ASKOFU MKUU NA MCHUNGAJI MKUU NI NANI?

ASKOFU MKUU NA MCHUNGAJI MKUU NI NANI?

Sasa hivi kuna madhehebu mengi duniani, na yanazidi kuongezeka kwa kasi. Madhehebu karibia yote yana Maaskofu na wachungaji…Na pia yana maaskofu wakuu…Ndio utasikia mahali fulani Askofu Mkuu wa kkkt anatajwa, askofu mkuu wa roman katoliki, askofu Mkuu wa fpct, Askofu Mkuu wa eagt, Askofu Mkuu wa Anglikana, Nabii Mkuu wa huduma fulani, Mwalimu Mkuu n.k

Je Hekima inasemaje juu ya vyeo hivi?

Vyeo hivi kwa Hekima ya kibinadamu havina tatizo lolote..kwasababu hata katika ngazi za uongozi wa nchi kunakuwa na Mkuu wa Nchi, na kisha wapo walio chini yake n.k Ili kuwepo na uongozi unaosimama na ulio katika utaratibu Mzuri ni lazima ngazi ziwepo, mmoja awe juu ya mwingine kiukuu.

Hekima ya KiMungu inasemaje?

Lakini tukirudi katika Hekima ya KiMungu, Jinsi uongozi wa KiMungu unavyojiongoza ni tofauti na wa kiulimwengu…Huwa inatumika Hekima nyingine tofauti kabisa na hekima ya ulimwengu huu.

Uongozi wa kiMungu hautumii ngazi za ukuu, kwamba mmoja anakuwa mkuu kwa mwingine bali unatumia kitu kinachoitwa KARAMA ZA ROHONI. Kumbuka ni za rohoni na si za mwilini…. Na  karama hizi za rohoni hazina mtu aliye Mkuu kuliko mwingine au aliye Mkuu wa Mwingine. Ni kwanini? kwasababu vyote vina umuhimu sawa na vyote ni vikuu katika mwili wa Kristo. 

Mtume Paulo alizilinganisha karama za rohoni na viungo vya Mwili, na kwa uwezo wa Roho akaonyesha kuwa viungo vyote ni vya muhimu na hakuna kilicho kikuu zaidi ya kingine kwasababu vyote vimeshikamana …Kiungo kilicho kikuu zaidi ya vingine vyote ni Kichwa tu! ambacho hicho Biblia ndio imesema ni KRISTO, lakini vilivyosalia vyote hakuna kilicho kikuu zaidi ya kingine.

Na ni kwanini kichwa ndio kiungo kikuu kuliko vyote?

Ni kwasababu ndio kiungo pekee kinachoongoza viungo vyote vya mwili, taarifa za kunyanyua mkono zinatoka kwenye kichwa (yaani ubongo), taarifa za kusogeza mguu zinatoka kwenye kichwa na sio kwenye mikono…Hivyo mkono hauwezi kuwa mkuu juu ya mguu…n.k

Kumbuka Laiti vipawa hivi visingekuwa ni vipawa vya rohoni, na kuwa vipawa vya mwilini, basi ingekuwa ni sawa kuwepo na Askofu Mkuu, au Mchungaji Mkuu au Nabii Mkuu, au Mwalimu Mkuu au kiongozi mkuu…lakini kwasababu sio vya mwilini hivyo sio sawa kuvigawanya na kusema kimoja ni kikuu kwa vingine mkono hauwezi ukauamrisha mguu utembee.. Kwahiyo Askofu anayejiita ni Mkuu kwa askofu mwenzake, anafanya jambo lililokinyume na maandiko….Huko ni kujikuza na kuchukua nafasi ya Kristo.

Biblia inasema.

1Wakorintho 12:11 ‘lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo’….

14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.

15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?

16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?

17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.

21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.

22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.

23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.

24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;

Hebu leo hii, mtu ambaye anajiita Askofu Mkuu, mwingine akosee tu kidogo na kumwita Askofu bila kuongezea hapo mbele neno ‘Mkuu’ uone atakavyowaka au kukasikira…Sasa hasira hizo za nini? kama kweli huyo hana nia ya kutafuta ukubwa?. 

Kwahiyo Askofu Mkuu ni nani?

Ni Yesu Kristo peke yake, Nabii Mkuu ni Yesu Kristo peke yake, Mwalimu Mkuu ni Yesu Kristo peke yake, sisi tukijiita walimu, au wachungaji au maaskofu au manabii inatosha! zaidi ya hapo ni kinyume na maandiko!

Waebrania 13:20 “Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu”

Ubarikiwe.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

DANIELI: Mlango wa 1

DANIELI: Mlango wa 10

UMEPATANISHWA NA MAADUI ZAKO?

YUDA ISKARIOTE! MTUME ALIYECHAGULIWA NA BWANA YESU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Paul
Michael Paul
10 months ago

Nimejifunza kitu hapo,uliyaongea ni kweli kabisa,utakuta mtu kama ana cheo lazima mwishoni aweke “MKUU” hata kama si kiongozi wa kanisa na wakati wanakosea.Barikiwa sana kwa somo hili zuri.