SWALI: Shalom!
Luka 23:27 “Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata,na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua vyao na kumwombolezea.Yesu akawageukia,akasema,Enyi binti za Yerus’alemu,msinililie mimi,bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.29″KWA MAANA TAZAMA SIKU ZINAKUJA mtakaposema,HERI WALIOTASA,na MATUMBO YASIYOZAA,na MAZIWA YASIYONYONYESHA. Naomba kufahamu Siku hizo Kwanini hao walisema “Heri waliotasa..heri matumbo yasiyozaa..heri maziwa yasiyonyonyesha??
JIBU: Shalom! Hayo maneno a Bwana Yesu aliyazungumza kabla ya kupandishwa msalabani, Tunaona wale wanawake waliokuwa wanamfuata walimwonea huruma sana na kusikia uchungu mkubwa kwa mateso aliyokuwa anayapitia…lakini Bwana Yesu akawaambia msinililie mimi bali jililieni ninyi nafsi zenu na watoto wenu.. Kwanini alisema vile…
Kwasababu aliona kipindi kifupi sana kinachokuja mbeleni…kwamba mambo yaliyompata yeye yatakwenda kuwapata na wao pia, pamoja na watoto wao tena makubwa zaidi ya hayo…ambapo na wao pia watakatwa katwa na wanawake watachichwa kama kuku. Na kama unafuatilia unabii vizuri wa Biblia utakuja kuona kuwa kipindi kifupi tu baadaye AD 70 (yaani miaka 37 baada ya kusulibiwa kwa Bwana)..Jeshi la Rumi lilikuja na kuuzingira mji wa Yerusalemu na kuuchoma moto na kuwaaua watu wengi sana wakiwemo wanawake na watoto …historia inasema zaidi ya watu milioni moja na laki moja waliuawa…Mpaka ikaonekana kuwa ni heri mwanamke aliyetasa ambaye hakuzaa mtoto kuliko Yule aliyezaa na kuona mtoto wake anachichwa kama kuku mbele yake,Yerusalemu kulikuwa na maombolezo makubwa sana, hiyo ni kutimiza unabii alioutoa Bwana juu ya Mji huo katika..
Luka 19: 41 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako”.
Mathayo 23.37 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! 38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa”.
Unaona hapo? Sababu ya Mji kuharibiwa na kufanywa ukiwa?..Ni kwasababu hawakujua saa ya kujiliwa kwao, ni kwasababu Masihi alikuja kwao na wao wakamkataa wakasema anapepo, anakufuru n.k hawakujua kuwa yeye ni mwokozi na ndiye aliyeteuliwa na MUNGU kuwa ukombozi kwa mwanadamu…Na kwasababu hiyo, Bwana akawaambia ule ulinzi na amani vimeondoka kwao siku zinakuja siku watakapoteketezwa na kuangamizwa na kutolewa kutoka katika nchi yao..Ndio maana Bwana akawaambia msinililie mimi, bali jililieni nyinyi na watoto wenu..kwasababu yatakayokuja kutokea mbeleni ni makubwa kuliko haya yangu.
Hiyo ilikuwa ni dhiki au adhabu kwa wayahudi (yaani waisraeli) kwa kumkataa Masihi, na kadhalika itakuja dhiki nyingine iliyo kubwa na isiyo na mfano kwa watu wa dunia nzima, kwa wale wote ambao wanamkataa Kristo sasa na kumsulibisha katika akili zao..Dhiki hiyo itakuwa ni kubwa isiyokuwa na mfano kuliko hiyo iliyowapata wayahudi..Biblia inaeleza hivyo. Kwahiyo tukiyajua hayo, sio wakati wa kuchezea hatima yetu ya milele, kabla dhiki kuu haijamiminwa duniani tunapaswa wakati huo tuwe tumekwenda na Bwana katika unyakuo. Je! Na wewe una uhakika utakuwepo miongoni mwao watakaomlaki Bwana mawinguni?
Bwana akubariki.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NGURUMO SABA
JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.
WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.
TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?
About the author