Nuhu alipataje ujuzi wa kuwatambua wanyama wale wote na kuwaweka ndani ya Safina?

Nuhu alipataje ujuzi wa kuwatambua wanyama wale wote na kuwaweka ndani ya Safina?

SWALI: Shalom!.Ndugu zangu Biblia inatuambia kuhusu kazi yakutoa jasho aliyopewa Nuhu ya”KUVIINGIZA KATIKA SAFINA”VIUMBE VIRUKAVYO-Vya kiume na vyakike kwa jinsi yake” “KILA NAMNA YA WANYAMA-Wakiume na Wakike kwa jinsi yake” .

Swali Ni je! Nuhu Alipata wapi ujuzi huo wa kuvitambua hivyo viumbe vyote, na je! Hao wanyama wote aliwatolea wapi?

  JIBU: Ukisoma mstari wa 20 sura ya 6 wa kitabu kile cha Mwanzo Biblia inasema : 20 Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI.   Unaona hapo, hilo neno WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI

Ni kuthibitisha kuwa sio wanyama wote Nuhu alikwenda kuwachunguza kujua jinsia zako au kuwakamata, hapana wengine walikuja wenyewe Mungu ndiye aliyewaleta,isipokuwa wale wa kufungwa, lakini wengi wa hao waliosalia Mungu aliwaleta mwenyewe kwa Nuhu,  kazi ya Nuhu ilikuwa ni kuwaingiza tu ndani.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

JE! VIUMBE VINATAZAMIAJE KWA SHAUKU KUFUNULIWA KWA MWANA WA MUNGU?

JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.

KISASI NI JUU YA BWANA.

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments