MATESO YA MWENYE HAKI

MATESO YA MWENYE HAKI

Zaburi 34:19 “Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote”.

Wengi wanauliza inawezekana mwenye haki akapitia mateso?..Jibu ni ndio! Mwenye haki anapitia mateso..

Tunaweza kuchukua mifano kadhaa katika Maandiko, Yusufu alikuwa mwenye haki, alimheshimu Baba yake kuliko kaka zake 11, hakusema uongo kwa Baba yake, na zaidi ya yote alipendwa na Baba yake kutokana na haki yako..Lakini tunasoma alipitia mateso makali…Alinusurika kuuawa na ndugu zake, aliuzwa Utumwani, akawa mtumwa, zaidi akafungwa gerezani akakaa huko sehemu ya mateso kwa miaka mitatu. Lakini kama maandiko yanavyosema Mateso ya mwenye haki ni Mengi lakini Bwana atamponya nayo yote. Hataacha hata moja!!

Tangu akiwa na kijana wa miaka 16 mateso yake ndio yalianza, na yalikuja kupungua akiwa na miaka 30 na kuisha kabisa akiwa na miaka 37…Bwana alimponya nayo yote…

Kadhalika Ayubu, alipotelewa na mali zake zote ndani siku moja, kondoo, Mbuzi, punda, ngamia, Wafanyakazi na zaidi ya yote akafiwa na Wanawe wote na akakaa vile kwa muda mrefu mpaka mkewe akamshauri amkufuru huyo Mungu wake akafe…Lakini Biblia inasema Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana atamponya nayo yote..

Ulipofika wakati wa kuponywa alivipata vyote alivyovipoteza kwa wakati mmoja na mara mbili zaidi.

Ipo mifano Mingi, unaweza ukaenda kuisoma mwenyewe, mifano kama ya akina Hana, Yefta, Daudi, Ruthu, Bathsheba, n.k

Wa  mwisho mwenye haki kuliko wote na aliyepitia Mateso makuu kuliko wote ni BWANA WETU YESU KRISTO, Huyo alitemewa mate wazi wazi bila kosa lolote je wewe ambaye una dhambi ulishawahi kuchukiwa kiasi hicho cha kutemewa mate wazi wazi?!..yeye alisulibiwa akiwa tupu, je wewe ulishawahi kuchukiwa kiasi cha watu kufikiria kukuua kikatili kiasi hicho?

Kwahiyo kama unapitia mateso kwa ajili ya Imani yako nataka nikupe Moyo, Bwana atakuponya nayo yote, haijalishi ni siku ngapi, wiki, miezi au miaka mingapi itapita lakini siku moja utauona wokovu wa Bwana. Kama Bwana Yesu alivyouona wa Mungu kumfufua na kumweka juu sana zaidi hata ya Malaika.

Hivyo ukipitia mateso mtafakari Yesu,  yeye aliponywa nawe utaponywa!

Waebrania 12:2 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu”.

Ubarikiwe sana, Kama Hujampa Yesu Maisha yako, Ni vyema ukafanya hivyo kabla siku ya Unyakuo haijafika.


Mada Nyinginezo:

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

MNGOJEE BWANA

JE! MUNGU ANAUPENDELEO KWA WANAUME ZAIDI YA WANAWAKE?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Wanjiro
Wanjiro
1 year ago

Ujumbe huu umebariki moyo wangu sana na kunipa faraja kuu. Mungu akubariki na akuzidishie neema ya kuihubiri injili hii yake Yesu Kristo.