Usipokuwa na uelewa wa kutosha juu ya ndoto, unaweza ukajikuta unatoka nje ya kusudi la Mungu ambalo amekukusudia wewe uishi kwalo hapa duniani..
Na hiyo imewafanya watu wengi wazunguke huko na huko, kutafuta tafsiri ya ndoto zao..Lakini jambo la kwanza na la msingi sana kufahamu ni kuwa, tunapaswa kujua kuwa ndoto yoyote ni lazima iwepo katika mojawapo ya makundi haya matatu:
> Kundi la kwanza ni ndoto zinazotokana na Mungu,
> Kundi la Pili ni ndoto zinazotokana na shetani,
> na kundi la tatu ni ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.
Sasa ndoto hizi zinazotokana na mtu mwenyewe huwa zinaathiriwa sana na mambo mbalimbali aidha kutokana na mazingira ya mtu yanayomzunguka au shughuli anazozifanya mara kwa mara, au mambo anayoyawaza kila wakati..Na aina hii ya ndoto ndiyo inayochukua asilimia kubwa sana ya ndoto watu tunazoziota kila siku, naweza kusema hata asilimia 95 ya ndoto tunazoziota kila siku na hizi huwa hazina maana sana, lakini watu kwa kukosa ufahamu imefanya wahangaike kutwa kuchwa kutafuta tafsiri ya kila ndoto yanazoziota mpaka inawafanya kuwa watumwa wa ndoto…Kumbe kiuhalisia sio kila ndoto ina ujumbe wa kutufaa..
Hivyo mtu akishakuwa na uelewa wa namna ya kuzigawanya ndoto hizi katika makundi haya hatapata shida kuitafsiri ndoto yake..Hivyo nakuashuri pitia kwanza somo hili kisha ndio tuendelee. >> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?
Sasa ukiota una mimba: Ikiwa ndoto hiyo haitokani na shughuli zako mwenyewe au mazingira yanayokuzunguka, au mawazo unayoyawaza kila mara, kwasababu kumbuka ndoto kama hizi huwa zinawatokea mara nyingi wanawake, kwahiyo uwezekano wa kuangukia katika kundi hilo la tatu la ndoto ni mkubwa kwasababu wanawake maisha yao tangu wakiwa watoto wanawaza siku moja ni kuwa na mtoto kwahiyo kuota wamebeba mimba si jambo la kushangaza, au utakuta mwingine maisha yake yote anatamani sana kuwa na mtoto, hana watoto, moja kwa moja mtu kama huyo ni rahisi kuota ni mjamzito au mwingine utakuta anaishi na mwanamke mjamzito karibu na mazingira yake au jana amemwona mwanamke mmoja barabarani akipita akiwa mjamzito akajikuta usiku anaota kabeba mimba akadhani kuwa ndoto hiyo inamaana sana kwake..,
Ikiwa ni hivyo, basi zipuuzie tu, ni ndoto zinazokuja kutokana na mawazo yako. Hizo hazibebi ujumbe wowote kwako.
Lakini hapa tunadhania kuwa ndoto hiyo haijatoka katika vyanzo vya namna hiyo,
Sasa fahamu kuwa tendo lolote kuchukua mimba liwe ni jema au liwe ni baya, liwe limekuja kwa njia ya uzinzi au kwa njia ya haki ni lazima tu kiumbe kipya kije duniani mwisho wa siku hakuna namna!..Na kabla hakijaja lazima dalili Fulani zionekane…Hivyo kama ndoto yako imekuwa ni ya kujirudia rudia basi itilie maanani zaidi kwasababu inaweza kuwa imebeba ujumbe kutoka kwa Mungu,..
Utakumbuka Farao alipoota ndoto ile ihusuyo miaka saba na njaa na miaka saba ya neema, ilikuja mara mbili, hata kama ilichukua taswira nyingine lakini ujumbe ulikuwa ni mmoja..ndipo akawa na uhakika wa kuwa ndoto ile ni ya kuizingatia..Vivyo hivyo na wewe ikiwa unaota mara kwa mara una mimba, ni mjamzito izingatie sana ndoto hiyo.
Kwahiyo jambo unalopaswa kufanya hapo kwa kuwa wewe ndiye unayeyafahamu maisha yako zaidi kuliko mtu mwingine yeyote , kaa chini kwa utulivu mwingi utafakari maisha yako na njia yako unayoiendea sasa hivi..iwe ni katika huduma yako, iwe ni katika familia yako, iwe ni katika shughuli yako unayoifanya sasa, kuna uamuzi uliuchua, au kuna jambo ulilifanya ambalo hivi karibuni utakwenda kuona matokeo yake..
Hivyo kama ulimwomba Mungu juu ya kitu Fulani, kwa muda mrefu akupatie basi kaa katika matarijio ya kukipata, au kama ulijitaabisha katika kitu ambacho kwasasa faida yake haionekana kaa katika matarajio ya kukipata muda si mrefu..
Sara alikuwa katika matarajio ya kupata mtoto kwa muda mrefu, lakini wakati ulipofika malaika alimjia na kumwambia panapo wakati kama huu mwakani utalea mtoto..VIvyo hivyo na wewe kama upo katika mstari ulionyooka na Mungu wako basi tarajia Mungu kukupa kile ulichokuwa unakitafuta. Kwasababu mimba sikuzote ni matokeo ya ile mbegu iliyoingia ndani yako..Kama ni mbegu njema uliipanda basi utavuna kilicho chema.
Vile vile kama ulikuwa ni mwovu unafanya mambo yasiyompendeza Mungu nawe pia kaa katika matarajio ya kukipata hicho ulichokuwa unakifanya, ikiwa ulikuwa mchawi jiandae kuvuna matunda ya uchawi wako, ikiwa ulikuwa ni tapeli au mla rushwa jiandae kukumbana na ulichokihangaikia, kama ulikuwa ni mrushi vile vile jiandae kukutana na malipo yake hivi karibuni…
Usishangae kukutana na mabaya, kwasababu biblia inasema dhambi nayo huwa inapitia hatua hizo hizo mpaka kufikia mauti.
Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”
Zaburi 8:14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.”
Isaya 59:3 “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya.
4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.”
Hivyo kama unatenda maovu sasa, acha mara moja, Tubu dhambi zako, umegukie muumba wako YESU KRISTO kabla huo wakati wa mabaya haujafika, lakini kama unajijua upo katika njia iliyonyooka na umekuwa katika dua ya kumwomba Mungu kwa ajili ya kitu Fulani chema..Basi kuwa katika matarajio ya kukipata siku za hivi karibuni.
Ubarikiwe.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
About the author