SAYUNI ni nini?

SAYUNI ni nini?

JIBU: Tukirudi Mwanzo kabisa Daudi alipoenda kuiteka Yerusalemu,na kufanikiwa eneo lile liliitwa ngome ya SAYUNI (2Samweli 5:7).Hivyo Sayuni kwenye biblia imetumika kama Mji wa Daudi au Mji wa Mungu (YERUSALEMU).. 

Kadhalika na lile eneo la mlima ambalo hekalu la Mungu lilijengwa liliitwa pia mlima Sayuni, ambalo lipo hapo hapo Yerusalemu (Yeremia 31:6,12). 

Sehemu nyingine biblia imetaja Sayuni kama watu wa Mungu yaani wayahudi;

 Isaya 60: 14 “Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako [Israeli] na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli” 

Unaweza kuona hapo. Kadhalika ukisoma pia (Zakaria 9:9, Sefania 3:14-19),biblia inamtaja Israeli kama binti Sayuni. Yote haya yanaonyesha pia Wayuhudi mbele za Mungu ni sawa na SAYUNI yake. Lakini tukirudi katika agano jipya neno Sayuni limezungumziwa kama ufalme wa watu wa Mungu wa rohoni. 

Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,” 

Hapo Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho anaonyeshwa Sayuni hasaa ambayo Mungu aliikusudia kwa watu wake tangu zamani yaani hiyo Yerusalemu ya mbinguni kanisa la Mungu. Mtume Petro pia aliandika katika…

 1Petro 2: 6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.”

 Habari hiyo nayo inathibitisha kuwa kanisa ndiyo Sayuni ya Mungu na ndio pia Yerusalemu ya mbinguni,..na tunafahamu Kanisa msingi wake ni Yesu Kristo, na hapo hiyo Sayuni jiwe kuu lake la pembeni linaonekana nI YESU KRISTO BWANA WETU. Kwahiyo na sisi pia tujitahidi tuwe na sehemu katika hiyo SAYUNI/ YERUSALEMU mpya ya Mungu ambayo Mungu alishaanza kuiandaa na anaendelea kuiandaa hapa hapa duniani. 

Ubarikiwe.

MLIMA WA BWANA.

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

Rudi nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments