NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

Tunasoma mara baada ya Bwana Yesu kuwatuma wanafunzi wake wengine 70 wawili wawili wamtangulie kila mahali alipotaka kwenda, na kuwapa amri ya kufanya ishara zote alizokuwa anafanya yeye, walipotii na kwenda kuhubiri kwa furaha na kurudi kumpa Bwana ripoti ya mambo yote yaliyotendeka huko…Wao Hawakujua ni kitu gani Bwana Yesu alikuwa anaona huku nyuma, pengine wao kwa nje walikuwa wanaona ni jambo la kawaida tu, wanatimiza wajibu wao uwapasao kufanya, lakini Bwana Yesu aliwafumbulia alichokuwa anakiona aliwaambia maneno haya:

Luka 10:17 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.

18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”.

Unaona yaani kwa jinsi walivyokuwa wanalisambaza lile Neno la Mungu na kuiangaza nuru ya injili kila mahali, huku Nyuma shetani alikuwa anaanguka kwa kasi ya ajabu sana mfano wa Umeme/radi, hakuna kitu kinachosafiri kwa kasi zaidi ya umeme, hivyo hapo Bwana alipokuwa anasema nilimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme, alimaanisha ni anguko ambalo halikuwa na kipingamizi chochote kile (flawless). Leo hii shetani anaweza kuleta vipingamizi katika maombi, anaweza ukaomba lakini bado shetani akabakia pale pale ameshikilia..Lakini kwa pamoja tunapoamka na kwenda kuhubiri injili ya Kristo kila mahali, anajua hawezi kubaki pale pale, ni lazima aanguke tu, na ndio maana jambo kubwa ambalo shetani analipiga vita kuhubiri injili.

Kumbuka kibiblia mbinguni sio tu, kule Mungu alipo, mbinguni inaweza ikawa nafasi ya juu sana, ambayo kimsingi ndio inayompasa Mungu peke yake aikalie, lakini wanadamu au shetani wanaweza kutafuta nafasi hiyo kwa nguvu na kuketi hapo, na hivyo rohoni wakaonekana kama wamefika mbinguni. Soma Danieli 4:9-37, soma pia:

Isaya 14:13 “Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.

14Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.

15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.

16 Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;

17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?

18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;”

Ikiwa wewe umeokoka na umekaa katika hali hiyo kwa miezi sasa, au miaka, na hutaki kuangaza nuru ya injili kwa wengine ili na wenyewe waokoke kama wewe, hutaki kuitumia karama Mungu aliyoiweka ndani yako kumtangaza yeye na huku unamwomba Mungu watu waokolewe nataka nikuambie shetani atendelea kuwatesa tu..Usitegemee kuwa shetani ataondoka kwenye jamii unayoishi, usitegemee huyo mkuu wa giza ataacha aliye katika eneo lako ataacha kuwapufusha watu macho wasiiamini Injili..Ataendelea sana kuziangusha roho za wengi…

Unadhani mapepo hayo yatadondoka kwa maombi tu?…Bwana Yesu hakuwaambia kauli ile walipotoka kusali, lakini aliwaambia kauli ile walipotoka kuhubiri..Vivyo hivyo na wewe, leo hii usipozaa matunda utafika wakati Bwana atakukata, unaposikia injili Mungu anatazamia na wengine waisikie hiyo hiyo uliyoisikia kwa kupitia wewe..Lakini kama wewe utakuwa ni kupokea tu hutaki kutoa ili na wengine waokolewe, wakati utafiki utakatwa.

Popote pale ulipo unaweza kuwahubiria wengine injili, iwe ni kazini, iwe ni shuleni, iwe ni mtaani, iwe ni nyumbani, iwe ni mitandaoni, iwe ni safarini, iwe barabarani..Kwa karama Mungu aliyokupa na mlango aliokufungulia itumie hiyo hiyo kumletea Kristo faida..Tukishirikiana kwa pamoja, hakuna nguvu yoyote ya shetani itakayoweza kuzuia watu wasimjue Mungu, yeye kazi yake itakuwa ni moja tu, kila sekunde ni kuanguka huko aliko kwa kasi ya umeme. Kuhubiri Injili ni moja ya zile silaha zilizotajwa katika..

Waefeso 6: 13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani”

Unapowahubiria wengine wokovu, unammaliza shetani na upande wa pili.

Ni maombi yangu utafanya hivyo kuanzia huu wakati. Bwana akubariki…

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP




Mada Nyinginezo:

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

INJILI YA MILELE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments