Katika 1Yohana 5:6-9, (a) Ni kwa namna gani Yesu alikuja kwa maji na damu?

Katika 1Yohana 5:6-9, (a) Ni kwa namna gani Yesu alikuja kwa maji na damu?

Kadhalika naomba kufahamu.. (b)Mashahidi watatu washuhudiao mbinguni wanatajwa, Neno ambaye ndiye Yesu bado ana nafasi ya mwana hata baada ya kutoka duniani? (c)mashahidi wa duniani (roho,maji na damu) wanaotajwa ni kwa namna gani wanashuhudia? BARIKIWA SANA !


JIBU: A) Kwanza ni muhimu kufahamu wakati, Bwana Yesu alipokuwa pale Kalvari, baada ya kuchomwa mkuki ubavuni na yule Askari wa Kirumi, kulitoka MAJI NA DAMU, ikiashiria kuwa dhambi zetu, zinaoshwa kwa damu na kwa njia ya maji. Ikiwa na maana kuwa mtu ili apate ondoleo la dhambi zake ni lazima akabatizwe kwanza kwa kuzamishwa katika MAJI mengi kama ishara, na ndipo dhambi zake ziweze kusafishika kwa DAMU ya Yesu Kristo. Na ndio maana Bwana alisema aaminiye na kubatizwa ataokoka…  

B) Na aliposema wapo watatu washuhudiao mbinguni na wapo watatu washuhudiao duniani, haikumaanisha kuwa kuna nafsi tatu za watu duniani na kuna nafsi tatu nyingine mbinguni. Hapana haimaanishi hivyo kwasababu maji yatashuhudiaje? Hayawezi kuongea wala kuhubiri injili, hivyo anaposema wapo watatu duniani yaani maji, damu na Roho anamaanisha zipo hatua tatu “mwanadamu kuzifuata ili kukamilika duniani” yaani mtu anapaswa aoshwe dhambi zake kwa kubatizwa katika MAJI, ili apate ondoleo la dhambi zake kwa DAMU ya Yesu na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye ndiye muhuri wa Mungu.Hatua hizi tatu ndizo zinazoshuhudia kwamba mwanadamu akizifuata hizo amekombolewa na kukamilishwa.  

Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”  

C) Na aliposema wapo watatu mbinguni hakumaanisha tena kuna nafsi tatu mbinguni kila moja inajitegemea, hapana! Biblia ilimaanisha kuwa zipo hatua tatu mbinguni MUNGU MMOJA alizozitumia “kumpatanisha mwanadamu na nafsi yake ”, hatua ya kwanza alizungumza na wanadamu kama Baba(yaani MUNGU JUU YETU), hatua ya Pili alizungumza nasi kama NENO(MUNGU PAMOJA NASI,EMANUELI,)

Waebr 1:1“Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika MWANA, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.”

Hatua ya tatu kazungumza nasi kama ROHO MTAKATIFU(MUNGU NDANI YETU), katika Roho Mtakatifu ndio utimilifu wa Mungu kuzungumza katika ukaribu zaidi, yeye ndiye atufundishaye mioyoni mwetu na kututia katika kweli yote,  

Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 WALA HAWATAMFUNDISHA KILA MTU JIRANI YAKE, NA KILA MTU NDUGU YAKE, WAKISEMA, MJUE BWANA; KWA MAANA WATANIJUA WOTE, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.  

Kwahiyo kwa hatua hizi tatu mwanadamu amepatanishwa na kusogezwa karibu zaidi na Mungu….Tofauti na zile za kwanza(maji,damu, na Roho) ambazo ni mwanadamu anapaswa azifuate kukamilika mbele za Mungu, lakini hizi za mwisho(Baba, Neno na Roho) ni Mungu anazitumia kutupatanisha sisi na nafsi yake (au kutusogeza karibu zaidi na yeye)..  

Ubarikiwe sana.  


Mada zinazoendana:

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

BIDII YA MFALME YOSIA.

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Katika sehemu ambayo mmefeli ni apa ombeni roho mtakatifu awasaidie kufahamu juu ya andiko hili 1yohane 5