Bwana Yesu alikuja, akaondoka naye atarudi tena?
Swali ni je! atarudi kufanya nini?
Jibu: Atarudi kuitawala hii dunia pamoja na watakatifu wake, Biblia inasema dunia hii, enzi na Mamlaka amepewa Yesu na Mungu Baba…Mamlaka hayo, hapo mwanzo yalitoka kwa Mungu…akampa Adamu…Adamu akayapoteza, na shetani kuyachukua…Na alipokuja Yesu Kristo, shetani alinyanganywa mamlaka hayo na na kukabidhiwa Yesu Kristo. Hivyo ni lazima Kristo aje kutawala dunia..Kwasababu hakuna mamlaka yoyote isiyokuwa na Utawala.
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.
Na kama atakuja kutawala, wapo watu waovu wasioupenda utawala wake, hivyo hao atawaondoa..na wale wanaoupenda atawapa thawabu na nafasi za kutawala naye.
Ufunuo 2:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”
Ufunuo 2:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”
Kwa urefu jinsi utawala huo utakavyokuwa fungua somo hapa chini lenye kichwa kinachosema UTAMBUE UTAWALA WA MIAKA 1000
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
UTAWALA WA MIAKA 1000.
KATI YA UNYAKUO WA KANISA, DHIKI KUU, VITA VYA HAR-MAGEDONI, UTAWALA WA MIAKA 1000, VITA YA GOGU NA MAGOGU, HUKUMU YA KITI CHA ENZI CHEUPE. JE, NI KIPI KINAANZA NA KINGINE KUFUATA?
BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?
JE! WATAKAOENDA MBINGUNI NI WENGI?
Rudi Nyumbani:
Print this post