naomba kwanza tusome andiko lifuatalo..
Isaya 40:29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo”.
Kama huna nguvu ya kusimama, bali umechoka na unakaribia kuzimia kutokana na hali unazozipitia, hili ni neno lako.
Hapo ulipo piga magoti, omba toba ya kumaanisha kabisa, kisha dhamiria kutafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU (Matendo 2:38), hapo Roho Mtakatifu atakuja juu yako, na kukuongezea nguvu katika nyakati zote na vipindi vyote.
Pia zingatia kuwa na vipindi vya maombi binafsi kila siku, na vipindi vya maombi ya mkesha.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ