Kwanini Musa alipewa mbao mbili za mawe na sio moja au zaidi

Kwanini Musa alipewa mbao mbili za mawe na sio moja au zaidi

SWALI: Tukisoma Kutoka 34:1-5 Tunaona Musa anaambiwa atengeneze mbao mbili za mawe mfano wa zile za awali. Sasa swali ni kwanini ziwe mbili na sio moja au Zaidi? Na ni kwanini ziwe mbao za mawe. Je kuna ufunuo wowote kuhusu hilo?


KWANINI ZILICHONGWA KWENYE MAWE.

Sababu kuu ya Mungu kuzichonga kwenye mawe na si penginepo ni kuonyesha uthabiti na ubora wa sheria zake., kumbuka kitu chochote kinachochongwa katika mwamba ni tofauti na kile kinachochorwa katika karatasi au kinachochongwa katika ubao..Mwamba wakati wote ni mgumu hivyo hata kile kinachochonga kitahitaji jitihada Zaidi katika kuchongwa, Japo inatumia nguvu zaidi na gharama lakini faida yake mwisho wa siku inakuwa ni kubwa, nayo ni UBORA..tofauti na  kile kinachochorwa katika katarati ambapo kifuto kikipita kidogo tu maandishi yale yanafutika na kazi yote inakuwa bure, au kile kinachochorwa  katika mbao ambacho nacho pia moto kidogo tu ukipita kazi yote inateketea na kumbukumbu lote kufutika….Lakini mwamba hata moto ukipita, ndio kwanza inazidi kuwa imara Zaidi, Na ndio maana utaona baada ya pale zile mbao mbili za mawe zilidumu kwa maelfu ya miaka mbeleni..

Kufunua kuwa upo ubao ulio mgumu Zaidi ya mwamba, ambapo Mungu aliuweka tayari huko mbeleni kuandika amri zake zisizoweza kufutika milele..na ubao huo si mwingine Zaidi ya moyo wa mwanadamu, huo ni bora Zaidi ya mwamba wowote duniani…Mungu akishaandika sheria  zake ndani ya mwaminio, haziwezi kufutika tena milele, wala kupotea, kama ilivyokuwa katika agano la kale watu walikuwa wakizisahau sahau mpaka wakumbushwe vilevile vibao vile vilikuja kupotea baadaye na wala kumbukumbu lake halijulikana lilipo mpaka leo…

Lakini biblia inasema..

Yeremia 31:31 ‘’Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena’’.

Soma pia..

Waebrania 10:16  ‘’Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo’’,

Unaona huo ndio ubora wa agano jipya..Sheria ile inaandikwa juu ya vibao vya mioyo yetu kwa sisi tulioamini isiyoweza kuharibiwa au kufutwa na mtu yeyote milele.. Hivyo kama wewe upo nje ya Kristo, mlango wa neema bado upo wazi, lakini hautakuwa wazi hivyo milele..Mkaribishe leo ndani ya maisha yako, kwa kutubu na kuacha dhambi zote, kisha baada ya hapo ataanza kukutengeneza na sheria yake ataiandika moyoni mwako, na wala dhambi haitakushinda milele, kwasababu sheria hiyo imechorwa ndani ya vilindi vya moyo wako asipoweza mtu wala shetani kuifikia na kuifuta…sheria hiyo itakulinda mpaka siku ile ya kwenda mbinguni katika Unyakuo.

Tubu dhambi zako sasa, nawe uufurahie wokovu, na neema ya bure ya BWANA YESU.

NA JE! KWANINI ZIWE MBAO MBILI ZA MAWE NA SI PUNGUFU AU ZAIDI?

Fahamu kuwa zile amri kumi za Mungu ziliganyika katika mafungu makuu mawili, la kwanza ni Upendo kwa Mungu wetu, na la pili Ni upendo kwa jirani zetu kama nafsi zetu..Hakuna shaka zile nne za kwanza zilikuwa katika ubao mmoja unaojitegemea ambazo zinamuhusu Mungu, na zile sita za pili zilikuwa katika ubao wa pili ambazo zinatuhusu sisi, …

Na hiyo ndio mihili mikuu miwili  hata katika agano jipya ambayo tunapaswa tutembee nayo, hizo ndizo mbawa zetu mbili tunapaswa turuke nazo kila siku, ya kwanza ni hiyo ya kumpenda Mungu, ambapo tukimpenda Mungu tutafanya yote anayotuagiza, na ya pili ndio hiyo tuwapende jirani zetu kama nafsi zetu tukiwapenda ndugu tutasitiri wingi wa dhambi, na kila tendo ovu dhidi ya majirani zetu na jamii kwa ujumla….Hatuwezi kuruka na mbawa mojawapo katika ya hizo, bali zote mbili zinakwenda pamoja..

Ubarikiwe sana..jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

FIMBO YA HARUNI!

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments