Swali: Sabato tatu ni nini? Kama tunavyosoma katika Matendo 17:2
Jibu: Tusome,
Matendo 17:1 “Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko SABATO TATU,
3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo”.
Mstari huo haumaanishi kwamba kuna aina tatu za sabato au sabato zipo tatu. Hapana, bali unamaanisha Sabato tatu mfululizo.
Kwamfano tafakari hii sentensi.. “Yohana baada ya kuokoka alihudhurua kanisani JUMAPILI TATU mfululizo za mwezi uliopita”. Sasa hapo simaanishi jumapili zipo za aina tatu, bali namaanisha ni jumapili za majuma matatu. Ndivyo Paulo alichomaanisha hapo katika sabato tatu. Maana yake kwa sabato tatu mfululizo aliingia hekaluni kuhojiana nao kwa maneno ya maandiko.
Sasa unaweza kuuliza je! kwa mantiki hiyo na sisi tunapaswa tuishike sabato?
Jibu ni la! Sabato halisi katika agano jipya sio siku moja maalumu, bali ni kila siku ya maisha yetu tunayoishi, sasa kwanini hapo Paulo aingie kuhojiana nao wakati wa sabato?. Ni kwasababu kwa wakati huo wayahudi (yaani waisraeli), walikuwa bado wana desturi ya kuishika sabato. Hivyo siku pekee ya kuweza kukutana nao ni siku ya sabato katika masinagogi yao, siku nyingine zozote wasingeweza kupatikana ndio maana hapo Paulo alikwenda kukutana nao katika siku yao ya kuabudu.
Ni sawa leo utafute namna ya kuwapata watu wa dini Fulani kuhojiana nao kuhusu imani, huwezi kuwapata nje na ile siku yao wanayokutana kuabudu. Kama ni ijumaa, au jumamosi au jumapili, au siku nyingine yoyote ile, sasa kitendo cha wewe kuwafuata ili uwashuhudie katika siku yao ya Ibada haimaanishi kwamba na wewe umeihalalisha siku ile.
Kufahamu zaidi kuhusu Sabato halisi ni ipi, mwisho wa somo hili chini kabisa utaona orodha ya mada hizo zinazohusiana na sabato, zifungue uzisome.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
About the author