KITABU CHA UCHAWI.

KITABU CHA UCHAWI.

Kabla ya kutafuta kitabu cha uchawi ni vizuri kufahamu kwanza Uchawi asili yake ni wapi.

Wapo watu wengi mitandaoni, wengine ni wachawi kweli, na wengine ni matapeli, wameandika vitabu wanakuambia ununue, na katika vitabu hivyo, wanaorodhesha njia mbalimbali za kutatua matatizo yako, au njia za kuwapiga maadui zao.. Lakini kabla hujafikiria kuungana nao ndugu yangu, ni vizuri kwanza ukafahamu uchawi asili yake ni wapi?

Uchawi ni kitendo cha kwenda kutafuta msaada kutoka katika mamlaka mengine tofuati na yale ya Mungu  ili kutimiziwa malengo Fulani, ya mwilini au rohoni. Na kama tunavyofahamu hakuna mamlaka mengine yaliyo tofauti na Mungu zaidi ya yale ya shetani.

Kwamfano, unapokuwa na uhitaji labda wa mke, na unaona kwa akili zako huwezi kumpata mwanamke umtakaye, hapo inakugharimu kutafuta msaada kutoka katika mamlaka nyingine..

Ndio hapo yanazuka mambo mawili, aidha uende kwa Mungu, au uende kwa shetani, ukienda kwa shetani utapata maagizo Fulani, yanatoka katika kitabu cha kichawi walichonacho, Vivyo hivyo ukienda kwa Mungu utapokea maagizo kutokana na kitabu kitakatifu cha Mungu kiitwacho BIBLIA.

Lakini jambo ambalo watu wengi hawajui ni kuwa, shetani hana lengo lolote zuri  na mwanadamu zaidi ya kumwangamiza, atakupa kwa lengo la kukuangamiza mwisho wa siku, na ukishakufa ni moja kwa moja unakwenda katika moto wa milele..

Zipo shuhuda nyingi za watu waliokwenda kwa waganga, kutafuta msaada wa shetani, lakini mwisho wake wameishia pabaya sana.. Na kibaya zaidi ulimwengu huu wa sasa, watu wengi wanakimbilia humo hawajui kuwa lile ni shimo kubwa sana la mauti..Ambalo ukiingia kutoka huko ni kugumu sana.

Usihatarishe maisha yako, kwa mambo ambayo hayakupeleki popote, Usije ukasema haujaambiwa, kukutana na ujumbe huu ni makusudi kabisa Mungu anakuonya, ikiwa wewe ni mmojawapo unayetafuta kujui kitabu cha uchawi, hizi ni siku za mwisho, biblia inasema hivi..

1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”

Unaona, biblia inasema wengi watajitenga na Imani na kusikiliza mafundisho ya mashetani,..Kumbuka Uchawi wa kwanza kabisa ulifanywa na Shetani pale Edeni, Ukitaka kujua uchawi wenyewe ni upi na madhara gani yalitokea baada ya pale..fungua hapa usome..>>>> JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

Na ndio maana hata katika Israeli Mungu alipiga kabisa marufu watu wanaofanya uchawi, kwasababu alijua madhara yake kwao.

Kumbukumbu 18:9 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako”.

Hivyo ndugu, usifirie kutafuta eti hicho kinachoitwa kitabu cha uchawi, Ni heri utubu dhambi zako leo umgeukie YESU KRISTO, haijalishi wewe utakuwa ni muislamu, au mhindu, vyovyote vile, ukimpa Yesu maisha yako leo atakuokoa na kukupa uzima wa milele. Na atakupa pia vile vitu ambavyo ulikuwa na haja navyo kwa wakati wake.

Hivyo kama upo tayari leo kufanya hivyo, na unahitaji kuyakabidhi maisha yako kwake, basi fungua hapa kwa ajili ya sala ya Toba na Mungu akubariki..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Pia unaweza pia kufungua na masomo mengine hapa chini ujifunze, naamini yatakutoa sehemu moja hadi nyingine kiroho.

Mada Nyinginezo:

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ukristo wenyewe tu ni ushirikina tosha ww uliye chapisha andiko hili uko ndani ya shirk rudi kwa allah

Fidelice makio
Fidelice makio
2 years ago

ningependa kuwa na miujiza ya kugeuza nina cho taka

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Leave your message

Peter chalawe
Peter chalawe
3 years ago

My WhatsApp does not respond