SWALI: BWANA YESU ASIFIWE SANA ndugu zangu..naswali naomba kujua BWANA alikuwa anamaana gani kusema haya maneno…Mathayo 5:13 ‘Ninyi ni chumvi ya dunia;lakini chumvi IKIWA IMEHARIBIKA ITATIWA NINI HATA IKOLEE?….’
JIBU: Bwana Yesu alitumia mfano wa chumvi kuonyesha jinsi watakatifu wanavyopaswa wawe waangalifu hapa duniani..Chumvi ni kama sukari, hata siku moja hujawahi kuweka sukari kwenye chai na ukakutana na kipande cha jiwe ndani yake, tofauti na vitu vingine kama vile mchele, au maharage ambavyo utakutana navyo sana, vivyo hivyo na chumvi nayo inapotengezwa, huwa inatengenezwa kwa umakini wa hali ya juu sana, kuhakikisha kuwa hakuna uchafu wowote unajipenyeza ndani ya chumvi ile..
Kwasababu wanafahamu chumvi ni tofauti na nafaka, ikiingia uchafu kidogo tu, basi haifai tena ni ya kutupa, ni kitu ambacho kisichoweza kuchambulika kama vile mchele, huwezi ukatoa punje moja moja ya chumvi uitenganishe na uchafu, hiyo haiwezekani, ikiingia uchafu kidogo tu, basi hiyo haifai tena, hata kamaa ukijaribu kuiweka katika mboga haiwezi kukolea kwa namna yoyote ile.
Vivyo hivyo na sisi tuliookoka, Bwana anasema ni chumvi, hatupaswi kutiwa unajisi na kitu chochote kichafu, kwasababu ulimwengu unatuangalia sisi kama viungo vya kipekee sana, na ndio maana hata leo ukisikia watu wawili wamefumaniwa katika uzinzi na mmojawapo ni mchungaji, utaona watu wote wanaacha kumfuatilia yule mwingine, na kuanza kufuatilia habari za yule mchungaji,..
ni kwasababu yeye alikuwa ni chumvi, lakini sasa ameshatiwa doa, unadhani mtu kama huyo hata kama akitubu kwa dhati kabisa, na Mungu kweli akamsamehe, Unadhani ile jamii inayomzunguza bado itamwelewa?, haiwezekani tena, utumishi wake ndio tayari umeshaharibika hivyo..
Na ndio maana Bwana anasema “chumvi ikiwa imeharibikaitatiwa nini hata ikolee?”, Wewe unasema umeokoka halafu bado unaonekana unatukana ovyo, utumishi wako utaaminikaje mbele za watu?, Unakwenda Disco, au muda wote wewe ni kusengenya watu, unadhani wale watu wanaokuzunguka watakuaminije hata kama utawapelekea habari za Mungu..
Waefeso 5:25 “……….kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”.
Hivyo hapo Bwana alikuwa anatuonya tuwe waangalifu, sisi ni chumvi, tuliotakaswa siku ile tulipookoka tusio na hila wala waa wala, kunyanzi lolote, na sio mchele ambao hata ukiingia uchafu unaweza kuchambulika.
Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/je-ni-vema-kwa-mkristo-kwenda-hospitali-au-kutumia-miti-shamba-anapougua/
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
About the author