SWALI: Ni sahihi kwa Mkristo mtakatifu kumwambia BWANA ailaze roho ya mtu aliyekufa mahali pema PEPONI?
JIBU: Sio sahihi, kwasababu ameshakufa. Tumepewa amri ya kuombeana sisi kwa sisi, yaani tunapokuwa tunaishi hapa duniani, baada ya kufa hatujapewa amri ya kuombeana. Hakuna maombi yoyote yanayoweza kubadilisha hatima ya mtu aliyekufa, kilichobakia kwa mtu aliyekufa ni hukumu tu! (Waebrania 9:27).
Mazishi ya watu wasioamini ni tofauti na mazishi ya watu waliomwamini BWANA wetu Yesu Kristo, wasiomwamini wao hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na mambo yatakayofuata baada ya kifo, ndio maana wanasema maneno hayo, lakini sisi tulioamini ndio tunaoelewa kwamba kama ndugu yetu amekufa katika Bwana, basi tunalo tumaini la kukufuka tena kwasababu ni kama amelala tu!.. Lakini kama mtu amekufa katika dhambi na hakumpokea Kristo basi huyo hana tumaini la uzima wa milele, hivyo hawezi kuokolewa kwa maombi yoyote yale. Kwasababu Bwana Yesu alitupa maagizo ya kuenenda ulimwenguni kote kuihubiri injili, AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA, hakutupa agizo la kuenenda ulimwenguni kote kuwaombea wafu waokoke au walazwe mahali pema peponi.
Kwahiyo saa ya wokovu ni sasa katika maisha haya, baada ya maisha haya ni hukumu.
Ubarikiwe.
Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312
Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
Mada zinazoendana:
WALE WATAKATIFU WALIOFUFUKA NA BWANA YESU KWAO JE! WALIKUWA PEPONI AU WAPI?
KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KUWEKA MSALABA MAKABURINI?
JE! NI SAHIHI KUWAOMBEA WAFU?
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO?
KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.
Rudi Nyumbani:
Print this post